Hukumu Ya Kuvaa Mawigi

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu Ya Kuvaa Mawigi

Question

Je, inajuzu katika Uislamu wanaume na wanawake kuvaa wigi kamili au nusu wigi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hakuna ubaya kufaa wigi ilimradi zisiwe na udanganyifu na hila. Hii inaeleweka kutokana na sababu ambayo mwenye kuunganisha nywele na yule mwenye kuunganishwa nywele wamelaaniwa kwa sababu hiyo. Pia ikiwa hakuna fitna na ushawishi wa kuvutia wanaume wa watu wasio Mahram. Baadhi ya Hadithi zinaonesha kuwa hii ndiyo ilikuwa sababu ya kuangamizwa kwa Wana wa Israili pale wanawake wao walipoichukua na walipodanganya watu kwa kujipamba katika mikusanyiko ya watu na mahekalu, kama ilivyosimuliwa na Al-Tabarani.

Kwa mujibu wa Madhehebu ya Imamu Ash-Shafi, kuunganisha nywele ni haramu ikiwa zimetengenezwa kwa nywele za binadamu au nywele za mnyama najisi. Hata hivyo, ikiwa zimetengenezwa kwa nywele twahara, kama vile nywele za kondoo au nyuzi za viwandani, zinaruhusiwa ikiwa zimefanywa kwa idhini ya mume. Baadhi ya Wanachuoni wameruhusu uvaaji wa wigi za asili chini ya masharti mawili: kwamba pasipo na udanganyifu au ushawishi; yaani ikiwa imefanywa kwa ujuzi na idhini ya mume, na ikiwa haitumiki kwa asiyekuwa yeye. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas