Hadithi ya Kuguswa na Shetani.

Egypt's Dar Al-Ifta

Hadithi ya Kuguswa na Shetani.

Question

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh.
Kuna Hadithi yenye maana kuwa:
“Mtoto yeyote anayezaliwa anakuwa anaguswa na shetani pale anapoanza kulia isipokuwa Nabii Isa tu na Mama yake”. Je Nabii wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.A.W aliguswa na shetani kwa kuzingatia kuwa yeye hajatolewa ndani ya Hadithi? Ahsante Sana.
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ama kuhusu Hadithi hiyo basi ni sahihi, imepokelewa na Al Bukhariy na Muslim.
Na Maana ya Hadithi iliyotajwa ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliitikia maombi ya Bibi wa Nabii Isa pale aliposema akimuombea Bibi Maryamu Binti yake:
{Na mimi nimemuita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shetani aliye laaniwa} [AALI IMRAAN: 36].
Hii haina maana kuwa maombi haya ni maalumu ambapo Mtume S.A.W hausiki au hayumo – Kwa mfano tuchukulie hivyo – kuwa sheitani anamuongoza na kujiwezesha kwa Mtume “Mungu atupilie mbali hali hiyo” baadhi ya Wanachuoni wamepitisha kuwa Manabii wote wanashiriki kwenye hali hiyo ya kutokuguswa na shetani, angalia kitabu cha sherehe ya An-Nawawy 15/120.
Wala Hadithi haituelezei kuwa Nabii Isa ni bora zaidi ya Mtume Muhammad S.A.W ambapo kumekuwa na Hadithi nyingi zinazoelezea ubora wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.A.W na kuwepo ubora pia kwa Nabii Isa Amani ya Mungu iwe kwake.
Imethibiti kupitia kauli ya Mtume S.A.W hauwezi kuondolewa kwa ujumla wake ubora uliothibiti kwa Mtume S.A.W.

 

 

Share this:

Related Fatwas