Msimamo mkali katika dini

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo mkali katika dini

Question

Ni ipi hukumu ya msimamo mkali katika mambo ya dini? Je, kuna mifano ya hili?

Answer

Misimamo mikali ni jambo la kulaumiwa na lilionekana kwa maana yake ya kimapokeo zamani. Qur’ani ilionesha kuwa lilikuwa ni jambo linaloenea katika mataifa yaliyotangulia, na kwamba lilikuwa ni sababu ya moja kwa moja ya kuwaletea taabu na dhiki. Mwenyezi Mungu amesema: {Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki.} [Al-Maida:77]

Mtume (S.A.W) ameashiria hayo katika maonyo yake kwa umma huu dhidi ya misimamo mikali, na kutofuatia yale ambayo mataifa yaliyotangulia yalitenda dhambi, kama vile misimamo mikali ya kupindukia. “Msiwe na shindikizo ili msije kufanyiwa shindikizo, watu wakijifanyia shindikizo, basi Mwenyezi Mungu huwafanyia uzito, basi hayo ndio masalio yao katika nyumba .

Moja ya mifano ya zamani ya shindikizo ni kisa cha wamiliki wa ng'ombe kilichoelezwa ndani ya Qur'ani Tukufu, kinaashiria ukaidi wa Wana wa Israili pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowaamrisha kuchinja ng'ombe. Ilibidi watii walichoagizwa, lakini walikataa, na walipendelea kufanya ubadhirifu na shindikizo katika kuomba sifa za ng'ombe. Kila walipojulishwa maelezo, walisisitiza kwa kuomba maelezo ya ziada , na wakasema mwishoni mwa Aya hiyo: { Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo} [Al-Baqarah: 71].

Ingawa kauli yao hiyo: “Sasa umetuonesha ukweli” ni kauli ambayo ina shambulio kubwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Musa, kwa sababu aliwaonesha ukweli katika kila jambo waliloliomba.

Share this:

Related Fatwas