Kuchanganya maana ni miongoni mwa m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchanganya maana ni miongoni mwa majanga makubwa ambayo yameikumba jamii

Question

Kwa nini Kuchanganya maana ni miongoni mwa majanga makubwa ambayo yameikumba jamii? Na mifano gani inayobainisha hilo katika maisha? Na ni ipi athari ya hilo katika kuenea itikadi kali na ugaidi.

Answer

Kuharibu maana na kuzichanganya ni moja ya sababu kubwa za kuenea itikadi kali na ugaidi, mara nyingi watu wenye itikadi kali hutoa dalili kwa vitendo vyao vilivyopetuka mipaka kwa maana za Matini za Qur`ani na Hadithi ambazo ni makosa, miongoni mwazo kuelewa kwao kauli ya Mtume S.A.W.: “Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu…” [Imekubaliwa na wote] wanaelewa kwamba Waislamu wameamrishwa kuua wasiokuwa waislamu mpaka watakapoingia katika Uislamu! Na uelewa huu wa kimakosa na ambao hakuusema wala hakuufahamu yeyote katika Maimamu wa Waislamu, umeleta majanga makubwa, dogo kabisa ni kupatikana kwa picha mbaya na batili vichwani mwa watu kuhusu dini hii ya upole na huruma, na ukweli ni kwamba Mtume S.A.W. amesema: “nimeamrishwa…” ni maalumu kwake Mtume S.A.W. na haimuendei mwingine, na neno “nipigane vita…” inajulisha kitendo shirikishi, pande ya pili ndiyo inayoanza vita, kwani faradhi ya kupigana vita ilichelewa kwa zaidi ya miaka kumi na mitatu na “neno watu…”  ni wale waliokuwa wanampiga vita Mtume S.A.W. katika washirikina wa Maqurayshi na wengineo, hili ni neno linalokusanya lililokusudiwa umaalumu.

Share this:

Related Fatwas