Hukumu ya Kuuza Nguo zenye chapa Ba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuuza Nguo zenye chapa Bandia

Question

Kazi yangu ni kuuza nguo zenye chapa bandia ambazo zinatengenezwa Tunisia, je, biashara hii ni haramu? Na ikiwa haramu, faida yake niifanyie nini? Na je! Kununua nguo zenye chapa bandia zilizosambaa katika maduka mengi hapa kwetu ni Haramu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kughushi chapa ya biashara kisharia hakufai, na kufanya kazi katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa za kucopy hakujuzu; kwa sababu katika hilo kuna kula haki za watu, lakini kuuza bidhaa hizi baada ya kuwa zimeshatengenezwa, jambo hili lipo katika sera za kiuchumi ambazo zinawekwa na kila nchi kwa ajili ya kulinda uchumi wake, ikiwa haijapigwa marufuku katika nchi yao, basi haikatazwi kuuza, kwa sharti kumweleza anayenunua uhalisia wa bidhaa kwamba si asili, ili mfanya biashara asiingie katika kugushi na kubambikia kulikoharamishwa, na mali iliyoazalishwa inakuwa halali kisharia, na ikiwa kufanya biashara katika bidhaa hizi kumepigwa marufuku na nchi, basi ni haramu, kwa sababu katika Uislamu usijidhuru wala usidhuru.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas