Hukumu ya Kurefusha Nywele kwa Wanaume
Question
Nimeona Waislamu wengi wenye nywele ndefu sana. Je, hiyo ni sawa au si sahihi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mtume (S.A.W) alikuwa na nywele ndefu ambazo pengine zilifika mabegani mwake. Nywele ndefu zake mwenyewe zenyewe hazikatazwi isipokuwa kama ni ishara ya uasherati, uovu, au ushoga. Huenda kitu kikawa chenye kudekezwa, lakini kikiwa ni ishara ya tabia ya dhambi, basi ni haramu. Wanachuoni wamesema hata kuvaa nguo nyeupe ni Sunna, likini itakapokuwa ni alama ya uchafu, katika hali hiyo ni haramu. Imethibitika kwamba mambo ya mapambo na mavazi yanatawaliwa na mila na desturi na yanatawaliwa na kanuni za jumla: kama vile wajibu wa kusitiri sehemu za Uchi, kukataza kujifananisha na watu wachafu na waovu, kukataza wanaume kujifananiza na wanawake na wanawake kujifananiza na wanaume, na kuharamishwa kibri, kujikweza, na kufanya ubadhirifu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
