Kusoma Yasin kwa nia ya kukidhi haj...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Yasin kwa nia ya kukidhi haja

Question

Ni ipi hukumu ya kusoma Yasin kwa nia ya kukidhi haja na mambo kuwa mepesi?

Answer

Kusoma Qur`ani Tukufu ni miongoni mwa mambo ambayo humletea msomaji wake Baraka na thawabu na ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na miongoni mwa sura ambazo zimepokewa Hadithi nyingi katika fadhila za kusoma kwake ni Yasin; Hadithi iliyopokelewa na Muukal bin Yasar R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: “na Yasin ni moyo wa Qur`ani, haisomi mtu yeyote anamkusudia Mwenyezi Mungu na Akhera isipokuwa husamehewa dhambi zake, na wasomeeni maiti wenu” imepokelewa na Ahmad.

Kusoma Yasin kuna fadhila kubwa, na atakayeisoma ana malipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wanazuoni wengi wamethibitisha kujuzu kusoma Yasin kwa nia ya kukidhi haja na kuondoa matatizo- kama kukunjuliwa riziki, kulipa deni na kufanya mambo yawe mepesi na mengineyo miongoni mwa mambo ya kheri- na kwamba Mwenyezi mwenye kuisoma akiwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atakidhi haja yake kwa Baraka ya kusoma Yasin atapata hitajio lake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Share this:

Related Fatwas