Kuchelewa kugawa mirathi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchelewa kugawa mirathi

Question

Ipi hukumu ya kuchelewesha kugawa mirathi baada ya kifo?

Answer

Mirathi baada ya kifo cha mrithiwa ni haki ya warithi wote hivyo anastahiki kila mrithi kupata fungu lake katika mirathi baada ya kuondolewa gharama za kuandaliwa maiti na baada ya kulipa madeni na kutekeleza wasia.

Wala haifai kwa yeyote katika warithi kuzuia pasi warithi wengine kupata mafungu yao yaliyopangwa na Sharia kwa kuwanyima au kukwamisha, kama vile haifai kujipendelea mmoja wao kutumia mali ya mirathi pasi ya idhini na ruhusa ya warithi wengine waliobaki, hivyo kuzuia ugawaji au kuchelewesha bila ya sababu ya msingi au ruhusa ni haramu Kisharia, na dalili ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na ukimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wacha-Mungu} Aal-Imraan: 133. Ndani ya Aya kuna amri ya kufanya haraka kuziendea sababu za msamaha na kuingia peponi, na miongoni mwa sababu kubwa za kuingia Peponi na kupata radhi za Mwenyezi Mungu ni kutekeleza haki za waja.

Share this:

Related Fatwas