Hukumu ya Masanamu yaliyo Uchi
Question
Je, ni ipi hukumu ya kisheria kuhusu kutumia Masanamu yaliyo uchi katika vyuo vya sanaa, ambapo huchorwa au kutengenezwa sanamu ya mtu aliye uchi kabisa — iwe ni mwanaume au mwanamke aliyeacha kufunika sehemu za siri — au nusu uchi kwa kisingizio cha kujifunza uwiano wa mwili wa binadamu au kuhisi maumbo yake? Je, inaruhusiwa kutumia masanamu inayofananishwa na mwanadamu aliye uchi kwa madhumuni haya, au ni haramu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hakika Mwenyezi Mungu Amemtukuza mwanadamu kwa jinsia zote mbili wa kiume na wa kike, Akamtunza na udhalilifu na uovu, Amesema (S.W.): {Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada...} [Al-Araaf: 31], na Amesema: { Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. [Al-Ahzaab: 59], na katika surat ya An-Nuur Amesema (S.W.): { Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} [An-Nuur: 30-31].
Na Sunnah Tukufu imebainisha kwamba si halali kwa mwanamume Mwislamu kuvua nguo zake hadi sehemu zake za siri zionekane, nazo ni kati ya kitovu na magoti ya mwili wake. Na si halali kwa mwanamke, anapofikia utu uzima kisharia kwa kupata hedhi au kufikia umri wa balehe, kuvua nguo zake isipokuwa mbele ya mume wake tu. Hakika si halali kwa maharimu wake kama baba, mwana au ndugu wa kiume kumwona kati ya kitovu chake na magoti. Hii ni haki ya mume wake peke yake, kama inavyoelezwa wazi katika aya tukufu za Qur’ani. Na imepokelewa na Abu Dawud kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), kwamba Asmaa bint Abu Bakr (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S. A.W.) akiwa amevaa nguo nyepesi, Mtume (S.A.W) akamgeukia na kusema: "Ewe Asmaa, mwanamke anapofikia hedhi, haifai kuonekana katika mwili wake isipokuwa haya," na akaashiria kwenye uso wake na viganja vya mikono yake.
Kwa ajili hii, wanazuoni wengi wa fiqhi (Ijma’a) wameafikiana kwamba si halali kwa mwanamke kuonyesha mwili wake mzima, na kutazamwa na wengine isipokuwa uso na vidole vya mikono. Kulikuwa na tofauti kuhusu miguu, ikiwa ni sehemu ambayo haifai kuonyeshwa au ni sehemu inayoruhusiwa? Imam Ahmad Ibn Hanbal alisema kwamba si halali kwa mwanamke kuonyesha mwili wake kwa mtu mwingine isipokuwa kwa wale waliotajwa katika aya ya mwisho. Hii ni hukumu ya Mwenyezi Mungu aliyoiteremsha katika Kitabu chake na kwa ulimi wa Mtume wake (Rehema na Amani ziwe juu yake). Kwa hivyo, kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, si halali kwa mwanamke kuondoa nguo zake kabisa au sehemu zake, wala si halali kwa mwanaume kuvua nguo zake mpaka sehemu zake za siri (kutoka kitovuni hadi magotini) ziwe wazi, isipokuwa tu kwa dharura kama vile matibabu kwa msaada wa daktari. Lakini nje ya dharura, hakuna kilichoruhusiwa, na si dharura hili la kutumia mfano wa mwanamke au mwanaume alie uchi kwa madhumuni ya sanaa au uchoraji, kwa sababu hakuna dharura hiyo.
Mchoraji anaweza kujitolea kuchora maua, miti, na vitu vingine ambavyo Mwenyezi Mungu amevihalalisha kwa waja wake, na katika hivyo kuna uzuri ambao hauwezi kulinganishwa na mwili wa binadamu akiwa uchi. Kwa kweli, Mwenyezi Mungu alimtunza Adam na Hawa kwa kuwalinda miili yao alipowaumba, na aliwakataza kula kutoka kwenye mti na akawakanya kwa kosa lao la kula kwao kwa kudhiirsha uchi wao. Hivyo ndivyo inavyoweza kueleweka katika neno "Saw’a" ambalo linaonyesha ubaya wa kutazama kile ambacho Mwenyezi Mungu ameagiza kifichwe kisionekane na macho ya watu. Kwa sababu hiyo, si halali kisharia kumvua mwanamke nguo zake au kumvua mwanaume kile kinachoficha kilicho kati ya kitovu na magoti isipokuwa kwa dharura ya matibabu na kutumia dawa pekee. Na ni haki ya wazazi na walezi - sisi tunajenga taifa letu kwa maadili mema katika uwanja wa elimu na imani – kuinua haiba, na kuonyesha Utukufu wa uumbaji wa Mungu katika kile alichohalalisha na si kile alichokataza. Na kila mmoja atakumbuka maneno ya Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) yaliyopokewa na An-Nasa’i na Ibn Hibban katika Sahihi kutoka kwa Anas, amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu atamwuliza kila Mchungaji katika kile alichokichunga: Je, alikihifadhi au alikipoteza? Hata atamwuliza mwanaume kuhusu familia yake”.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
