Misimamo mikali na Ugaidi

Egypt's Dar Al-Ifta

Misimamo mikali na Ugaidi

Question

Misimamo mikali ni nini na Ugaidi ni nini?

Answer

Asili ya misimamo mikali ni kutoka katika hali ya kupita kiasi, kwa hivyo inasemekana kuwa jambo hili ni itikadi kali likiwa litajitenga na liko ukingoni, na misimamo mikali katika jambo ikiwa imevuka mipaka ya wastani na haisuluhishi, na kutoka humo vikundi vyenye misimamo mikali vinaitwa hivyo kwa sababu havisuluhishi na vinakwenda nje ya mipaka ya wastani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani” [Al-Baqara:143].

Ama ugaidi kufuatana na isimu una maana ya vitisho, na una hali mbili katika matumizi:

Hali chanya: Miongoni mwazo ni kauli yake Mola Mtukufu: “Na niogopeni Mimi tu” [Al-Baqara: 40], ambapo Mwenyezi Mungu anawaogopesha waja wake wasivunje ahadi yake, na pia dua ya Mtume (S.A.W): “Na nimeutegemeza mgongo wangu kwako kwa matajarajio na kwa kukuogopa, …”. Na hali hasi: Miongoni mwao ni kauli yake Mola Mtukufu: “Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu, na wakaleta uchawi mkubwa” [Al-Araf 116],. Hii ni pamoja na kuelezea "magaidi" kama vikundi vya haramu ambavyo vinachukua njia ya vurugu kwa kuua na kuhujumu serikali na watu ili kufikia malengo yao ya kisiasa.

Share this:

Related Fatwas