Kuomba Dua Katika Swala kwa Dua Il...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuomba Dua Katika Swala kwa Dua Iliyopokelewa na Isiyopokelewa Kutoka kwa Mtume (S.A.W).

Question

 Je! Ni ipi hukumu ya kuomba dua katika Swala kwa dua iliyopokelewa na isiyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W.?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Kuomba dua ni kitenzi jina cha kusema, nimeomba dua ya kitu fualni, kwa maana kutaka kitu kwa sauti na maneno yako. [Maqayiis Al-lugha 2/279, Dar Al-Fikr].
Ibn Mandhur amesema: mtu ameomba dua: yaani ameita, na jina ni: dua, na nimemwita mtu fulani: yaani nimemwita kwa sauti” [Lisan Al-Aarab 16/1386, Darul Maarif].
Na dua kwa upande wa Sheria kama alivyosema Al-Khatabi: “Maana yake ni mja kumwomba Mola wake S.W., uhifadhi, na kuomba msaada kutoka kwake. Na ukweli wa hali hii ni kuonesha ukosefu wa mja kwa Mwenyezi Mungu S.W., na kukana uwezo na nguvu, na hali hii ni ya utumwa, na kuhisi unyenyekevu, na dua ina maana ya kumsifu Mwenyezi Mungu, na kuongeza ukarimu na wema kwake.” [Shanu Duaa kwa Al-khatabi uk. 4, Darul Thaqafah Al-Arabiyah]
Na kuomba dua katika swala na nje yake kunapokelewa kwa mujibu wa Aya na Hadithi nyingi zilizotajwa kuhusu fadhila ya dua, Mwenyezi anasema: {Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Ninapokea maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniombe Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka} [AL BAQARAH 186], na Mwenyezi anasema: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.} [GHAFER 60], na Mwenyezi anasema:. {Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka} [AL AARAF 55], na Mwenyezi anasema: {Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usiiswali Swala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo} [AL ISRAA 110], na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., anasema, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Aswhab Al-Sunan na Al-Hakim kutoka kwa Al-Nu'man Ibn Bashir, anasema: "dua ni ibada, kisha akasoma {Niombeni nitakuitikieni} [GHAFER 60]", na imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi kutoka kwa Anas kwamba Mtume, S.A.W anasema: "Dua ni ubongo wa ibada". Vile vile imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi na Ibn Majah na Ibn Hibban kutoka kwa Abu Hurayrah akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.: anasema: "Hakuna kitu chochote ni karimu kwa Mwenyezi Mungu zaidi kuliko kuomba dua", na imepokelewa kutoka kwa Al-Dilimiy katika kitabu cha: [Al-Firdaws], Ahmad na Al-Bukhari katika kitabu cha: [Al-Adab na Al-Hakim] kutoka kwa Anas R.A., anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W anasema: "Hakika mja wakati anapoomba dua hakosi jambo moja miongoni mwa mamabo matatu: dhambi inasamehewa, au heri inaharakishwa kwake, au heri inahifadhiwa kwake".
Na kuomba dua katika swala kwa dua iliyopokelewa na isiyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W ni halali, kwa mujibu wa kauli ya Mtume S.A.W, katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ahmad na Abu Dawood, kutoka kwa Ibn Masuod anasema: "Tulikuwa tukikaa pamoja na Mtume S.A.W. katika swala tunasema: “Assalaamu ‘ala-Allaahi min ‘ibaadihi (amani ziwe juu ya Allah kutoka kwa waja Wake) Assalaamu ‘alaa fulaanin wa fulaan (Amani zimfikie fulani na fulani) Mtume S.A.W akasema: "Msiseme Assalaamu ‘ala-Allaah, kwani Allaah Mwenyewe ni As-Salaam, lakini kama mmoja wenu akikaa basi, aseme: Maamkuzi mema, na rehema na mazuri yote, ni kwa Mwenyezi Mungu, amani zishuke juu yako Ewe Mtume na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu walio wema, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu na ninakiri kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, kisha achague mmoja wenu dua aliyoipenda ili aiombe". Katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imam Muslim: "Kisha achague miongoni mwa dua anayoitaka". Na katika Hadithi nyingine: "Kisha baada ya hivyo achague miongoni mwa dua anayoitaka, au anayoipenda".
Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., hakuainisha dua maalumu, na Maswahaba zake Mtume walikuwa wakiomba dua katika swala ambazo hawajajifunza kutoka kwake, na Mtume S.A.W., hakuwakataza. Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawood katika Sunan yake kwamba mtu alikuwa akiomba dua katika swala yake kwa dua ambayo hajajifunza kutoka kwa Mtume na Mtume S.A.W., Na Mtume S.A.W., hakumkataza. Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Jaber Al-Ansari, R.A, anasema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alimwuliza mtu mmoja, unasemaje katika swala? Akasema: Nasoma Tashahhud, namwomba Mwenyezi Mungu aniingize peponi na najikinga kwake kutokana na moto, lakini naapa kwa Allah siwezi kuomba dua kama unavyoomba na kama Muaz anavyoomba, Mtume S.A.W. anasema: mimi na Muaz tunaomba dua kama unavyoomba" [Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah na wengine] na Mtume, S.A.W aliposema "Katika sujuda mwombeni dua nyingi" na hakuainisha dua maalumu, hali hi ni dalili ya kwamba Mtume S.A.W amerahisisha dua zote.
Ar-Ramli anasema katika kitabu cha [Nihayatul Muhtaj]: “Vilevile inaruhusiwa kuomba dua baada ya kusoma Tashahhud ya mwisho kama tunaomba mambo ya dini au ya kidunia kama nikisema Ewe Mola wangu naomba nipatie mwanamke mzuri, kwa mujibu wa Hadithi isemayo: "Kama mmoja wenu akikaa katika swala, aseme Maamkizi mema, na rehema na mazuri yote, ni kwa Mwenyezi Mungu hadi mwisho wa Tashahhud, kisha achague miongoni mwa dua anayoitaka na anayoipenda".
Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim, aidha imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari: "Kisha achague miongoni mwa dua anayoipenda ili aombe", na imepokelewa kutokana na maana ya matini hii kwamba inachukizwa kuacha dua”. [Nihayatul Muhtaj kwa Ar-Ramli 1/511, Al-Halabiy].
An-Nawawi amesema katika kitabu cha: [Rawdhatul Twalibiin]: “Inapendekeza kuomba dua baada ya kumsalia Mtume, na mwenye kuomba dua ana uhuru wa kuomba mambo anayoyataka miongoni mwa mambo ya dunia na Akhera.” [Rawdhatul Twalibiin kwa An-Nawawi 1/256, Al-Maktabul Islami].
Ad-Dardeer Anasema katika kitabu cha: [Al-Sharhul Kabiir]: “Inaruhusiwa mtu kuomba dua kama anavyopenda katika mambo yote mazuri siyo kwa mambo ya dini tu, bali kwa mambo ya kidunia pia.” [Al-Sharhul Kabiir Limukhtasar Khalil 1/251, Dar Al-Fikr].
Qudaamah anasema katika kitabu cha [Al-Mughni]: “Al-Athram anasema: nilimwambia Abu Abdullah: Hakika hawa (Baadhi ya watu) wanasema: hatuombi dua katika swala iliyofaradhiwa isipokuwa kwa dua zilizotajwa katika Qur'ani tu, Abu Abdullah akakasirika, na akasema: Nani anasimama juu ya kauli hii, na zilipokelewa Hadithi nyingi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., kinyume na kauli yao hiyo. Abdullah Ibn Ahmad anasema: nimemsikia baba yangu anasema katika sijida yake: Ewe Mwenyezi Mungu, kama unavyohifadhi uso wangu usisujudu isipokuwa kwako tu, basi uhifadhi uso wangu kutokana na kuomba wengine. Abdul Rahman alikuwa akisema hivyo katika sijida yake, na amesema: nilisikia dua hii kutoka Athawri ambapo alikuwa akisema hivyo katika sijida yake. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Al-Mundhir kutoka kwa Imam Ahmad anasema: Hakuna kitu kibaya kwamba mtu anaomba dua kwa mahitaji yake yote, kutokana na mambo ya dunia na Akhera, na jambo hili ni sahihi, Mungu akipenda, kufuatana na Hadithi za Mtume, ambapo Mtume, S.A.W. anasema: "Kisha achague kutokana na dua", na akasema: "Kisha ajiombea dua kama anavyotaka", na kusema: "Kisha baada ya hivyo aombee kama atakavyo".
Na Imepokelewa kutoka kwa Anas, R.A., anasema, Umu Sulaim alikujia Mtume, S.A.W., akisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nifundishe dua ili niombe kwa dua hii katika swala zangu, Mtume S.A.W., anasema: "Umshukuru Mwenyezi Mungu mara kumi, na umtakase mara kumi, kisha umwombe kama unavyotaka, Mwenyezi Mungu atasema: Ndiyo, ndiyo, ndiyo". Imepokelewa kutoka kwa Al-Athram, na kwa sababu Maswahaba zake Mtume S.A.W., walikuwa wakiomba dua katika swala zao kwa yale ambayo hawakujifunza, na Mtume S.A.W., hakuwakataza, kwa hivyo Mtume, S.A.W., alipomwuliza mtu mmoja unasema nini katika swala zako? Akasema: ninasoma Tashahhud, kisha ninamwomba Mwenyezi Mungu aniingize peponi, na ninajikinga kwake kutokana na moto, basi Mtume S.A.W., akakubali dua yake hii, pasipo na kumfundisha dua hii. Na wakati Mtume, S.A.W., aliposema kuwa: katika sijida mwombeni dua nyingi, hakuainisha dua maalumu ili waziutmie katika maombi yao, na hali hii inaonesha kwamba inaruhusiwa kuomba dua zozote, isipokuwa dua iliyotajwa kwa dalili”. [Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 1/322, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Kwa hiyo, dua katika swala inaruhusiwa ikiwa imepokelewa au haipokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas