Kutotimiza kwa Mume Ahadi zake

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutotimiza kwa Mume Ahadi zake

Question

Mume wangu hakuwa mwaminifu kwangu na alienda kinyume na kila kitu tulichokubaliana. Iwe katika makao yetu au katika jinsi alivyonitendea mimi na watoto wetu, alinitendea vibaya na kunishambulia mimi na watoto wangu zaidi ya mara moja, na akafanya maisha ya familia yetu kuwa habari ya kuchapishwa katika magazeti na kuwapa habari zisizo za kweli kunihusu. Je, ni ipi hukumu ya Sharia ya Kiislamu juu ya hili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Uislamu unatuamrisha kutimiza ahadi zetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlioamini timizeni ahadi}. [Al-Ma’idah:1] Na Mtume (S.A.W) amesema: “Waislamu wako juu ya masharti yao isipokuwa sharti inayoharamisha halaal au inayohalalisha haraam”. Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy na kuthibitishwa naye. Mtume (S.A.W) alieleza kuwa masharti yanayostahiki zaidi kutekelezeka ni masharti ya ndoa. Kwa heshima ya mke na kuhifadhi haki zake, Mtume (S.A.W) alisema: “Masharti yanayostahiki zaidi kutimizwa ni yale ambayo kwayo mnahalalishia tupu.” Hadithi hii imekubaliwa. Fatwa juu ya masharti ya ndoa ni kwamba kila sharti linalomnufaisha mke na lisilopingana na misingi ya mkataba ni wajibu kwa mume kulitimiza. Hii ni pamoja na kuweka masharti ya mahali pa kuishi. Ikiwa mume atashindwa kulitimiza sharti hilo, hii inampa mke haki ya kudai kubatilisha ndoa, na haki zake zimewekwa kikamilifu. Imaam Ibn Qudamah amesema katika kitabu cha Al-Mughni: “Iwapo akimwoa na akaweka sharti kwamba hatamuoa mwanamke mwingine, basi mkewe huyo ana haki ya kumtaliki ikiwa ataoa mwanamke mwingine. Jumla ya hayo ni kuwa masharti ya ndoa yamegawanyika katika makundi matatu: Moja wapo ni lile linalopaswa kutimizwa, ambalo ndilo linalomnufaisha, kama vile kumpa sharti kwamba hatasafiri na nyumba yake au hatatoka nje ya nchi. au asioe mwanamke mwingine, au asimtwalie suria, basi ni lazima awe mwaminifu kwake katika jambo hili. Asipofanya hivyo, basi mkewe ana haki ya kuibatilisha ndoa hiyo. Imepokelewa kutoka kwa Omar Ibn Al-Khattab (R.A) na Saad bin Abi Waqqas, Muawiyah, na Amr Ibn Al-Aas, (R.A), na hivi ndivyo walivyosema Shurayh, Omar Ibn Abdul Aziz, Jabir Ibn Zaid, Tawus, Al-Awza’i na Ishaq… Tunayo kauli ya Mtume (S.A.W): “Hakika inayostahiki zaidi kutimizwa ni masharti yale ambayo kwayo mmehalalisha tupu.” Imepokelewa kutoka kwa Said, na kwa maneno: “Masharti yanayostahiki zaidi kuyatimizwa ambayo kwayo mmehalalisha tupu.” Hadithi hii imekubaliwa, na pia kauli yake Mtume (S.A.W): “Waislamu wako chini ya masharti yao,” na kwa sababu ni kauli ya mmoja wa maswahaba mashuhuri, na hatumjui yeyote ambaye alihitilafiana nao zama zao, na ilikuwa ni Ijmaa. Imepokelewa kutoka kwa Al-Athram kwamba: Mwanaume alioa mwanamke na akaamuru apewe nyumba yake. Kisha akataka kumhamisha, hivyo wakaupeleka mgogoro wao kwa Umar. Akasema: mke ana sharti lake. Yule mtu akasema: Basi mtatutaliki. Umar alisema: Haki hukatwa wakati masharti yanapowekwa. Kwa sababu ni hali ambayo inamnufaisha na ina lengo ambalo halizuii lengo la ndoa, ni jambo la lazima, kana kwamba alitangaza ongezeko la mahari au sarafu nyngine isipokuwa pesa ya nchi.

Kwa hiyo, kila kitu kilichotajwa katika swali hilo, kama vile kuvunja agano, kutendeana vibaya, na kuyafanya maisha ya ndoa kuwa mada ya kuchapishwa kwenye magazeti, ni haramu ya kidini na yanapingana na yale yanayojulikana ya dini ya Kiislamu, ambayo inakataza dhulma, tuhuma za uwongo, na uasherati katika mizozo. Hakika baadhi ya haya ni madhambi makubwa, na hayana uhusiano wowote na Uislamu wala mafundisho yake matukufu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas