Programu ya Lugha ya Nyurolojia (Lu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Programu ya Lugha ya Nyurolojia (Lugha ya Akili).

Question

Ni nini hukumu ya kujifundisha program ya lugha ya nyurolojia (lugha ya akili) na kufaidika nayo kwa kuitekeleza katika nyaja za kidini kama kuihamasisha nafsi kufanya mambo ya kheri katika ibada au miamala au kutafuta elimu ya kisheria?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hakika uislamu umesifia elimu na wanachuoni na ukaelezea  kunyanyua daraja zao duniani na akhera, na ukawahamasisha waislamu kutafuta elimu na hekima, anasema Mola wetu Mtukufu katika kitabu chake kitukufu: {Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu} [AL-MUJAADALAH:11], akasema tena Mola Mtukufu: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili} [AZZUMAR:9].

          Akasema tena: {Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu} [TWAHA:114], aya zikajulisha juu ya umuhimu wa kuzidisha elimu kuwa ni kuzidisha kheri na fadhila, kama zilivyojulisha kuwa elimu ndio njia ya watu wenye akili kwa ajili ya kujikumbusha na kuwaidhika kwa Aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu za Quraani na ulimwengu, bali elimu ndio njia ya kweli ya kunufaika na sheria za dini alizozishusha Mwenyezi Mungu na vile vitu ambavyo aliwadhalilishia watu, isipokuwa hata Mtume (S.A.W) alikuwa akijilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa, ikawa katika dua zake (S.A.W) katika yale aliyoyapokea Muslimu katika kitabu chake kotoka Hadithi ya Zaydi Ibn Arqam (R.A): “Ewe Allah najilinda kwako kutokana na elimu isiyokuwa na maunufaa, na kutokana na moyo usio kuwa na unyenyekevu, na kutokana na  nafsi isiyoshiba,na kutokana na dua isiyopokelewa”, na Allah Mtukufu anasema {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana} [AL AHZAAB: 21]. Ikafahamika katika haya kwamba manufaa ndiyo kigezo cha Uislamu ambacho kinapanga elimu ambazo inafaa kujishughulisha nazo kwa kuwa kwake ni zenye manufaa ya duniani au akhera; na elimu ambayo haifai kujishughulisha nayo ni kutokuwa na manufaa; ama elimu ambayo inasababisha madhara kwa mwenye kuisoma kujizuwia kutojishughulisha na elimu hiyo inakuwa ni wajibu  na bora. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua} [AL BAQARAH: 102]; na kwa kukisia kwa kukusanyika manufaa na madhara katika elimu Fulani, wakati huo hukumu itafuata sehemu kubwa kati ya hizo, amesema Shams Al Aimah El Sarkhasiy El hanafiy katika kitabu cha [Al Mabsout 10/196, Ch. Dar Al Maarifah]: “Hukumu ni kwa mshindi, kwa kuwa mwenye kushindwa anakuwa mtumiaji katika mahojiano na mshindi, na mtumiaji katika hukumu ni ziro / hayupo”.

Lakini wakati huohuo imeshurutishwa kwa anayejishukhulisha awe na elimu ya kutosha katika misinigi ya uislamu kama vile tawheed na sheria, kama walivyoshurutisha wanachuoni hapo awali kwa mtu anayesoma elimu ya mantiki iliyochanganyika na mafundisho mabya ya wanafalsafa awe amepitia kwanza katika elimu Quraani na Sunnah na yaliyomo ndani yake  kutokana na mafundisho,sheria na tabia.

Mwanachuoni Al -Akhdar mwenye kitabu cha: [Al- Sullam katika Elimu ya Mantiki amesema:

na kauli iliyo mashuhuri na sahihi

 

Ni sawa kwa ukamilifu wa akili

Kuifahamu Quraani na Sunnah

 

Ili imuongoze kwenye njia sahihi

Amesema mwanachuoni Al Mulawiy katika kusherehesha kwake kitabu cha: [Al Sullam uk. 42, Ch. Mustafa Al Halabiy): ( Kuisoma Sunnah) yaani Hadithi (kitabu) yaani Quraani inajuzu kwake, (ili imuongoze kwenye njia sahihi) kwa kuwa atakuwa kailinda imani yake haitamduhuru baada ya hapo kusoma kwake imani mbovu na shaka zake, ama akiwa ni mjinga haifai, kwa kuwa atakuwa hana uwezo wa kuondoa shaka zao huenda zikakaa ndani ya moyo wake na hivyohivyo akiwa ni mwenye akili lakini si mwenye kufahamau Kitabu na Sunnah)).

Na programu ya lugha ya akili nielimu au taaluma ya majaribio ambayo ni mpya, na huitwa kwa lugha ya kiingereza: (Neuor Linguisitic Programming) au kwa kifupi (NLP). Na maudhui ya elimu hii ni kufahamu jinsi ya kumuhamasisha mwanadamu vipi atafaulu katika kufika kwenye lengo lolote analolikusudia, na jinsi ya kuvivuka vikwazo vinavyomkwamisha kutofanikiwa katika hayo kwa kiasi itakavyowezekana, sawa sawa vikiwa vikwazo au ugumu ule ni wa kweli au wa kuhisi, na hiyo ni kupitia kuiathiri nafsi kwa mambo chanya kwa kutumia maelezo (lugha) ya ulimi au mwili ambazo zitaingia katika nafsi na kutia imani na hamasa itakayomsukuma katika kuelekea mafanikio na kumuondosha kwenye kutosheka na mambo hasi.

Na imesemekana kuhusu elimu hii kuwa ni uinjinia wamafanikio ya mwanadamu na ikasemwa kuwa ni ibara ya: Mkusanyiko wa njia na mbinu zinazotegemea misingi ya kisaikolojia inayolenga kutatua baadhi ya matatizo ya kisaikolojia na kuwasaidia watu katika kupata mafanikio bora katika masha yao.

Shule hii ya kisaikolojia inasifika kuwa mwenye kuzifahamu vizuri njia zake basi hahitajii tabibu kutoka nje, yenyewe inaweza kuwa njia ya kutibu nafsini tiba ya saikoloji ya tabia binafsi, inajaribu kupanga mbinu za wazi za kufaulu kisha kutumia mbinu za kisaikolojia ili kuimarisha tabia yenye ufanisi zaidi na kujaribu kuvunja na kuondoa akida za kale ambazo zimegundilika kuwa kikwazo cha maendeleo ya mtu, na kutokea hapa ilikuja fikra ya kuiita programu yaani inarejea kuipanga akili kwa njia ya ulimi au lugha.

Na wakwanza aliyependekeza mbinu ya programu ya lugha ya akili alikuwa (Richard Bandler) na (John Girender) mwaka 1973 kama kundi la mifano na kanunu za kusifia mahusiano kati ya akili lugha sawa sawa ikiwa ni lugha ya herufi au isiyokuwa ya kiherufi (kimwili) na jinsi gani yapasa kupangilia mahusiano kati yao (program) ili kuweza kuathiri juu ya akili ya mtu mwili wake na fikra zake. Athari hii inaweza kuwa kwa elimu na uelewa wa mtu anayetibiwa au hata bila uelewa. Na utafiti wa kujenga uzowefu wa mtu, ni msingi unaoasisiwa juu ya tabia kamili za mtu muundo wake ni wenye kukubali kupangika kivitendo.

Na inaonekana kuwa fikra ya elimu hii imesimamia kuwavitendo vyetu vyote na mazoea yetu katika maisha yanatoka kwenye kundi la imani ya akili kamili, kwa hivyo ikiwa imani hii ni chanya huwenda mtu akafaulu katika kufanya anachokitaka, na ikiwa ni hasi basi huwenda akafeli, na kazi ya programu ya lugha ya akili ni kudhibiti mfumo wa imani hizi kwa kubadilisha au kufuta au kuongeza  kwa yale yatakayoleta mafanikio katika kazi, na waasisi wa programu ya lugha ya akili kutokana na majaribio wamekuta kwamba kwa kawaida mwanadamu huielekezea nafsi yake ujumbe wa lugha ( kwa ulimi na mwili) ambao huathiri katika imani yake ya kiakili  na kutoa tabia yake na kutegemea mafanikio yake au kufeli kwake kwa kiasi kikubwa, taarifa hizi ndio njia ambayo inayoizingatia /kuilenga,elimu ya programu kwa ajili ya kufikia kuithibiti dhati na vitendo vyake na kuviboresha kuwa katika hali bora. Na kutumia lugha kwa malengo haya inazingatiwa kuwa ni matumizi ya kitaalamu kama vile kuitumia katika mashairi na kuigiza na mfano wa hayo kwa ajili ya kumuathiri msikilizaji au mtazamaji kwa kuyaelekeza mawazo yake katika kupenda kitu fulani na kumwita kukifanya au kukiona kibaya na kukikimbia /kutokifanya.

Kwa ujumla elimu hii ni taaluma katika utafiti wa chombo cha kiufundi yenye kuathiri katika nafsi ya mwanadamu anaweza kukitumia kwa ajili ya kutatua baadhi ya matatizo ya kisaikolojia jambo litakalo msaidia kupata mafanikio katika maisha ya vitendo, na hakuna katika lengo kama hili yanayopingana na sheria katika chochote, hakika matumaini na hali chanya na kuwa na nguvu ya juu na kuihamasisha nafsi kwa ajili ya kufanya kazi njema zenye maslahi ya kidunia au akhera ni katika mambo mazuri na ambayo sheria tukufu imeyahimiza na kudharau na kwenda kinyume na hivvo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akitoa wito kwa waja wake kwa kutojisalimisha mbele ya ujumbe wenye kukatisha tama ambao anautuma mwanadamu mwenye kuifanyia israfu nafsi yake: {Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu} [AL ZUMAR: 53]. Na akaema Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia Mtume wake Ibrahim (A.S) {Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?} [AL HIJIR: 56]. Akasema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia Mtume wake Yaqoub (A.S) {Wala msikate tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri} [YOUSUF: 87]. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akizihamasisha nafsi za wamumini kushindana kwenye mafanikio ya kufanya mambo ya kheri: {Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri} [AL MAIDAH: 48]. Akasema Mola Mtukufu: {Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia, Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana} [AL MUTAFFIFIN: 22-26], akasema Mola Mtukufu akisifia ushujaa na subira katika tabu ili kufikia ushindi: {Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanao subiri} [AAL IMRAN: 146], akasema Mola Mtukufu katika kuwainua hamasa waumini pindi walipopatwa na matatizo na kukataa tama katika vita vyao na washirikina: {Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.Kama yamekupateni majeraha, basi na hao watu wengine yamewapata majeraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu} [AAL IMRAN: 139-140], akasema pia Mola Mtukufu: {Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao} [AN-NISAA: 104], Akasema Mola Mtukufu katika kulaumu kusalimu amri kwa  udhaifu na uzito wa kunusuru haki: {Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache} [TAWBAH: 38], na katika kuwalaumu wenye kukatisha watu wenye ujumbe hasi na kutahadharisha kuto wasikiliza, anasema Mola Mtukufu {Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa! Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu} [TAWBAH: 46-47],na kulaumu au kulaani uvivu na kufanya kazi kwa kulazimishwa bila kuamini faida zake, anasema Mola Mtukuufu: {Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila nao wamechukia} [TAWBAH: 54].

Akasema Mtukufu Mwenye kutukuka katika kuwahamasisha waumini kwenye jihadi kwa aya zenye kudumu milele wanazirejea waislamu ndani ya swala na nje yake: {Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua} [TAWBAH: 41], akasema pia {Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea. Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu{ [AAL IMRAN: 159-160].

Akasema Mola Mtukufu katika kubainisha kuwa baadhi ya maneno na visa au Hadithi zipo zinazokuwa na athari kubwa katika kumthibitisha mwanadamu katika njia sahihi na kumsukuma kwenye mafanikio ya kweli: {Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo} [IBRAHIMU: 27], na akasema mwenye utukufu wa mambo: {Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako} [HUUD: 120].

Na katika kuchukua kiigizochema na kufahamu sababu za kufanikiwa viongozi na kupigiwa kwao mifano- na hicho ndicho kilicho tajwa katika programu ya lugha ya akili kwa jina la “mfano”- Mwenyezi Mungu amemuamuru Mtume wake (S.A.W) kufuata mfano wa muongozo wa viumbe bora na wenye hima ya juu na wenye nafsi safi na mwenye tabia njema na matendo nao Mitume (A.S) baada ya kutaja visa vyao na hali zao na sababu za kufaulu kwao, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao} [AL NAAM :90], akasema Mola Mtukuufu: {Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa} [AL-AHQAAF: 35]

Na Mweneyezi Mungu akawahimiza kumfuata Mtume wao (S.A.W) akasema: {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu} [AL aHZAB: 21].

Lakini kilichokosolewa juu ya elimu ya programu ya lugha ya akili  ni kuwa waasisi wake walipuuzia kusisitiza juu ya mambo muhimu ya mafanikio moja kwa moja, nao ni upande wa mawasiliano ya mja  na Mola wake, na imani yake  kwake na uwezo wake na hukumu yake na kadari yake, na wajibu wa kufuata mfumo wake na makatazo yake na maamrisho yake ya kwa ajili ya kupata mafanikio;  kwa hiyo wao wanaangalia mafanikio  kwa mtazamo wa kifedha /vitu tu, kana kwamba mafanikio yanaweza kupatikana mbali na kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, kana kwamba mwanadamu haimfurahishi na kumfanya kuwa radhi na nafsi yake  isipokuwa mafanikio ya kifedha katika maisha ya dunia  na katika mahusiano yake pamoja na viumbe, utangulizi huzalisha matokeo ya upagani mbaya (Kumkana Allah), nayo ni kuwa furaha ya mtu haishurutishwi kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala kufuata muongozo wa Mitume waliotumwa na haya yanakadhibishwa na maumbile anayoyakuta kila mwanadamu ndani yake, kama unavyokadhibishwa uhalisia wa kijamii zisizokuwa na dini ambazo zimepata mafanikio makubwa ya kifedha lakini utupu wake wa kiroho(kutokuwa na imani) kumewafanya watoto wao kupotoka na uharibifu na mwisho wake kujiuwa, haja ya mwanadamu kuwa na dini na uchamungu ni swala la lazima ambalo ulazima wake si chini ya mahitajio ya chakula, maji, hewa, kuihifadhi nafsi, akili,kizazi na mali.

Pamoja na hayo kwa muda ambao katika elimu hii kuna kitu ambacho kinawezekana kunufainaka nacho basi hakuna tatizo kwa wataalamu katika waislamu kujishughulisha nayo kwa kuirekebisha  na kuipanga na kuiongezea juu yake kwa mujibu wa misingi ya uislamu na sheria zake za kivitendo na kitabia na kutoa mifano kwa mifano ya ustaarabu wa kiislamu na watu maarufu katika uislamu waliofanikiwa ambao historia imeendelea kuwataja na wengineo, kulikuwa kuchukua na kuchanganya pamoja na kuboresha ndio desturi ya waislamu katika kujifungua kwenye staarabu zingine  na kuzibadilisha kuwa tamaduni na elimu zenye manufaa na ufundi mzuri pamoja na nyumati mbali mbali, na ikawa kauli mbiu yao katika hili ni kwamba hekima imempotea muumini popote atakapoikuta yeye ndiye mwenye haki nayo, na kuwa mbora wa watu ni mwenye manufaa na watu.

Katika yaliyopita inabainika kujuzu /inafaa kujishughulisha kusoma programu ya lugha ya akili ikiwa ndani yake hakuna mambo yanayopingana na misingi ya uislamu na sheria zake; na kama si hivyo basi ingekuwa kujuzu kwake kuna wahusu wataalamu tu ambao wanaoifanyia maboresho ili iwafikiane na muongozo wa uislamu  na wanufaike nayo watu.Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayejua.

Share this:

Related Fatwas