Kushughulikia Turathi za Kifiqhi za...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushughulikia Turathi za Kifiqhi za zamani kwamba zote ni thabiti ni miongoni mwa sababu za kuingia katika fikra za Khawariji

Question

Kwa nini kushughulikia Turathi za Kifiqhi za zamani kwamba zote ni thabiti ni miongoni mwa sababu za  kuingia katika fikra za Khawariji?

Answer

Kuzingatia Turathi za Kifiqhi za zamani kwamba zote ni thabiti ni makosa makubwa, hukumu nyingi za kisharia zinaathirika sana kutokana na wakati na sehemu, hili wamekubaliana Wanazuoni wote, na sehemu na wakati zikiwa hazijatofautiana sana huenda zisiathiri Fatwa au hukumu ya kisharia kwa tofauti hiyo, hilo tunaweza kuligundua katika miaka elfu moja na mia mbili ya kwanza katika Uislamu, kukilinganishwa na mabadiliko makubwa ambayo yamezuka ulimwenguni baada ya mapinduzi ya mawasiliano na usafiri ambayo yameanza tangu karne mbili takriban. Mabadiliko hayo hayakubadilisha umbo la ulimwengu tu, bali yamekuja kwa kasi sana, jambo ambalo linawalazimisha Wanazuoni wa kila zama kuendana na mabadiliko hayo ya haraka ili kuendana na hukumu za Kifiqhi katika uhalisia wa kasi ya mabadiliko, jambo ambalo hawalijui watu wenye itikadi kali, kwani wao wanazingatia kuwa kuendena na mabadiliko mapya ni kutoka katika madhehebu ya watu wa zamani, na ukweli ni madhehebu hayo hayo, na dalili ya hilo ni kwamba wao wameenda kinyume na waliowatangulia kwa sababu ya mabadiliko ya hali zao.

Share this:

Related Fatwas