Kushiriki katika mashindano

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushiriki katika mashindano

Question

Nini hukumu ya kushiriki katika mashindano ya kubahatisha michezo?

Answer

Imethibitishwa kisheria kuwa kamari, na rihani ni haramu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” [Al-Ma’idah: 90]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema pia: “Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua”(Al-Baqarah: 188), vile vile  Mwenyezi Mungu akasema: “Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.” [An-Nisaa:29].

Ikiwa shindano hili linahusisha ushiriki wa kifedha kutoka kwa washindani, basi hakuna shaka kwamba linajumuisha rihani iliyopigwa marufuku na kamari. Kwa sababu kwa njia hii, kila mmoja miongoni mwa washiriki ametoa kiasi fulani cha pesa, kisha mshindi huchukua pesa hizi zote kutoka kwao.

Ikiwa ushiriki katika shindano hili sio badala ya pesa; Hukumu ya kisheria juu yake inajuzu.

Ipasavyo; Kushiriki katika shindano la kubahatisha michezo ambalo halihitaji kulipa pesa kunaruhusiwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu iwapo mshiriki ataegemeza utabiri wake kwenye masomo na uchambuzi wa kimantiki.

Share this:

Related Fatwas