Kuipuuza Lugha ya Kiarabu na kuidha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuipuuza Lugha ya Kiarabu na kuidharau ni miongoni mwa milango ya kuingia kwenye itikadi kali kwa mwanadamu

Question

Kwa nini Wanazuoni wa Kiislamu wameilinda lugha ya Kiarabu? Na Kwa nini kuipuuza Lugha ya Kiarabu na kuidharau ni miongoni mwa milango ya kuingia kwenye itikadi kali kwa mwanadamu?

Answer

Lugha ya Kiarabu ni lugha Aliyoteremshia Qur`ani Mwenyezi Mungu, na aliyozungumza Mtume S.A.W. na kutoijua kunapelekea kutojua maana ya Qura`ni na Hadithi, na kuelewa vibaya makusudio ya maneno ya Mwenyezi Mungu, ndimi za watu zilipodhoofika na makosa ya kusoma kuwa mengi, Wanazuoni wa Kiislamu wakatilia umuhimu mno Lugha ya Kiarabu mpaka wakazigawa elimu za Lugha hiyo katika mafungu kumi na mbili au zaidi. Na kuna Matini (Maandiko) nyingi za Qur`ani na Hadithi ambazo ikiwa mtu hatakuwa anajua elimu ya Lugha ya Kiarabu na maana zake, basi zitampeleka kwenye itikadi kali, miongoni mwa Matini hizi ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu…” hakika dalili ya herufi Ti ya mtendaji katika neno Nimeamrishwa (Umirtu) na tofauti ya kilugha kati ya neno Aqtul (Niue) na Uqaatil (nipigane vita) na aina ya Lamu ya Maarifa katika neno (An-Nnas) watu, yote haya yanaweza kubadilisha maana moja kwa moja, kutoka Matini inayohalalisha haki ya kisharia kwa kawaida, nayo ni haki ya kujitetea, na kuwa Matini ya kumwaga damu inayoasisi fikra ya itikadi kali na ugaidi.

Share this:

Related Fatwas