Makhariji wa zama hizo
Question
Je, kuna Makhariji katika zama hizi?
Answer
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Ali Ibn Abi Talib (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) alisema: Watatokea watu katika zama za mwisho wajinga Wasio na busara; au akasema ni chipukizi watakuwa wakisema kauli nzuri ya viumbe (lakini) imani yao haivuki kwenye koo zao (hawana imani), wanatoka katika dini kama mshare unavyotoka katika kiwindwa, basi popote munapowakuta wauweni, kwani katika kuwaua wao kuna ujira mkubwa Siku ya Kiyama kwa atayewaua”. Hizi ni baadhi ya sifa za Makhawariji ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisimulia juu yake, kama alivyosema kuwa watatokea mwisho wa zama, basi yeyote aliyezitumia sifa hizi ni miongoni mwao katika kila zama, na hapana shaka kwamba makundi yenye misimamo mikali katika zama hizi kama vile Daishi na mfano wake waliowaasi watawala wa Waislamu wakidai Kufikia ufalme wa Mwenyezi Mungu na kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu, na kuwafanya umma kwa ujumla kuwa makafiri, kuhalilisha damu ya Waislamu na heshima zao, na kueneza mauaji na fitna miongoni mwa watu wa Waislamu. Yote haya yanaashiria kwamba mbinu ya Makhawariji ilitumika kwa baadhi ya makundi katika wakati huu, yakiongozwa na Daishi