Kutotafautisha kati ya asili na taw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutotafautisha kati ya asili na tawi ni miongoni mwa kuathirika na fikra za Khawariji wenye itikadi kali

Question

Kwa nini kutotafautisha kati ya asili na tawi ni miongoni mwa kuathirika na fikra za Khawariji wenye itikadi kali?

Answer

Miongoni mwa sifa mbaya zaidi za Khawariji ambayo wametofautiana nayo na watu wa Sunna na Jamaa ni kuwakufurisha wenye kutenda dhambi, na tunakusudia kwa hiyo dhambi kwenda  kinyume na matawi, sawasawa madhambi makubwa, kama kuacha Swala ya Faradhi, kula mchana wa Ramadhani, au madhambi madogo kama kusikiliza usengenyi au kusalishwa watu na wanayemchukia. Elimu ya Fiqhi ni elimu inayojihusisha na kuchunguza matawi ya dini, na Muislamu kwa madhehebu ya watu wa Sunna na Jamaa hakufurishwi isipokuwa baada ya kuhakikisha kuwa amepinga asili miongoni mwa asili za dini, kama kupinga umoja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Kadhi ndiye anayesimamia hilo kisha anatoa hukumu, na elimu inayohusiana na tafiti za Misingi ya dini ni elimu ya Akida, lakini wenye itikadi kali wanaijumuisha moja kwa moja baadhi ya masuala ya matawi kwa Misingi ya dini, kama kutawasuli kwa Mawalii wema wa Mwenyezi Mungu, ni jambo linalopendeza na linalojuzu kwa Wanazuoni wa Fiqhi wa madhehebu manne, na wenye itikadi kali hawakutosheka na kwenda kinyume na Jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi kwa kusema kuwa Tawssul ni Haramu kwa mfano, bali wamekufurisha wanaotawasuli kupitia kwa mmoja ya mawalii wa Mwenyezi Mungu! Na kwa hili wakaitwa Khawariji wa zama za sasa.

Share this:

Related Fatwas