Mkinzano wa Hadithi na Qur'ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Mkinzano wa Hadithi na Qur'ani

Question

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Na shukrani ni za Mwenyezi Mungu. Swala na salamu zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W
Waheshimiwa tume ya Ofisi ya Mufti – Al-Azhar Al-Sharif:
Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh

Answer

 Imenifikia barua kutoka kwa mmoja wa Wakristo anayedai kuwa kuna Hadithi nyingi zinazokinzana na Qur'ani Tukufu, pindi nilipomtaka kuleta dalili juu ya hilo akanitumia ujumbe ulio na maswala anayodai kuwa Mtume S.A.W alikwenda kinyume na Maandiko ya Kitabu na kwenda kinyume na Mwenendo wake Mtakatifu, lifuatalo ni andiko la ujumbe wake baada ya kufuta utangulizi na maeneo mengine ya pembeni ambapo anasema:
Kuna kanuni katika Uislamu miongoni mwao ni:
Kanuni ya Kwanza: Amesema Mungu wa Uislamu ndani ya Qur'ani:
{Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda? * Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda} [AS-SWAFF: 2, 3].
Kanuni ya Pili: Amesema pia:
{Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za wanayo yafanya} [AN-NUUR: 30]
Kanuni ya Tatu: Amesema Mtume wa Uislamu, kutoka kwa Abi Said Al-Khudry kuwa Mtume S.A.W amesema:
“Jihadharini na kukaa njiani, wakauliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu lazima sie tukae njiani kwa sababu ndio makazi yetu huwa tunazumgumza, akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa mutakataa basi barabara ipeni haki yake, wakauliza ni ipi haki ya barabara ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akasema Mtume S.A.W ni kuinamisha macho, kuzuia kero, kujibu salamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya”. [(Sahihi- Hiyo Sahiha- 2421 Hejabu ya Mwanamke 34), Hadithi namba ya 4030, katika Sunann Abi Dawud, sehemu ya tatu, Uk.940, Mlango wa Adabu na Kupiga Hodi, Swelah, na ilisahihishwa na Al Albaniy.]
Kutoka kanuni ya kwanza anasema Mungu wa Uislamu kuwa katika machukizo makubwa ni kuongea usiyoyafanya….na katika kanuni ya pili amewaamrisha Waumini kuinamisha macho yao wala wasiangalie mbinguni, na kama hivyo ameamrisha Mtume wa Uislamu pia katika kanuni ya tatu…basi ni ipi adhabu ya mwenye kuangalia wanawake kwa matamanio mpaka akafikia kwenye kilele cha matamanio “Naomba radhi kwa kueleza hivyo” na kutokuwa na uwezo wa kudhibiti matamanio yake?
Haya ndio yaliyotokea kwa Mtume wa Uislamu….hakufanya yale aliyoyasema, wala hakutekeleza amri za Mwenyezi Mungu, soma aliyoyasema yeye mwenyewe:
“Alipita karibu yangu mwanamke mmoja, moyo wangu uliingia kwenye kumtamani, mwisho nikaenda kwa mmoja wa wake zangu na kukutana naye, basi fanyeni hivyo, kwani kufanya hivyo ni katika mifano ya matendo yenu ya kuendea halali”.
Kutoka kwa Abi Kabasha Al-Anmaary amesema: Mtume siku moja alikuwa amekaa na Maswahaba zake kisha akatoka na akaoga, tukamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je kulikuwa na chochote? Akasema ndio, alipita mwanamke fulani…….mpaka mwisho, na Hadithi ina ushahidi kupitia Hadithi ya Abi Zarr kutoka kwa Jabir: Mtume alimuona mwanamke akampenda, akaja Zainabu na kumaliza haja yake, na akasema: Mwanamke hukutana naye kwa sura ya shetani na huzingatia katika sura ya shetani, pindi mmoja wenu anapomuona mwanamke na akavutiwa naye basi na arudi kwa mkewe, kwa kufanya hivyo mwanamme hurejesha yaliyo kwenye nafsi yake” imepokelewa na Imamu Muslimu na Abu Daud pamoja na Ibn Habban katika sahihi yake pia Baihaqy na Ahmad na Twabrany katika kitabu cha Al-Kabeer kwa njia ya Abu Zubeir, na ina shahidi mwingine kutoka kwa Abdillah Ibn Mas’ud amesema: Mtume S.A.W siku moja alimuona mwanamke na akampenda, kisha akaja Sauda akiwa amejipamba vizuri akamaliza haja yake, kisha akasema: Mwanamme yeyote aliyemuona mwanamke akapendezewa naye basi na asimame na aende kwa mke wake, kwani mkewe anacho mfano wake, imepokelewa na Daramy na Sary Ibn Yahya katika Hadithi ya Thaury kutoka kwa Abi Isaqa kutoka kwa Ibn Mas’ud.
Hadithi nambari 235. Marejeo: Mfululizo sahihi 1 ukurasa wa 470 maudhui kuu: Kuoa, watoto, talaka, kunyonyesha, aina ya Hadithi ni sahihi.
Na Hadithi hiyo hiyo katika upokezi Ahmad Hadithi nambari 17337.
Vile vile katika kisa cha Zainab Binti Jahshi aliingia nyumbani kwa mtoto wake Zaidi, kuna siku alimuona mwanamke akiwa uchi, badala ya kuinamisha macho chini akawa anamuangalia kwa mazingatio mpaka mwishowe akaingiwa na matamanio moyoni mwake, na akasema Ametakasika Mgeuza nyoyo…mpaka mwisho wa kisa.
Matukio haya hayakuwa mara moja wala mara mbili, lakini yametajwa kwa uchache tu mara nne, je waonaje nani tumuamini na ni Sunna gani tufuate, je tufuate amri za Qur'ani za kuinamisha macho chini au tufuate Sunna za Mtume kuangalia wanawake mpaka kujenga hisia, kisha tunarudi kwa wake zetu wakati wa hisia hizo? Tafadhali chukuwa Hadithi na zifikishe ofisi yeyote ya Mufti….kisha tuletee majibu uliyoyafikia.
Je niliyoyasema yanamaanisha kumfanyia uhalifu Muhammad? Na je nimemzushia au nimemfanyia dhuluma kuwa hajasema au hajafanya? Je vitendo hivi vinaendana na Nabii atokaye kwa Mwenyezi Mungu? Mwiso wa swali la Mkristo.
Waheshimiwa Mamufti, ni matumaini yangu kupata maelezo kuhusu maswala haya….niwatakie kila la kheir.
Wassalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuhu.
Muwasilishaji kwenu ni: Eng. Ashrafu Abdulfattah Al-Abajjiy.
Mkurugenzi wa utaalam katika moja ya kampuni ya kiuwekezaji. Ndani ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Jibu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swali hili ulilotumiwa na mmoja kati ya Wakristo limekusanya makosa mengi, na ilipaswa kwako kufahamu hilo na kumkabili nayo na kutojisalimisha kwa maneno yake yaliyokosa ufahamu na uelewa sahihi.
Hadithi ambazo amezielezea hazikwenda kinyume na Aya za Qur'ani kama alivyofahamu yeye, kwa sababu Mtume S.A.W hakuwaangalia hawa wanawake kwa matamanio kama alivyotaka kukuchezea akili huyu ndugu Mkristo, lakini kilichotokea ni kuwa jicho la Mtume S.A.W liliangukia kumuangalia mwanamke bila ya kukusudia kumuangalia, kisha akageuza macho kwa kutomuangalia, lakini kuangalia huku kwa kwanza ambako hakuzingatiwi na Mwenyezi Mungu kulizalisha kwenye nafsi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W kwa msukumo na maumbile ya kibinadamu matamanio, na hili ni jambo la kimaumbile “Wala hakuna amri katika mambo yanayotokea kimaumbile” ikiwa mwanamme atatokea kumpenda mwanamke ni jambo linalokuja kimaumbile kwa maana ya asili ambayo ameumbia nao mwanadamu, hivyo basi Mwenyezi Mungu hazingatii hilo, akatufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu kuyaweka matamanio yetu katika sehemu yake na mwanamme anatakiwa aelekee kwa mke wake ili kukidhi haja yake.
Na kwa vile Mtume S.A.W ni mwenye nafsi iliyosawa kitabia na kimaadili hakumuangalia huyo mwanamke kwa mara nyingine na wala hajafanya kitu kilicho haramishwa na Mwenyezi Mungu, ni vipi hali yeye akiwa ndio kiumbe bora zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu, na yeye ni katika waliokingwa na Mwenyezi Mungu kufanya makosa madogo madogo miongoni mwa dhambi pamoja na makosa makubwa kama haya anayomnasibishia huyu mtu ambaye asiyefahamu chochote katika hukumu za Uislamu, na wala hajasoma sifa za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W wala hafahamu kuwa kuzuiliwa kufanya dhambi ni jambo la lazima kwake S.A.W kama vile ni jambo la lazima pia kwa Mitume wote, na kama Muislamu hatoamini hili basi hukumu zote za dini zitabatilika, hivi inawezekana kwa Mtume kuibadili dini na kupingana nayo kwa kauli yake na vitendo vyake!! Na pindi likitokea hilo basi haifai kuamini hukumu zote za dini.
Uislamu umeamrisha kuinamisha macho chini, na maana ya kuinamisha macho ni mwanamme kuto angalia mwanamke si halali yake, na kuangalia hapa maana yake kuhusisha macho yake kwa mwanamke na kurefusha kumuangalia ambapo hufitinika kwa kuangalia huko na kuibua hisia haramu ndani ya nafsi yake, lakini pindi macho yake yanapotokea kumuona mwanamke pasi ya kukusudia hilo halihesabiwi bali huhesabiwa katika hali ya kuendelea kuangalia.
Sisi tuna amini kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W ni mwanadamu, lakini ni mwenye kuzuiliwa kufanya dhambi, kwani Mtume si Mungu, naye Mtume S.A.W kutokana na ubinadamu wake anapenda wanawake, lakini kuzuiliwa kwake na Mwenyezi Mungu hawezi kuingia kwenye haramu, baadhi ya sheria zingine zina amini kuwa Manabii si wenye kuzuiliwa kufanya dhambi hivyo si vigumu kwa mmoja wao kujenga fikra kuwa baadhi ya Mitume wa Mungu kama ilivyokuja katika baadhi ya vitabu kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Luut alizini na binti yake, na kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Daud alitoa amri ya kuuliwa Aury “Ni Muhabeshi” ili apate kumuoa mke wake ambaye alimpenda pale alipomuona akiwa anaoga hali ya kuwa yupo uchi, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa matukio baadhi ya watu wanayanasibisha kwa Manabii Wakubwa ambao ni waja wa Mungu wa kheri na ambao Mwenyezi Mungu amewakinga na kufanya makosa na dhambi, ni jambo la kusikitisha sana.
Miongoni mwa makosa ambayo ilipaswa kuzinduka nayo vile vile Hadithi hizi nyingi ni dhaifu, bali Hadithi ambayo ameitaja kuhusu Bibi Zainabu Binti Jahshi haina ukweli wowote kuongezea pia kuwa imerudia mara nyingi kama alivyodai muulizaji mwenye ujumbe, wafasiri wengi wamemjibu miongoni mwao ni Mwanachuoni Imamu As-Shanqitwy katika kitabu cha Adhwau Al-Bayan, na mwingine ni Prof/ Sayyid Twantwawy Sheikh Mkuu wa Al-Azhar kupitia kwenye tafasiri yake na wengine wengi.
Na wewe Mheshimiwa Eng: Ashrafu Abdulfattah Al-Abajjy, unapaswa kusoma kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W na kujifunza hukumu za dini zaidi hivyo ili uwongo kama huu dhidi ya Mtume S.A.W usikuingie wala kuchafua dini ya Kiislamu. Shukrani kwa kuonesha umuhimu wako.

Share this:

Related Fatwas