Kuapa sana

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuapa sana

Question

Nini hukumu ya kuapa sana wakati wa kununua na kuuza?

Answer

Inachukiwa kuapa sana wakati wa kununua na kuuza, kwa sababu kunapelekea kupoteza baraka, na kwani kuapa sana ni sababu ya kuondoka kwa Utukufu wa jina la Mwenyezi Mungu kwenye nyoyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha kuhifadhi viapo na akakataza kuzidisha viapo hivyo. Mwenyezi Mungu amesema: {Na hifadhini yamini zenu} [Al-Maaidah: 89], na Amesema vile vile: {Wala msifanye jina la Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu} [Al-Baqara: 224]. Imepokelewa katika Sunna iliyotakasika kukataza kwa kuapa sana kwa ujumla na hasa wakati wa kufanya biashara kwa sababu baraka huondolewa kwake; Mtume (S.A.W) amesema: “Kiapo kinasaidia kuuza bidhaa lakini kinafuta baraka” (Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari). Sio lazima kuapa sana hata kama anayeapa ni mkweli au muongo.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas