Hukumu ya Kuvaa Dhahabu Nyeupe kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuvaa Dhahabu Nyeupe kwa Wanaume

Question

Nina pete mbili za Ndoa za dhahabu ya manjano, na nilijua kwamba dhahabu ya manjano ni haramu kwa wanaume, kwa hiyo nitatengeneza pete mbili nyingine, lakini swali langu sasa ni: Je, pete zinazotengenezwa kwa dhahabu nyeupe ni haramu kwa wanaume?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Jina la Dhahabu nyeupe huitwa kwa vitu vingi, huitwa kwa jina hilo madini ya platinamu, na hayo madini ni ruhusa kwa wanaume kuyatumia kwa Ijmaa ya wanazuoni, hakuna katazo lolote lililopokelewa kuhusu madini haya.

Ama kuyaita madini ya platinamu kama dhahabu nyeupe haiyafanyi madini hayo yawe haramu, kwani madini hayo hayahusiani na dhahabu yenyewe isipokuwa kwa jina tu la kuazimwa pamoja na kuwapo tofauti ya uhalisia wake, na jambo la kuzingatia ni vinavyoitwa na wala sio majina, na iliyo haramu ni dhahabu ya njano iliyo maarufu tu. (Ni kipengele chenye nambari ya atomiki 79 na uzani wa atomiki 196.967).

Jina la dhahabu nyeupe hutumika pia kuiita dhahabu ya manjano iliyopakwa platinamu, na aina hii ndio inayopitishiwa hukumu ya dhahabu, na wala haijuzu kwa mwanaume kujipamba nayo.

Jina Dhahabu nyeupe hutumika pia kuuita mchanganyiko wa dhahabu maarufu ya manjano na maada ya Palladium au mada nyingine. na aina hii ya dhahabu, wenye Wanachuni wametofautiana hukumu yake. Wapo walioihalalisha na miongoni mwao wapo walioiharamisha, lakini ni vyema zaidi kujiepusha navyo, ili kujitoa katika tofauti.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas