Kundi Lenye Kuzuia Utekelezaji wa S...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kundi Lenye Kuzuia Utekelezaji wa Sheria.

Question

Ni nini makusudio ya neno kundi lenye kuzuia utekelezaji wa Sheria? Na je, inafaa kushiriki kwenye kitendo cha kulimaliza na kuua watu wake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Ama baada ya utangulizi huo:
Neno kundi kwa upande wa lugha: Ni mkusanyiko wa watu, lakini wakati mwingine hutumika kwa mtu mmoja, na kusudio ni kama kundi hilo hilo, na kundi la vitu maana yake ni sehemu ya hivyo vitu. Amesema Mujahid: Kundi linaanzia mtu mmoja mpaka alfu moja, ikasemwa kuwa ni kuanzia mtu mmoja na kuendelea, imepokelewa pia kuwa, uchache wa kundi ni kuanzia mtu mmoja, anasema Ataa: Uchache wake ni kuanzia watu wawili (Kamusi ya Lisan Al-Arab 9/223 Ch. ya Dar Swadir) ... Ama kundi la watu ni kama vile mkusanyiko unaozunguka mtu mmoja au kitu. Waarabu hulizingatia kundi kwa idadi inayofahamika. (Kitabu Maqayiis Al-Lugha, 3/432 Ch. ya Dar Al-Fikr)
Na kuzuia: Ni kuzuia, ni kuweka zuio kati ya mtu na kitu ambacho anakihitaji, na huitwa: Kuzuia kitu, pia husemwa: Amemzuia kutokana na kitu hiki na hiki, husemwa pia amemzuia kupata haki yake, na kuizuia haki yake kutoka kwake “Kitabu Taj Al-Arus, 22/218, Ch. ya Dar Al-Hidaya”, kitenzi kuzuia ni kuacha kwa makusudi, na kuzuia kitu ni kuepukana nacho na kuchukua hatua inayozuia kati yake na mwenye kuzuia.
Kusudio la kundi lenye kuzuia utekelezaji wa Sheria katika maana ya msamiati wa Kisheria: Ni mtu au kundi la watu ndani ya Dola ya Kiislamu lililoungana wazi wazi ili kwenda kinyume na mfumo mkuu na kuachana na ufuasi wa sheria pamoja na adhabu zake kwa kutumia nguvu kubwa, na hili ni kama vile ikiwa watu wa kijiji kimoja wamejizuia kutekeleza baadhi ya mambo ya lazima katika Uislamu au ulazima wa kutoshelezeana - ikiwa ni kundi la Kiislamu - au kuzuia baadhi ya haki ambazo ni za lazima zikiwa ni sehemu ya sharti la kuishi ndani ya nchi - ikiwa hilo kundi ni la watu wa Dhimma au wanaoishi kwa makubaliano - na kuchukuliwa sababu za kupigwa ni kusimamisha mamlaka ya kiongozi na kulazimisha kwake kutekeleza yaliyo lazima na kuheshimu sheria .
Kwenda kinyume kwa kundi hili huenda ikawa asili yake ni jambo muhimu katika Dini, pia huenda ikawa ni katika mambo ya matawi katika Dini na juhudi za wanazuoni wa Fiqhi wake ambao wanateuliwa na kiongozi ambapo wananchi wanalazimika kuwafuata, kutokana na hilo kundi lenye kuzuia huenda likawa ni kundi lililoiacha Dini ya Kiislamu, lakini huenda likawa ni kundi lenye kufanya maovu miongoni mwa Waislamu, au likawa kundi lenye kuendesha vita kama vile kundi la majambazi na wale wenye kwenda kinyume na amri za kiongozi na mfano wa hao.
Katika hali zote kundi hili lenye kuzuia utekelezaji wa Sheria linakuwa ni la uasi dhidi ya sheria na mamlaka halali, wakienda kinyume na mfumo mkuu, wanaokwenda kinyume na makundi ya uma na mifumo yake mikuu, wakitoa wito wa kuvuruga umoja na mshikamano wa kijamii na kisiasa, huzingatiwa kwenda kwake kinyume pamoja na kulizuia kwa kutumia nguvu ni kukinga kuibuka fitina na kutishia mfumo pamoja na kuondoka sura ya nchi na kutishia watu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua} [AL BAQARAH, 191], na Anasema: {Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu} [AL BAQARAH, 193].
Katika kanuni za Sheria ni kuwa: “Ikiwa kutakuwa na utatanishi katika vitu vyenye madhara, basi huachwa kile chenye madhara makubwa zaidi na kufanywa chenye madhara madogo” Kitabu Al-Ash-bah wa An-Nadhair cha Imamu As-Suyutiy, uk. 87, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya, na madhara ya fitina ni mabaya zaidi kuliko kuua au kupigana kama inavyooneshwa kwenye Aya za Qur`ani Tukufu, na kwa maandiko haya Sheria imehalalisha kulipiga vita kundi hilo lenye kuzuia utekelezaji wa Sheria - ikiwa itapatikana njia - ya kuondoa Fitina zake pamoja na kuondoa madhara ambayo yanatokana na migongano na kupingana na mifumo ya usalama, Sheria na mifumo mikuu, kuwashambulia watu wa makundi haya wakati huo inakuwa ni wepesi zaidi ya shari mbili na madhara yake ni machache, kama vile kuitoa muhanga sehemu ya kundi hilo na kubakia wengine wakiwa salama ni jambo la haki na sahihi katika mizani ya akili na uhalisia wa wanadamu na Sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini jambo la lazima kwa kiongozi au mtawala ni kwenda hatua kwa hatua kwanza kwa kulitisha kundi hili la kujitenga, wala asianze hatua ya kulipiga isipokuwa baada ya kuelezewa na kupewa hoja, kisha kushambuliwa hakukusudiwi kuwaangamiza kabisa isipokuwa kusudio ni kuwakemea na kuwarudisha kwenye njia sahihi.
Anasema Imamu Al-Mawridy katika kitabu cha: [Al-Ahkam As-Sultania, uk. 73: 75 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Ikiwa kundi la Waislamu litakiuka na kwenda kinyume na mtazamo wa umma, kisha likajitengenezea madhehebu yake ya kipekee, ikiwa wafuasi wake hawatatoka – kwa kuwa kwao katika madhehebu hayo – katika utiifu wa kiongozi wala kwenda kinyume na hukumu za nchi wakawa ni watu waliotofauti wakiwa wanapata nguvu na kuungwa mkono, basi wataachwa bila ya kushambuliwa, na watafanyiwa hukumu za uadilifu katika yale yanayo lazimu kwao na kuwa na haki, kwani kundi la Khawarij lilijitokeza na kumpinga Ally bin Abuu Twaalib R.A, kwa kuwa kinyume na mtazamo wake, na akasema mmoja wao akiwa anatoa hotuba juu ya mimbari yake: Hakuna hukumu isipokuwa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ally R.A, akakasema: Neno la haki limekusudiwa batili. Kwetu mna mambo matatu: Hatuwazuii kwenye Msikiti wa Mwenyezi Mungu kutaja humo jina lake, wala hatutaanza kuwapiga vita, wala hatuwazuii kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu madamu tu mpo nasi. Ikiwa wataonesha imani yao hali ya kuwa wamechanganyika na watu waadilifu, kiongozi atawawekea wazi ubaya wa imani yao na ubatilifu wa kile walichokianzisha lengo ni kuwarejesha kwenye imani sahihi na kukubaliana na umma, na kiongozi akapitisha hukumu ya kuadhibiwa baadhi yao kwa kuwaadhirisha kutokana na uharibifu kama ni njia ya ni kawatia adabu na kukemea pasi na kufikia kiwango cha kuwapiga au kuwapa adhabu kali ya kosa la jinai, imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kuwa amesema: “Si halali kumwaga damu ya Mwislamu isipokuwa kwa moja ya mambo matatu: Ukafiri baada ya kuamini, au uzinzi baada ya kuoa, au kuua nafsi pasi na hiyo nafsi kuua”. Ikiwa kundi hili litajirekebisha na kuungana na watu wa haki na Dola pamoja na kuchanganyika na umma, ikiwa halijajitenga na haki wala kuacha utiifu basi halitashambuliwa maadamu tu lipo kwenye utiifu na utekelezaji wa haki.
Kuna kundi la Khawarij lililompinga Ally R.A. huko Naharawan, kuna muda lilikuwa na kiongozi waliyemtii, naye kwao alikuwa anawatosheleza kwa usimamizi, mwishowe wakamuua wakatakiwa kumleta kwangu aliyemuua, wakakataa na wakasema: Sisi sote ndio tuliyemuua, akasema: Mleteni kwangu ili kisasi kilipizwe, akaenda kwao na kuwaua wengi wao. Ikiwa kundi hili ovu lingejizuia na utiifu kwa kiongozi na kuzuia vile vilivyokuwa kwao miongoni mwa haki na kujiwekea njia pekee ya kuchuma mali na kutekeleza hukumu, ikiwa watafanya hivyo pasi na wao kuegemea kwa kiongozi, basi mali waliyoichuma itakuwa ni ya uporaji haitaondoka kwenye dhima yao, na hukumu walizotekeleza ni zenye kurudishwa pasi na kuthibiti haki, hivyo watapigwa vita katika hali mbili ili ipatikane dalili na kuwa watiifu.... ikiwa Imamu amemuiga Amir katika kuua wale wenye kuzuia miongoni mwa waovu, basi kabla ya kuwashambulia ataanza kutoa onyo kwao, kisha atawapiga ikiwa wataendelea na uovu wao na wala hataanza tu na kuwashambulia, na kuwashambulia kwao kunatofautiana na kuwashambulia washirikina na wale walioritadi kwa namna nane”.
Anasema Imam Al-Mawardiy kuhusu kundi lenye kuzuia katika watu walioacha Uislamu [Kitabu- Al-Ahkam As-Sultania, Uk. 70: 71]: “Hali ya pili kuachana na Dola na kujitenga na Waislamu mpaka wanakuwa ni wenye kuzuia, basi ni lazima kuuawa kwa kuritadi kwao na kuwa mbali mitazamo yao na Uislamu na uwazi wa dalili zake, watapigwa vita baada ya kupewa onyo na hoja ya hukumu ya kuuliwa watu wa vita katika kupigana kwao kwa uwazi na kuuliwa kwa kukiuka kwao”.
Imepokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake kutoka kwa Abdillah amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Si halali kumwaga damu ya Mwislamu anayeshuhudia kuwa hakuna Mola wa haki isipokuwa Mwneyezi Mungu na mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa mambo matatu: Aliyeoa akafanya uzinifu, aliyeua nafsi bila nafsi na aliyeiacha Dini yake kwa kujitenga na umma”.
Anasema Imamu An-Nawawiy katika sherehe ya Hadithi “Sherehe ya An-Nawawiy ya kitabu cha: [Sahih Muslimu, 11/165, Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby – Beirut]: “Ama kauli yake Mtume S.A.W: - Na mwenye kuacha Dini yake na kutengana na umma - ina maana ya jumla kwa kila mwenye kuuacha Uislamu kwa namna yoyote itakayokuwa, basi ni lazima auawe ikiwa hatarudi tena kwenye Uislamu. Wamesema wanachuoni: Inakusanya pia kila mwenye kuachana na umma wa Kiislamu kwa uzushi au uovu au yasiyokuwa hayo, vile vile wenye kutoka kwenye mfumo wa Uislamu”. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Amesema Imamu Al-Qurtwubiy katika kitabu cha: [Al-Mufham, 5/40, Ch. ya Dar Ibn Kathir, Ch. ya Dar Al-Kalim At-Tayyib]: Uwazi wa kauli yake: “Mwenye kutengana na umma” hiyo ni sifa ya mwenye kuacha dini yake, kwa sababu pindi anaporitadi anakuwa ameachana na umma wa Waislamu, na inamuhusu kila mwenye kutoka na kuachana na Waislamu hata kama hajaritadi, kama vile mwenye kuzuia au kuukana utekelezaji wa adhabu ya uhalifu wa jinai pale inapowajibika, na anapambana kwa ajili ya hilo, kama vile watu waovu, majambazi wenye kupigana waliokuwa nje ya Uislamu na waiso kuwa hao. Amesema: kuzungumza kwao tamko la kujitenga na umma wa Kiislamu ni kwa njia ya ujumla na kama isingekuwa hivyo, basi isingefaa kuwajumuisha wote, kwa sababu inalazimisha kukanushwa yule aliyetajwa damu yake halali hivyo haifai kukusanya wote.
Maneno ya Sheria yamejitenga na hilo, yameonesha kuwa sifa ya kujitenga na umma inawakusanya hawa wote. Amesema: Ukweli wake ni kuwa kila mwenye kujitenga na umma wa Waislamu, basi ameacha Dini yake, tofauti na mtu aliyeritadi anakuwa ameacha yote, na mwenye kujitenga pasi na kuritadi anakuwa ameiacha sehemu ya Dini yake”.
Kuua watu wenye kujitenga wakati mwengine kunakuwa kwa mambo ya dunia, na kunaweza kuwa ni katika mambo ya Akhera, lakini katika hali zote ni kuwa haifai kuuliwa na watu tu wa kawaida isipokuwa ni kiongozi au makamu wake, kwani anasema Imam An-Nawawy katika kitabu cha Al-Minhaj, 1/465 – 466 ikiwa ni sherehe ya [Al-Khatwiib As-Sherbiniy, Mughniy Al-Muhtaj, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Sala ya jamaa ni katika Sala za Faradhi tofauti na Sala ya Ijumaa ni sunna iliyokokotezwa, na ikasemwa ni Sala ya Faradhi inayojitosheleza, kwa upande wa wanaume ni lazima ambapo huonekana mandhari ya Uislamu ndani ya kijiji, ikiwa watu wote wamejizuia kuitekeleza basi watauwawa”. Amesema Khatibu katika sherehe yake: “Inalazimu ambapo huonekana mandhari” kwa maana mandhari na alama ya umoja kwa kuisimamisha kwake ndani ya kijiji kidogo na vijiji vikubwa na miji huonekana alama na mandhari na kudondoka kwa matakwa ya kundi hata kama ni dogo, ikiwa itatekelezwa ndani ya majumba pasi na kuonekana kwa alama au mandhari, basi haitaondoka ulazima “Ikiwa watajizuia wote” kuitekeleza kama tulivyotaja “Watauliwa” kwa maana kiongozi atawauwa au makamu wake pasi na watu wengine”.
Ama likiwa kundi la watu waliozuia kufuata amri za Sheria Takatifu ni kundi la wasimamizi wa Dola na kuzuia na jeshi pamoja na ngome, katika haya kuna maelezo ya kina: Kwani huenda wakafanya au kuacha yanayolazimu kuchukua sifa ya kuritadi na ukafiri wa wazi, wakati huo ni lazima kwa kila Mwislamu mwenye uwezo kutoka na kulipiga kundi hilo, kinyume na hivyo, basi wanalazimika kuacha kazi za kuendesha Dola madamu tu hawawezi kusimamisha mandhari na sura ya Dini ndani ya hiyo nchi, hayo ni kutokana na yale yaliyopokelewa na Imamu Bukhari na Muslim katika vitabu vyao kutoka kwa Ibada Ibn Swamit R.A. amesema: Alituita Mtume S.A.W. na tukamuunga mkono kisha akasema katika yale tuliyoyachukuwa: “Ni muunge mkono kwa kusikia na kutii katika mambo yetu na machukizo yetu, mazito yetu mepesi yetu na yanayo athiri kwetu na wala tusiondoe watu na mambo yao, isipokuwa pale munapoona ukafiri wa wazi hali ya kuwa muna dalili itokayo kwa Mwenyezi Mungu”.
Anasema Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Fat-h Al-Bari, 13/123, Ch. ya Dar Al-Maarifah]: “Anaondoshwa Kiongozi - kwa ukafiri, kwa kauli za wanachuoni, ni lazima kwa kila Mwislamu kutekeleza hilo, kwa mwenye nguvu ya hilo anayo malipo, na mwenye kudharau kwa kufanya udangnyifu, basi anapata dhambi, na mwenye kushindwa ni lazima ahame eneo hilo”.
Ama ikiwa kuzuia kwa kundi la viongozi kufuata amri na kuacha makatazo ya Kisheria inalazimisha kuelezewa kwa sifa ya ufasiki pasi na ukafiri, ikiwa itawezekana kuondoshwa utawala wao kwa njia salama pasi na kumwaga damu ni bora zaidi, kinyume na hivyo, basi kipimo kinakuwa ni kujiepusha na uharibifu mkubwa zaidi kwa kutekeleza ulio mdogo.
Imekuja katika kitabu cha: [Al-Mawaqif na sherehe yake ya Sharif Al-Jerjaniy, 3/595 Ch. ya Dar Al-Jeel – Beirut]: “Wananchi wanaweza kumvua uongozi kiongozi na kumuondoa kabisa kwa sababu zinazowajibisha kufanya hivyo” mfano wa kuwepo kwa yale yanayopelekea mpasuko wa hali za Waislamu na kuharibika kwa mambo ya Dini kama ilivyokuwa kwao kumweka madarakani na kumdumisha kusimamia mifumo ya Dini na kuinua, ikiwa kumvua uongozi kiongozi kutapelekea fitina basi yatachukuliwa madhara madogo kati ya madhara mawili”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Ni kuwa kundi lenye kujitenga na amri za utawala linakusudiwa: Ni mtu mmoja au kundi la wananchi ndani ya Dola ya Kiislamu limejitenga na kuwa peke yake kwa uwazi jambo ambalo linapelekea kwenda kinyume na mfumo wa nchi na kupelekea matumizi ya silaha kinyume na sheria na athari za utumiaji wake, kulipiga vita kundi hilo ni jambo la halali ikiwa itabainika kwamba kuwapo kwake ni njia ya kuleta fitina, na inazingatiwa ni kutekeleza madhara madogo kati ya madhara mawili, na amri ya kuuawa au kushambuliwa inatolewa na kiongozi na wala sio mtu au kundi katika makundi ya kijamii, ni kiongozi anapaswa kuchukua hatua kwa hatua ya kwa kuanza na kuwatisha, na wala asianze kuwashambulia moja kwa moja isipokuwa baada ya kuwapa onyo na hoja, wala haikusudiwi katika kuwapiga vita kwa maana ya kuwamaliza kabisa, bali inakusudiwa kuwakemea na kuwatisha ili waelekee kwenye njia sahihi.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

Share this:

Related Fatwas