Matini za mwisho wa Dunia

Egypt's Dar Al-Ifta

Matini za mwisho wa Dunia

Question

Kwa namna gani makundi ya kigaidi yalieleza na kuelewa Hadithi za fitina na vita vya mwisho wa dunia na kuzitegemea kisingizio cha kuwatawala watu?

Answer

Hadithi za fitina na vita vya mwisho wa dunia aghalabu hazina hukumu, kinyume na Hadithi zenye kupitisha hukumu, sababu ya msingi ya hali hii ni pamoja na kufanana na ujumla ambao ni sifa kuu ya Hadithi za kuzungumzia fitina kwa jumla, ambapo Hadithi nyingi za aina hii zina matini zinayofanana na Hadithi nyingine au matini ya kijumla ambayo huwa hivyo hivyo bila ya kutaja maelezo kwa urefu, hali ambayo inapambanua Hadithi za aina hii na Hadithi nyinginezo. Pia, Hadithi za kuzungumzia fitina na vita zina sifa maalumu, lakini sifa zile zote zinahitaji kufafanuliwa; kwa hiyo zimejitokeza changamoto nyingi kuzielewa na kuzifasiri Hadithi hizo, ambapo kuainisha zama na muda maalumu wa kutokea fitina hizo ni jambo muhali kwani ni ghaibu ambayo hakuna yeyote anayejua isipokuwa Mwenyezi Mungu…vile vile, kufanana kupatikana pia katika baadhi ya watu ambao majina yao yanafungamana na fitina za mwisho wa dunia ..hivyo ishara huwa kwao kwa ujumla.

Kufungamanisha baadhi ya matini zinazohusiana na fitina na hali za siku za mwisho wa dunia na watu maalumu kumekithiri sana kama ilivyo katika masimulizi ya habari za Mahdy na Sofiany, ambapo amejitokeza anayedai kuwa: huyu ni Mahdy na yule ni Sofiany pasipo na dalili, jambo lililowashawishi watu kwa mambo yasiyo na msingi katika dini.

Share this:

Related Fatwas