Kuchelewa kugawa mirathi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchelewa kugawa mirathi

Question

Ni ipi hukumu ya kuchelewa kugawa mirathi kinyume na makusudio kwa baadhi ya warithi?

Answer

Baada ya kuhakikisha kifo cha mrithiwa kila mrithi anastahiki fungu lake katika mali ya urithi baada ya kutolewa matumizi ya maandalizi ya mazishi na kulipa madeni ya maiti na kutekeleza wasia na kafara na nadhiri na mfano wa hayo.

Hakujuzu kwa mrithi yeyote kufanya hila ili warithi wengine wasipate fungu lao la kisharia kwa kuwanyima au kuwacheleweshea, pia hakujuzu kujimilikisha mmoja wao kwa kutumia mali za urithi bila ya warithi wengine au idhini yao; kuzuia mgao au kuchelewesha bila ya udhuru au ridhaa za warithi ni haramu kisharia, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenye kuchelesha mirathi kwa warithi wake, Mwenyezi Mungu atakata mirathi yake peponi siku ya kiama”. Hadithi hii imepokelewa na Albayhaqyy23. Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas