Uislamu na Dini nyinginezo

Egypt's Dar Al-Ifta

Uislamu na Dini nyinginezo

Question

Je, kuna uadui wowote kati ya Uislamu na Dini nyinginezo?

Answer

Jibu:

Hapana uadui wa namna yoyote kati ya Uislamu na dini nyinginezo, bali ukweli ni kinyume kabisa, kwani Uislamu ndiyo dini ya amani, naye Nabii wa dini hiyo ndiye Nabii wa rehema (S.A.W.), Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} [Al-Anbiyaa: 107], naye Mtume (S.A.W.) amesema: "Muislamu wa kweli ni yule ambaye watu hawapati adha kutokana na adha ya ulimi wake na mkono wake, na muumini ni yule ambaye watu wamesalimika kuhusu damu na mali zao" [Imesimuliwa na An-Nasaiy], kwa hakika, yapo mambo mengi ya pamoja kati ya Waislamu na wasio Waislamu likiwemo la kukuza nchi, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo} [Hud: 61], hapa kukuza nchi maana yake ni kuijali na kuhakikisha maadili makuu ya pamoja kama vile; Kumlinda mwanadamu na kumhudumia, kwa upande wa Kielimu, Kiafya; Kimwili na Kisaikolojia, na kwa upande wa Kiuchumi, Kijamii, Kitabia, pia miongoni mwa namna za kukuza nchi kuhifadhi mazingira kwa kutunza maliasili na kuyaendeleza kwa kuwatunza wanyama, mime ana vitu visivyo na uhai, na kukataa ufisadi kwa namna zake zote, kukataa dhuluma, kuhakikisha uadilifu, kuwasaidia wanyonge, kushikamana na kusaidiana wakati wa kutokia janga au balaa, pamoja na maadili ambayo mwenye akili yeyote huwa anatakiwa kuwajibika nayo.

Share this:

Related Fatwas