Kupetuka Mipaka katika Mahari na At...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupetuka Mipaka katika Mahari na Athari zake

Question

Kuna tatizo la kijamii nchini India hasa katika eneo la Milibar, eneo hili linawasichana wengi wa Kiislamu ambao hawakuolewa, kwa sababu ya mahari kuwa juu. Muulizaji anaomba kuwekewa wazi hukumu ya sharia katika hilo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mtume S.A.W. anasema: “Enyi vijana mwenye kuwa na uwezo miongoni mwenu, basi aoe, na asieweza basi afunge, kwani hilo kwake ni kinga”, na uwezo ni gharama za mke kuanzia kula, kuvaa, na makazi …Nk. Hivyo basi katika Uislamu sharti pekee la kuoa ni uwezo wa kugharamia familia mpya ili iishi katika misha mazuri na ya heshima, kwa maana Uislamu haukuweka sharti ya utajiri, na Uislamu umewajibisha mahari kwa masilahi ya mwanamke mwenyewe, ili kulinda heshima yake, hivyo hakusihi mahari kuwa kikwazo cha ndoa au kumchosha mume, na Mtume S.A.W. amesema kuhusu mahari akimwambia mtu aliyekuwa akitaka kuoa: “Tafuta japo hata pete ya chuma”, ikiwa pete ya chuma inafaa kuwa mahari ya mke, basi mahari kubwa si katika Sunna ya Uislamu; kwani mahari kubwa ni kikwazo cha ndoa na hakiendani na malengo asili ya ndoa ambayo ni kujizuia na machafu kwa mvulana na msichana kwa kulinda usafi wa mtu na jamii.

Na Mtume S.A.W. anasema: “wanawake wenye mahari ndogo ndio wenye baraka”, Uislamu ijapokuwa haujaweka kiwango cha juu cha mahari, lakini Hadithi tukufu zimelingania kuwepesisha ndoa na kuhimiza kwa mwenye uwezo kwa njia zote ziwezekanavyo, na Masahaba wa Mtume S.A.W walikuwa wakio, na mahari ya mke ni kumfundisha Qur`ani, anasema Mtume S.A.W. anamwambia mtu alietaka kuoa: “Muoe kwa ulichonacho katika Qur`ani. Kumfundisha baadhi ya Aya katika Qur`ani ndio mahari; basi ni wajibu kutozidisha mahari, na baba arahisishe ndoa za mabinti wake kwa kiasi awezavyo aanapopatikana mume mwema ili tuwalinde watoto wetu wavulana na wasichana.

Mtume S.A.W. ametupa nasaha kwa kauli yake: “Atakapowajia mnayeiridhia dini yake na uminifu wake basi muozeni, msipofanya hivyo mtakuwa mmefanya fitina na uharibifu mkubwa”, nasaha hizi za Mtume S.A.W. zina maana kubwa, na ni wajibu kuzifanyia kazi na kushikamana nazo, ili kushinda tatizo hili la kijamii na kupanda kwa mahari. Na katika yaliotajwa tunapata jibu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas