Kumbukumbu Siku ya Arobaini kwa Mai...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumbukumbu Siku ya Arobaini kwa Maiti

Question

Nataka kuulizia muda wa siku arubaini baada ya kifo cha mtu, kwani najua kwamba ndani ya nchi za Ulaya na Misri; watu wanasoma kiasi kikubwa cha Quraani na wanafanya kumbukumbu ya siku arubaini kwa ajili ya maiti; kwani wanaamini kwamba roho ya maiti hukaa ardhini kwa muda wa siku arubaini. Basi mna maoni gani kuhusu jambo hili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hakika kusoma Quraani juu ya roho ya maiti na kumpa maiti thawabu ya kisomo hicho cha Quraani ni jambo halali lililohalalishwa kwa dalili za sheria ya Kiislamu, na neno la Wanazuoni wa Fiqhi wa madhehebu manne ya Fiqhi yanayofuatwa wamekubaliana hivyo. Na jambo hili ni zawadi yenye thamani ambayo inatolewa na mtu hai kwa maiti kama anavyosema Imamu Al Qurtubiy katika kitabu cha: [Atazkarah], na hakuna zuio la kusoma huko katika wakati wowote, na pia hakuna zuio kwa kuainisha siku fulani kwa ajili ya kusoma huko. Kwani haikutaja yanayolizuia jambo hilo katika sheria ya Kiislamu. Lakini yanayopigwa marufuku katika sheria ya Kiislamu ni kuichukulia siku hiyo na siku nyingine kuwa ni kwa ajili ya kujiliwaza na kurejesha huzuni tena, na hufanyika mambo mbali mbali ya kumliwaza mfiwa. Kwa hivyo basi, Mtume S.A.W. alikataza utoaji wa rambi rambi baada ya siku ya tatu tangu msiba utokee, ili kuepuka urejeshaji wa huzuni kwa mfiwa, na pia ni haramu kutumia mali ya mali ya watoto yatima kwa ajili ya matumizi ya siku hiyo.
Ama kuhusu suala la kukaa roho ya maiti muda wa siku arubaini ardhini, basi jambo hili ni la ghaibu halijulikanwi katika Sheria, lakini jambo liliotajwa katika athari ni kwamba ardhi inalia juu ya mtu mwenye imani siku arubaini anapokufa. Ama kauli ya kwamba roho inakaa ardhini muda wa siku arubaini ni jambo tusilolijua na hatuna Hadithi sahihi ya Jambo hili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas