Kununua gari kupitia kuweka gari la kale mbadala
Question
Je, inajuzu kununua gari kwa njia ya kuweka gari la zamani mbadala?
Answer
Kununua gari jipya kwa njia ya kuweka gari la zamani mbadala katika tangazo la taifa la kufanya hilo inajuzu kisharia kwani mkataba wa ununuzi hapa hujumuisha kuuza gari la zamani ambayo ni kulitathmini kama mabaki ya chuma halafu kukata thamani ya chuma kutoka thamani ya gari jipya linalonunuliwa kwa kunufaika kwa punguzo linalotolewa na serikali na benki huwa upande wa tatu kati ya muuzaji ambaye ni mwenye duka au maonesho ya magari na mnunuzi kwa kulipa gharama ya gari jipya, sura hii haina riba kwa kuwa bidhaa ikipatikana basi hamna riba.