Uislamu haukuenea kwa kutumia upang...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uislamu haukuenea kwa kutumia upanga

Question

Je, Uislamu ulienea kwa kutumia upanga?

Answer

Kwa kweli, Uislamu haukuenea kwa kutumia upanga hata kidogo, lakini dini hiyo ilienea kwa njia ya kulingania kwa njia ya Mwenyezi Mungu kwa kutumia hekima na mawaidha mema, pamoja na tabia njema za Waislamu na miamala mizuri yao kwa watu wote, na Imani yao thabiti kuhusu Mola wa walimwengu wote, dalili iliyo wazi zaidi ya kuthibitisha hayo kuwa Wanazuoni na Maimamu wengi wa Waislamu hawakutoka Uarabuni wala hawakuwa Waarabu kabisa, na Uislamu ungalikuwa umewalazimisha watu wajiunga nao wasingalikuwa na ufanisi mkubwa huu katika fani na taaluma mbalimbali kufikia viwango vya juu kabisa katika fani na taaluma hizo.

  Miongoni mwa Maimamu maarufu hawa Imamu mjuzi zaidi Abu Hanifa Al-Noa'aman kiongozi wa Madhehebu, Imamu Bukhary mtungaji wa kitabu cha Sahihi, Ibnu Majah mtungaji wa As-Sunan, mtaalamu mkubwa wa lugha Amr bin Athumani anayejulikana kwa jina la Sibaweih mtungaji wa kitabu cha Al-Kitabu, mwanafunzi wake Abul-Hassan Al-Akhfash, mwanazuoni maarufu wa Uislamu Abu Hamed Al-Ghazaly, Sheikh Raisi Mwanafalsafa tabibu Ibnu Siina, mwanafalsafa mashuhuri Al-Faraby, Khawarizmy mtaalamu wa falaki, hisabati na jiografia, na wengine wengi ambao mababu wao wangekuwa wamejiunga na Uislamu kinyume na matakwa yao kwa vitisho vya panga watoto na wajukuu wao wasingeipenda dini hiyo wala wasingeijifunza dini na kuitetea na kuieneza katika kila kona duniani.

Share this:

Related Fatwas