Kwenda kwa hatua ni katika makusudio makubwa ya Sharia Takatifu
Question
Vipi makundi ya kigaidi huonesha Uislamu kwa wasio kuwa Waislamu
Answer
Makundi ya ukufurishaji hutegemea kuelezea Uislamu kwa wengine kwa kufuata mfumo wa uadui uporaji na uuwaji, hilo ni dhidi ya kila ambaye hajafuata mafundisho ya Uislamu ambayo wanayaonesha, na ambayo yanakubaliana na fikra zao, na huu ni mfumo usiokubalika Kisharia, kwani Mtume S.A.W. amebainisha mfumo sahihi wa kuelezea Uislamu na kuusambaza kwa watu, nao ni mfumo unaosimama kwenye msingi wa kwenda kwa hatua na upole pamoja na kulinda mali nafsi na heshima, tunakuta amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwa Muadhi Ibn Jabal akitakiwa kuchunga mambo haya, na hasa kwa kuzingatia hali za watu aliopelekwa kwao katika watu wa Yemen, ambapo walikuwa watu wa Kitabu wanatakiwa kuhama dini na kuelekea kwenye dini ya Uislamu ambayo ni mpya. Mtume S.A.W. akasema akimwelekeza kitu atanza nacho na kipi atamalizia na namna gani atafikisha akisema: “Hakika yako utaenda kwa watu wa Kitabu utawalingania kwenye kushuhudia kuwa hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na katika mapokezi mengine, liwe la kwanza kuwalingania ni kumwabudu Mwenyezi Mungu ikiwa watatii hilo basi wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha ibada ya Swala tano usiku na mchana, ikiwa watatii hilo wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu Amewalazimisha kutoa sadaka huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao, ikiwa watatii hilo, jiepushe na mali zao, na ogopa dua ya mtu aliyedhulumiwa kwani kati yake na Mwenyezi Mungu hakuna kizuizi” .