Kutumia Rangi ya Kijani Katika Mava...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Rangi ya Kijani Katika Mavazi

Question

Liko kundi la watu wanaotumia rangi ya kijani katika mavazi yao. Na wanarejesha hayo kwa rangi ya Mnara (Quba) wa Msikiti wa Mtume S.A.W. na baadhi yao wanasema: Mtume S.A.W. alipozaliwa mwezi wa mfunguo tatu alikuja Jiburilu (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) na mkononi mwake ameshika bendera ya kijani na huku akiipepea kwa ajili ya kufurahia mazazi ya Mtume S.A.W. na kwamba malaika angani wao pia walikuwa wakipepea bendera, je mambo haya ni kweli?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Rangi ya kijani ni ishara ya ustawi wa maisha bora, kwa hiyo inatajwa katika Qur`ani Tukufu kwamba rangi ya mavazi ya watu peponi na ni rangi ya makochi na yanayoegemewa. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi.} [AL INSAAN 21]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: { na watavaa nguo za kijani za hariri na at'ilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi} [AL KAHF 31]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wameegemea juu ya viti vya kijani na mazulia mazuri} [AR RAHMAAN 76].
Na Mtume S.A.W. amesema kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atamvalisha vazi la kijani siku ya Qiyama, akasema: "Watu watafufuliwa siku ya Qiyama, basi mimi na umma wangu tutakuwa juu ya mlima, na Mola wangu Mtukufu atanivalisha vazi la kijani, kisha nitaidhinishwa nisema yanayotakiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu niyaseme, basi hapo ni mahala paliposifiwa vizuri". [Imepokelewa na Imamu Ahmad]. Na pia akasema kwamba roho za Mashahidi zitakuwa katika tumbo la ndege wa kijani.
Ama Mnara (Quba) wa Sikiti wa Mtume umepakwa rangi ya kijani tangu mwanzoni mwa miaka ya elfu moja na mia mbili, hamsini na tatu (1253) Hiijria.
Ama kuhusu bendera ya kijani, basi Al Kharaitwiy amepokea Hadithi ya Asmaa Bint Abi Bakr Aswdeeq R.A. kwamba Zaid Bin Amro Bin Nafeel alitoka usiku wa kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. hadi akafika mlima wa Abi Qais, basi akaomwona mwanamume anashuka na ana mabawa mawili ya kijani, basi akasimama juu ya mlima wa Abi Qais kisha akaielekea Makah na akasema: Shetani amedhalilishwa, na masanamu yamebatilishwa, na mwaminifu amezaliwa. Kisha akakunjua nguo (kitambaa) na akaipepea Mashariki na Magharibi, basi vilionekana vilivyomo chini ya anga na nuru kubwa ikang'aa hadi ikakaribia kuyapofua macho yake, na akaogopa kwa hayo aliyoyaona.
Basi mwanamume huyo mwenye mabawa makubwa akashuka juu ya Al Kaaba, na nuru kubwa ikang'aa hadi Tuhama na akasema: ardhi ikasitawi na ikatoa maua yake, na akayaelekea masanamu ambayo yalikuwa katika Al Kaaba basi yote yakaanguka. Alswalihiy ameitaja Hadithi hii katika kitabu cha: [Sabeelu Al Huda Wa Arashaad], Na pia vitu vyingine vimethibitishwa kutuka kwake kama vile hekaheka za Majini, na kung'aa kwa nuru.
Na majaribio ya kisayansi ya kisasa yamethibitisha kwamba rangi ya kijani ina athari nzuri juu ya saikolojia ya binadamu. Kwa hiyo Basi rangi ya kijani ni ina sifa nzuri, na kujipamba nayo kwa ajili ya kupata maana hiyo ni jambo linalopendeza pia, na jambo lilo sahii ni kuwaachia watu na tabia zao, wakiyaelezea mapenzi yao kwa Mtume S.A.W. na imani yao ya visivyoonekana kwa kuifananisha kwao rangi ya kijana kuwa ni ya watu wa Peponi.
Ama kauli ya baadhi ya watu kwamba mambo hayo ni Bidaa, siyo sahihi, bali kauli yao yenyewe ndiyo ni ya Bidaa, kwani inaifanya milango ya halali kuwa finyu wakati ambapo Sheria ya Kiislamu imeipanua kwa upande mwingine, na kauli yao ina katazo la mionekano ya upendo ambayo watu huiishi katika kusherehekea siku ya Mazazi ya Mtume S.A.W., kutoka upande mwingine.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas