Nembo zenye mvuto na hotuba laini ni mingoni mwa sifa kuu za makundi yenye siasa kali katika Historia
Question
Kwa nini nembo zenye mvuto na hotuba laini ni miongoni mwa sifa kuu za makundi yenye itikadi kali katika Historia? Vipi Mtume S.A.W. ametahadharisha hilo?
Answer
Miongoni mwa tahadhari maarufu za Mtume S.A.W. kwa makundi yenye itikadi kali zilizokuja katika Hadithi, ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Watakuja watu zama za mwisho… wanasema Qur`ani, wanatoka katika Uislamu kwa haraka kama utokavyo mshale kwenye upinde..” [Imekubaliwa na wote], sifa zao zimekuwa kwamba wao ni watu wa ulinganiaji wenye uongo, na maneno yao yanatofautiana na vitendo vyao, na hii ndiyo sababu ya kushuka adhabu ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu zake kwa waja wake, Anasema Mwenyezi Mungu: “Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyoyatenda”[As-Saff, 2], hivyo Mtume S.A.W. alikuwa anamwuliza aliyebeba ulinganiaji kuhusu hali yake, imepokewa kutoka kwa Awf bin Malik kwamba yeye alimwambia Mtume S.A.W.: Nimekuwa Muumini wa kweli, akasema Mtume S.A.W.: “Hakika kila kauli ina uhakika, ni upi uhakika wa hilo?”… Awf alipomweleza Mtume S.A.W. kinachothibitisha ukweli wa ulinganiaji wake, Mtume akamwambia: “Umejua - au umeamini - basi ushikamane na hilo” [imepokelewa na Ibn Abi Shayba], mazingatio yapo kwenye vitendo na hali na si katika maneno.