Kununua Gari Kupitia Benki

Egypt's Dar Al-Ifta

Kununua Gari Kupitia Benki

Question

Kulingana na ofa iliyowasilishwa na Benki ya Alexandria kwa madhumuni ya kufadhili ununuzi wa magari, tafadhali tunaomba mtupe kwa maandiko kuhusu uhalali wa ofa hii kutoka benki hiyo kwa madhumuni ya kuwanunulia wafanyikazi magari mapya, Pamoja na kizingatia yafuatayo:

1- Mfanyakazi anawasilisha kwa benki bei ya gari analotaka.

2- Mfanyakazi atatia saini kijitabu cha masharti kinachohusiana na benki, ambacho kinasomeka kwa nje "Mkopo wa Ufadhili wa Magari" na kinajumuisha maelezo ya muamala katika kipindi chote cha malipo.

3- Baada ya benki kumtambua mfanyakazi, na ikiwa imekubali kufanya nae muamala, hutoa maagizo kwenye chumba cha maonesho ya magari kuruhusu upelekaji wa gari, ikiweka sharti kuwa umiliki wa gari ni wa benki na itaendelea kuwa chini ya umiliki wake hadi thamani yake ilipwe, pamoja na faida iliyokubaliwa hapo awali na mfanyakazi anayetaka kununua gari hilo.

4- Thamani ya gari inatolewa kwenye chumba cha maonesho ya gari bila mfanyakazi kupokea bei yoyote.

5- Chumba cha maonesho kinafanya mkataba na benki kutekeleza uuzaji wa gari.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Imethibitishwa na Sharia kwamba uuzaji ni halali kwa malipo taslimu au kwa malipo ya awamu hadi tarehe maalumu. Kupanda kwa bei kwa malipo ya awamu inajuzu kwa mujibu wa Wanachuoni wa Fiqhi walio wengi, kwani hii ni aina ya murabaha, aina ya mauzo iliyoruhusiwa na Sharia ambayo inajuzu kubainisha ongezeko la bei kwa ajili ya malipo ya awamu na tarehe maalumu. Kwani muda japo kuwa sio pesa kiuhalisia, isipokuwa jambo hilo lipo katika sehemu ya Murabaha, bei inaongezwa kwa muda wake ikiwa tarehe maalum imetajwa badala ya bei iliyoongezeka. Hii inafanywa kwa nia ya kupata ridhaa ya pande zote mbili, kwa sababu hakuna uhalali wa kukataza, na kwa sababu watu, wawe wauzaji au wanunuzi, wanahitaji sana hivyo. Hii haizingatiwi riba, kwani kanuni ya Sharia inasema kwamba kama bidhaa zikiuzwa, basi hakuna riba.

Hivyo basi, kununua gari kupitia benki, ambapo benki humlipa muuzaji pesa na kisha kukusanya kiasi cha ziada kutoka kwa mnunuzi, inaruhusiwa kwa mujibu wa Sharia. Hata hivyo, tunapendekeza kuondoa maneno ya “Mkopo wa Ufadhili wa gari” na badala yake kuweka maneno ya “Ofa ya Ufadhili wa Gari," ili liwe jina sahihi la uhalisia wa uhusiano kati ya wahusika mbalimbali.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas