Kusoma Qur`ani bila ya kutawadha
Question
Je, inajuzu kusoma Qur`ani bila ya kutawadha?
Answer
Jibu: Hakuna pingamizi la kisharia kusoma Qur`ani bila ya kutawadha, na inapendekezwa kutoigusa karatasi ya Qur`ani bila ya kutawadha. Kwa mujibu wa Aya hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: “Hapana akigusaye ila waliotakaswa” [Al-Waqi’ah: 79], kinyume na Qur’ani ya kielektroniki; Hakuna ubaya kuigusa bila ya kutawadha. Kwa sababu masharti ya Qur`ani hayaihusu kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.