Kuandika Jina la Ibrahim Bila ya H...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuandika Jina la Ibrahim Bila ya Herufi ya Yaa

Question

 Ni vipi limeandikwa jina la Ibrahim bila ya herufi ya yaa?

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Kuandika jina la Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahim A.S. bila ya herufi ya yaa kumekuja katika sehemu moja tu ndani ya Qur`ani yote kama ilivyoelezwa, na sababu ya hilo ni kuwa ndivyo ilivyoandikwa mbele ya Mtume S.A.W. nayo ndiyo imefahamika baada ya hapo katika elimu ya uandishi wa Qur`ani kuwa “Maandishi ndani ya Qur`ani Tukufu ni Sunna ya kufuatwa” kwa maana ya kuwa Umma wa Kiislamu haifai kwao kujitenga na uandishi wa Msahabu ambao uliandikwa mbele ya Mtume S.A.W. kwa hivyo Wanachuoni wakasema “Hakika Qur`ani Tukufu ni muujiza katika uandishi wake kama vile yenyewe ni muujiza katika matamshi yake”.
Limepokelewa jina la Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahim A.S. kwenye lahaja sita, miongoni mwake ni pamoja na jina Ibraham kwa Ha na Ibrahim kwa Hi maana ya kuwa jina la Nabii huyu linatamkwa katika lugha ya Kiarabu kwa lahaja mbalimbali pamoja na kuzingatia tofauti kati ya lugha na lahaja, na imepokelewa katika shairi la Kiarabu kile kinachoitwa jina la Nabii huyu kwa lugha hii iliyotajwa “Abraham”.
Pindi ilipopokelewa katika Misahafu na kuandikwa mbele ya Mtume S.A.W. pia ilikuwa ni lugha sahihi na upokezi wake ni sahihi kwa Mtume S.A.W. uliokuja na usomaji sahihi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas