Uislamu umejali usafi

Egypt's Dar Al-Ifta

Uislamu umejali usafi

Question

Uislamu umejali vipi  usafi ?

Answer

Uislamu unahimiza usafi, unachukulia kuwa ni kiini cha ujumbe wake, na sehemu ya imani, na unawaamrisha wafuasi wake kuchunga sababu zake katika nyanja mbalimbali. Hii ni kwa sababu ya kuwa na  athari kubwa katika kuitakasa nafsi na kumwezesha mtu kubeba mizigo ya maisha. Uislamu ulifanya usafi kuwa ni ibada ya makusudi kwa ajili yake. Kama vile kutawadha na kuosha, na kufanya kuwa ni sharti na mlango wa ibada nyingi. Kama vile Swala, Tawaf (kuzunguka Nyumba tukufu), na kusoma Qur’ani. Mtume (S.A.W), amesema: “Haikubaliki Swala bila ya Twahara”.

Miongoni mwa dhihirisho la Twahara ni usafi katika Uislamu pia ni usafi wa nyumba na sehemu za umma na kuzitwaharisha na uchafu. Kwa mujibu wa kauli yake Mtume, (S.A.W): “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mzuri anapenda uzuri, Msafi anapenda usafi, Karimu anapenda ukarimu, Mpaji anapenda upaji(kutoa),basi safisheni kumbi zenu-viwanja vyenu -wala msijifananishe na mayabudi” Imepokewa na Al-Tirmidhiy.

Share this:

Related Fatwas