Mirathi ya Mke Aliyeachwa na Mume ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mirathi ya Mke Aliyeachwa na Mume Wake

Question

 Kaka yangu alikufa kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu tarehe 7/6/1998 katika hali ya uhai wa mama yake, na yeye alikuwa na mtoto wa kiume na mtoto wa kike ambao wawili hawa bado wadogo, baada ya kumtaliki mama yao, na matokeo ya talaka yakawa kama ifuatayvo:
1- Ugomvi mkubwa ulitokea kwa muda mrefu mwishoni mwa mwaka 1997, na hali kadhalika kabla ya tarehe hii ambapo wote wawili walikuwa wanakaa huko Marekani, kisha wakakubaliana kuwa talaka ndiyo ufumbuzi.
2- Marehemu alimtaka mke wake aache haki zake zote za mali Marekani na kumpa yeye umiliki wa mali zake zote zilizopohuko pamoja na ulezi wa watoto, na kujiuzulu kazi, kisha alirudi Kairo ili aweze kumtaliki, na hivyo ndivyo alivyofanya mke, akatuma barua yenye saini yake kwa mwanasheria wa mume kwa ajili ya kuipeleka mahakamani, ili mume aweze kupata mali zake zote Marekani pamoja na ulezi wa watoto.
3- Mhandisi Jamal… (wakiliwa kwanza wa wizara aliyestaafu), naye ni jamaa wa mume kama mjomba wake, na alikuwa na uhusiano mwema na mume na mkewe; kwa sababu ya kuwatembelea Marekani, na mke alikuwa akimtegemea katika kutatua matatizo yao, na mtu huyo ni wa daraja ya juu ya dini na tabia njema na kujiheshimu, na kwamba kukamilisha utaratibu wa mke kuachia haki zake za kifedha, mume alimwambia Bw. Jamal kuwa amekubaliana na mkewe kuwa mke mkabidhi vito, zawadi za dhahabu zilizopo mikononi mwake Kairo, pamoja na pete ya ndoa ili aweze kumtaliki.
4- Mke alifanya hivyo, ambapo alimkabidhi Mhandisi Jamal vito, zawadi na pete ya ndoa, sharti asimkabidhi mume vitu hivi isipokuwa mpaka atakapomtaliki. Na yote haya yametokea mwishoni mwa Januari 1998.
5- Mhandisi Jamala lishuhudia kuwa kweli alipata vitu hivi, akawasiliana na mume akamwambia, na mume akamwambia Bw. Jamal kuwa alimtaliki mke. Na hii ilikuwa mwishoni mwa Januari 1998.
6- Tarehe 18/2/1998, mume alipeleka ombi la dai la talaka kwa mahakama ya Marekani akitaka mirathi, ulezi wa watoto kwa mujibu wa sheriaya Marekani, aliambatanisha barua ya mkewe ya kuacha haki zake pamoja na ulezi wa watoto, kisha mahakama ilikubali ombi la talaka, mirathi na ulezi, na hii ilikuwa tarehe 21/4/1998.
7- Kaka yangu alikufa tarehe 7/6/1998, sasa mke aliyeachwa anataka kushirikiana na watoto wawili katika mirathi; kwa mtazamo wake kuwa tarehe ya talaka ni ileile ya kutoa uamuzi wa mahakama ya Marekani ya 21/4/1998, pia yeye hakiri kuwa kuwepo talaka mbele ya mahakama ya Marekani na talaka kwa mali haina Edda, kama tulivyojua -na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi- na talaka hii ni ndogo.
Je mke huyu ana haki ya kushirikiana na watoto wake wawili katika mirathi ya baba yao?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ikiwa hali kama ilivyokuja katika swali, basi mke anayeachwa kamwe hamrithi mtalaka wake aliyekufa; kwa sababu talaka iliyotajwa ni kubwa kwa kuwa ilikuwa kwa kulipa mali, na hukumu inayoamuliwa katika Fiqhi kuwa talaka kubwa ni kizuio kisheria cha mirathi, kwa hiyo mke anayeachwa hamrithi mume mtalaka aliyekufa, hata kama alikufa katika muda wa Edda yake, zaidi ya hayo kifo chake kilitokea baada ya zaidi ya miezi minne ya talaka ya mke, kwa mujibu wa jinsi swali lilivyoulizwa, na hii inatosha kuwa mke alimaliza Edda yake kwa kawaida ndani ya muda huu na kabla ya kifo cha mume.
Na Mwenyezi Munguni Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas