Kusoma Al-Fatiha mwanzoni mwa mabaraza ya suluhu, na mabaraza ya elimu na Fatwa
Question
Ni ipi hukumu ya kusoma Al-Fatiha mwanzoni mwa mabaraza ya suluhu na mabaraza ya elimu na Fatwa?
Answer
Kusoma Surat Al-Fatiha mwanzoni mwa mabaraza ya suluhu, au mabaraza ya elimu na Fatwa, au mambo mengine muhimu - inajuzu kwa mujibu wa Sharia, na inazingatiwa miongoni mwa wema na mambo bora zaidi. Watu wema waliotangulia wamefanya na wakarithiwa bila pingamizi lolote. Walikuwa wakiisoma ili kutimiza mahitaji na kukamilisha kazi zote.