Hukumu ya Kuotesha Nywele.
Question
Nini hukumu ya kuotesha nywele za asili?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kitendo cha kuotesha nywele ikiwa nywele zitaendelea kudumu kama vile nywele asili basi hakuna ubaya wowote na wala hakizingatiwi kama ni udanganyifu, ama zikiwa nywele zinaota kwa muda mfupi halafu zinatoka tena, basi hukumu yake ni sawa na nywele bandia; hasa zikikusudiwa udanganyifu na hadaa katika posa kwa mfano au kuvutia wanawake ili kuingia kwenye madhambi basi ni haramu kisharia. Ama ikiwa kwa nia nzuri mbali ya hayo basi si haramu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
