Maana ya kutawala kwa Mwenyezi Mung...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya kutawala kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Question

Nini maana ya kutawala kwa Mwenyezi Mungu kwenye Kiti chake cha enzi? Ndani ya kauli ya Mola Mtukufu:  {Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi} Twaha: 05.

Answer

Katika imani thabiti kwa Waislamu ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hajumuishwi sehemu wala kuzuiliwa na wakati, kwa sababu sehemu na wakati vimeumbwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hawezi kuzungukwa na chochote katika alivyoviumba, bali Yeye ndio Muumba wa kila kitu, naye ni mwenye kukizunguka kila kitu, na imani hii imekubalika kwa Waislamu hakuna yeyote mwenye kupinga hilo, watu wa elimu wamelezea hilo kwa kauli yao: Mwenyezi Mungu amekuwa hana sehemu, naye yupo kama alivyo kabla ya kuumba sehemu, hajabadilika vile alivyokuwa.

Ama yaliyokuja katika Qur`ani na Sunna miongoni mwa Maandiko yanayonesha kuvuka kiwango kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, kusudio lake ni kuvuka kiwango cha nafasi utukufu utawala na nguvu, kwa sababu Mola Mtukufu amepukana na kufanana na waja wake, na wala sifa zaka si kama sifa za viumbe zenye upungufu, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye sifa za ukamilifu na uzuri wa majina, na kila unachofikiria akilini mwako Mwenyezi Mungu yu kinyume na hivyo, kushindwa kufikia uelewa ni uelewa, na kutafiti namna Mwenyezi Mungu alivyo ni kumshirikisha.

Aliwahi kuambiwa Yahya Ibn Muadhi Ar-Razy: Tuelezee kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: Ni mola mmoja, akaulizwa:  Yupo vipi? Akasema: Ni Mmiliki Mwenye uwezo, akaulizwa: Yupo wapi? Akasema: Pa kuchunguzwa, muulizaji akasema: Sijakuuliza kuhusu haya, akajibu: Majibu yasingekuwa haya angekuwa na sifa za viumbe, ama sifa yake hakuna aliyeielezea.

Share this:

Related Fatwas