Kutayarisha Mawazo ya Suala la Fatw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutayarisha Mawazo ya Suala la Fatwa.

Question

Wanachuoni wanasema: Suala la fatwa linavipitia vipindi vinne katika akili ya mwanazuoni wa fiqhi kabla halijatolewa, na miongoni mwa vipidi hivyo ni “Kutayarisha mawazo (Taswiir) ya Suala” la maudhui ya fatwa. Je, nini ufafanuzi wa istilahi hii, na nini vigezo vya matayarisho sahihi ya Suala la Fatwa? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Suala la fatwa linapita vipindi vinne katika akili ya mwanafiqhi kabla ya kutolewa, navyo ni: Kutayarisha mawazo (Taswiir), kuainisha, kuweka hukumu na kutoa fatwa. Vipindi hivi ni tangulizi za fatwa, na hali ya kuwa tangulizi hizi ni sahihi, basi matokeo yake, yaani fatwa, yatakuwa sahihi pia, na haiwezekani tangulizi hizi kuwa sahihi isipokuwa kwa kuangalia vigezo, kwa hiyo, ni muhimu kuangalia vigezo vya tangulizi hizi.
Mwanzo wa tangulizi hizi ni kutayarisha mawazo kuhusu fatwa (Taswiir), asili yake ya kiarabu ni kitenzi (Sawara), Ibn Al-Athiir katika kitabu chake: [An-Nihaya Fi Ghariib Al-Hadiith: 3/59, Ch. ya Al-Maktabah Al-Ilmiyah] anasema: “Sura katika maneno ya waarabu ni umbo la kitu, hakika yake, au sifa yake, na inasemwa kwa mfano: sura ya kitenzi yaani umbo lake, na sura ya jambo yaani sifa yake”.
Katika kitabu cha: [Al-Mu’jam Al-Wasiit: Kidahizo cha: (Sa Wa Ra), Uk. 528, Ch. ya Dar Ad-Da’wah]: “Aliisawiri, yaani aliichora akilini mwake sura ya mwili, na katika uteremshaji Mtukufu: {yeye ndiye anayekutengenezeni sura matumboni jinsi apendavyo}”.
Alsawiri kitu au mtu, yaani alimchora katika karatasi au ukuta kwa kalamu, na alisawiri jambo, yaani alilieleza kubainisha sehemu zake, pia inasemwa: Nilitayarisha mawazo ya jambo fulani, yaani nilijua hakika yake na sura yake.
Al-kufwiy [Uk. 559, (kwa mabadiliko kidogo), Ch. ya Muassasat Ar-Risalah] anasema: “Neno sura huenda likawa linaonesha muundo wa maana ya dhahania, kwa sababu maana zina muundo, mpangilio, na mnasaba, na hayo yote huitwa sura, kama ikasemwa: Sura ya suala, Sura ya tukio, na Sura ya elimu za kihesabu, n.k.,”.
Kupata mawazo (Tasawur), ni kupata sura ya kitu ndani ya akili, au kufahamu misamiati, kwa mujibu wa istilahi ya wanamantiki; kwa hiyo, kupata mawazo na kutayarisha mawazo (Taswiir) istlahi hizi mbili zina maana moja.
Kutayarisha mawazo (Taswiir), kwa mujibu wa istilahi ya wanamsingi na wanafiqhi, hakika haupatikani ufafanuzi maalumu kutokana na istilahi zao, na huenda wakawa wameutosha uwazi wa maana yake ya kilugha; kwa vyo vyote vile, wanakusudia kutayarisha mawazo kuwa ni: kubainisha hakika ya kitu ili kidhihirike katika akili ya mwanafiqhi, na katika hali hii haututoshi ufafanuzi ambao ni njia ya kupata mawazo kimantiki, kwa sababu kupata mawazo ya suala kifiqhi kunakaribiana na ukweli ambao ni nguzo ya msingi kati ya nguzo za kutoa fatwa.
Imamu Al-Haramain anasema: “Mwanzo wa ufunguaji ni kutayarisha mawazo ya suala”, [Al-Burhan: 2/233, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-ilmiyah].
Kama alivyosema: “Ilivyo muhimu sana ni: kutayarisha mawazo ya Qiyasi ya ulingano, na kuitofautisha na Qiyasi ya maana”. [Al-Burhan: 2/53].
Pia akasema: “Suala likihakikishwa na upande wa kutayarisha mawazo, hapatakuwa na tofauti’. [2/256].
Al-Ghazaliy alipokuwa anaizungumzia elimu ya Masahaba na waliowafuata, anasema: “Wao, yaani Masahaba, wameushughulikia uwekaji wa kanuni na kudhibiti nguzo za Sheria, na kuasisi mambo makubwa, na hawakutayarisha mawazo kwa bahati, na hawakugawanya milango kwa urefu na kwa wingi, lakini walikuwa wakijibu matokeo vya kutosha, kisha mambo yakabadilika, na nyakati zikapita, na bidii zikapungua, na sera na sifa zikabadilika, na maimamu wakawa wanahitaji kukadirisha masuala, na kusawirisha na matokeo kabla hayajakuwa kamili, hata wanafunzi nao waweze kuyachukua kwa urahisi, na bila ya ugumu na taabu”. [Al-mankhuul: Uk. 608, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Ibn Daqiq Al-Id, kwenye utajo wa suala la matini zinazopingana zenyewe kwa zenyewe, moja yake ni kwa ujumla, na nyingine ni kwa umahususi, anasema: “kuhakikisha hivyo mwanzoni, hutegemea kutayarisha mawazo ya suala”. [Ihkaamul-Ahkaam: Uk. 289].
Na matini nyingine, ambazo zinatufahamisha kuwa kutayarisha mawazo ya suala yaani kuyafahamu yalivyo, ili mwanafiqhi asonge mbele na vipindi vifuatavyo, kama vile: Kuainisha suala… n.k., na kwa umuhimu wa kipindi cha kutayarisha mawazo ya suala, Ibn As-Salah anaona kuwa ufahamu wa kweli wa masuala haupatikani ila kwa mwanafiqhi mmbobezi, mwenye hadhi ya utaalamu wa fiqhi. [Adabul-Fatwa: 48].
Wanachuoni walitaja kuwa: haijuzu kwa Mufti kuzembea kuifahamu fatwa, au kuitoa kwa haraka kabla hajaichunguza katika suala linaloulizwa, kwa hiyo, watungaji wa Adabu ya kutoa fatwa walitaja kuwa: Mufti lazima azingatie karatasi ya fatwa neno kwa neno, na aangalie Zaidi mwishoni mwake kuliko mwanzoni, na akipata tatizo, basi amuuliza mwomba fatwa, kisha adhibiti muandiko kwa masilahi ya nafsi yake na wengine, na kama asipofahamu suala, basi analazimika kutotoa jawabu, kwa kutoweza kuleta ufumbuzi unaofaa, pia lazima amuulizia mwenye swali kusudio na muradi wake, ili aweze kutoa jawabu sahihi la suala lake. [Adabul-Fatwa, na Ibn As-salah:uk. 124].
An-Nawawiy anasema: “Mufti asipolifahamu swali kwa undani, au hakuhudhuria tukio, As-Saimariy anasema: Mufti anatakiwa kuomba maelezo zaidi ili aweze kujibu, au aandike: sikufahamu swali… Na Al-Khatiib anasema: Mufti asipofahamu swali amwongoze mwenye swali atafute Mufti mwingine, wala asitoe fatwa mpaka atakapolijua jibu”. [Adabul-Fatwa: Uk. 75, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Ibn As-Salah katika kauli yake ya juu ameonesha kuwa kutayarisha mawazo ya suala ni sharti la kuleta ufumbuzi unaofaa nalo, kwa sababu Mufti anapotafuta hukumu ya suala jipya, azifuate njia kadhaa kwa ajili ya kuifikia hukumu yake, na miongoni mwa njia hizi ni kuleta sababu ya hukumu ya suala lililotangulia na kuitumia katika suala hili jipya. Kwa hiyo, twaweza kuunganisha lisilokuwepo na linalokuwepo, ambayo huitwa; Qiyasi ya Sheria, na haiwezekani kuleta ufumbuzi pasipo na kulifahamu kwa yakini suala ambalo anataka kuliunganisha.
Adabu hizi zote walizozitaja watungaji wa Adabu za kutoa Fatwa zinashirikiana kuleta mambo kadhaa yanayofaa yawe kama Vigezo vya kulifahamu kiundani suala la fatwa, na kutayarisha mawazo ya suala ni lengo la Sheria, ambalo si jambo la hiari kwa mwanafiqhi, afanye asifanye, kwa sababu kulifahamu suala kimakosa, kwa sababu yeyote iwayo, matokeo yake ni kosa katika utoaji wa fatwa. Zaidi ya hayo, Mufti atapata dhambi, akiwa na kasoro ya kulifahamu suala husika, kwa sababu anasema yanayomuhusu Mwenyezi Mungu bila ya elimu, na hii haijuzu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo}. [AL ISRAA: 36].
Ili Mufti aweze kuifikia ngazi kamili na sahihi ya kutayarisha mawazo, lazima aangalie mambo muhimu yafuatayo:
Kwanza: Kukusanya kiasi kikubwa zaidi cha habari za suala la fatwa, kama anakijua chake, vipengele vyake, aina zake, namna lilivyotokea, sifa zake kuu, pande zake, na maendeleo yake. Kazi kama hii ni nyepesi kwa mtazamo wa mapinduzi ya media ya kisasa, lakini anahitaji pia kuutekeleza na kuutumia ukweli wa suala ili aweze kukamilisha ufahamu wake kuhusu suala hilo. Mkusanyiko huu unahitaji kurejea kwa wataalamu wa elimu zilizo mbali na elimu ya Sheria, kama vile: tiba na uchumi, n.k.
Pili: Kuuliza kwa kurefusha katika hali ya kuwa mwenye suala ni mtu maalumu, ambapo Mufti anaweza kumwuliza juu ya mambo yanayomtatiza, na kubaini yasiyo dhahiri, kwa ajili ya kufikia ufahamu madhubuti, na hivi ndivyo ilivyopokelewa na Ibn Abbas RA, alisema: “Alipokuja Mai’z ibn malik Mtume S.A.W, alimwambia: Wewe huenda ulibusu, au uligusa, au uliona, akasema: La, Ewe Mtume wa Allah, akasema: Je, ulimwingilia?, akasema: hapo aliamuru apigwe mawe”. [Muttafaq, na tamko hili ni la Bukhariy].
Na imepokelewa na An-Nu’man Ibn Bashiir, kuwa baba yake alimwendea Mtume S.A.W, akasema: “Mimi nilimtoa mwanangu huyu awe mtumishi, akasema: Je, umewatoa watoto wako wote mfano kama ulivyomfanyia mtoto huyu?, akasema: La, akasema: Basi mrudishe”. [Muttafaq].
Dalili hapa ni maswali ya Mtume S.A.W, kwa lengo la kuitoa hukumu ya tukio baada ya kutayarisha mawazo kamili juu yake.
Mufti huenda akawa anatumia fasili kwenye kutayarisha mawazo au suala husika kiukamilifu, na kwenye kutojua kwa uwazi hali ya mwenye swali, au ikiwa suala ni la kiujumla, kwa mfamo, anasema: Ikiwa suala ni kadhaa, basi hukumu ni kadha, na kadhaa wa kadhaa… n.k., na hii ni dalili ya hukumu ya Mtume S.A.W, kama ilivyopokelewa na Salama Ibn Al-Muhabiq kuwa Mtume wa Allah, alitoa hukumu kuhusu mwanamume aliyemwingilia mjakazi wa mkewe: “Akimlazimisha, basi mjakazi ni huru, na mwanamume ampe mwenzake kijakazi mwingine, lakini kijakazi akiwa na hiari yake, basi ni haki ya mwanamume, pamoja na kumpa mwenye chake kijakazi mwingine”. [Wameipokea Ahmad, Abu-Dawuud, na An-Nasaiy].
Tatu: Mufti lazima ajue kwa uwazi hali za watu, wanaoishi kwa mchanganyiko, na ajue njia zao katika matendeano, ili apate uwezo wa busara, ambapo hupelekea kutofautisha kati ya haki na batili, kwa sababu aliyeuliza fatwa na hali yake ya kuwa si mjuzi wa uhalisia wa watu, na mbali na kuchanganywa, hali hii huenda ikampelekea kufanya kosa wakati akitayarisha mawazo. Kwa hiyo, Ibn As-Swalah anasema: “Haijuzu kwa Mufti atoe fatwa zinazohusu yamini, makiri, n.k., na mambo yanayohusu matamshi isipokuwa mwenyeji wa mahali pa lafudhi hizi, au anakuwa na ujuzi wa muradi wao wa matamshi na matumizi, kwa sababu kama si hali hii, basi makosa yake yatazidi kama majaribio yanavyoonesha”. [Adabul-Fatwa: Uk. 71].
Hayo yote yanafungamana wazi wazi na ujuzi wa matokeo ya matendo, kwa hiyo, kwa kweli kuna uhusiano wa kusababisha kati ya ujuzi wa Mufti wa maisha, usomaji wake kwa uwazi , na ujuzi wa matokeo ya matendo, kwani ujuzi wa kwanza ni sababu ya pili.
Kwa mujibu wa hayo, kuangalia vigezo hivi katika kutayarisha suala, hupelekea usahihi wa ufahamu, kwa sababu, usahihi wa mwanzo hujenwa na usahihi wa mwisho, na maana ya mwanzo hapa ni mawazo, na maana ya mwisho ni kutoa hukumu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas