Ukhnuukhna Wala Sio Idris

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukhnuukhna Wala Sio Idris

Question

Aya yenye kuleta shaka: Imekuja ndani ya Quran:
{Na mtaje katika Kitabu Idris . Hakika yeye alikuwa ni mkweli Nabii * Na tulimuinua daraja ya juu} [MARYAM: 56, 57].
Qur`ani imetaja jina la Nabii huyu kuwa ni Idris, ndani ya Taurat jina la huyo Nabii ni Ukhnuukh, hivyo Qur`ani imekuja na jina Idris kutoka wapi?
 

Answer

Shaka hii imetokana na ukosefu wa ufahamu sahihi wa matumizi ya Qur`ani Tukufu lugha ya Kiarabu na muundo wake wa kunukuu maneno na majina maarufu kutoka lugha yake ya asili. Qur`ani Tukufu pindi inaponukuu jina maarufu kutoka lugha asili kwenda lugha ya Kiarabu kunukuu kwake hakuachani na hali tatu:
Hali ya Kwanza: Jina maarufu katika lugha ya kwanza liwe kwenye wizani uliosawa na wizani wa lugha ya Kiarabu, katika hali hii hunukuliwa kama lilivyo, mfano jina kama Isa na Musa.
Hali ya Pili: Jina maarufu katika lugha ya kwanza liwe kwenye wizani unaokaribiana na wizani wa lugha ya Kiarabu, hufanyiwa baadhi ya mabadiliko yanayokubaliana na lugha ya Kiarabu, mfano kama Yohana na Yunan, ndani ya Qur`ani utakuta jina la kwanza ni Yahya na jina la pili ni Yunus.
Hali ya Tatu: Jina maarufu katika lugha ya asili lisiwe sawa wala kukaribiana na wizani wa Kiarabu, katika hali hii Qur`ani haileti hilo jina kutoka kwenye lugha yake kama lilivyo, bali hufasiri maana yake katika lugha ya Kiarabu, na hii imetokea katika jina la Idris amani ya Mungu iwe kwake, neno “Ukhnuukh” maana yake katika lugha yake ya kwanza ni “Mwanafunzi” hivyo Qur`ani Tukufu ikalinukuu kwa jina la Idris likiwa na maana pia ya mwanafunzi.
Hali hii si katika lugha ya Kiarabu tu peke yake bali ipo kwenye lugha zingine pia, nayo ni kuwekwa majina maarufu kwa mujibu wa kanuni zake, hivyo yamekuja majina mengi ya Mtume huyu Mtukufu katika lugha zingine, miongoni mwa lugha hizo ni kama vile Wagiriki walimwita (Harmas) na imenukuliwa kutoka kwa Ibn Al-Ibrii katika historia yake kuwa “Idris lilikuwa jina linaloitwa na Wagiriki wa zamani “Trismegist” na maana yake kwa lugha yao ni mafunzo ya pande tatu, kwa sababu walikuwa wanamuelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa tatu nazo ni Uwepo Hekima na Uhai” [Kitabu cha historia ya Ibn Ibrii 1/7]
Na Ibn Ashuur amesema akielezea yaliyotajwa: “Hakuna kinachojificha ukaribu wa herufi za mwanzo katika jina hili la Idris huenda Waarabu wamefupisha jina kwa urefu wake na wakalifupisha mwanzoni na kufanya mabadiliko” [Kitabu cha Tanwiir 16/ 130 na kuendelea].
Kisha kuna miongoni mwa watafasiri waliosema kuwa neno “Idris” ni la Kiarabu, na kukusudiwa kufasiriwa jina hili kwa Kiarabu, na wapo waliosema: Ni jina maarufu kwenye lugha ya Kigeni na imekusudiwa maana yake ambayo imetafasiriwa nayo, ikasemwa: Ni Syriac, na ikasemwa pia ni lugha ya Kiibrania, na ikasemwa neno Idris lugha yake asili ni lugha ya Kiarabu Kibrania na Kisyriac, na kwa mitazamo hiyo halielezewi jina hili kuwa si la Kiarabu kama vile halielezewi kuwa si Kiibrania bali ni la lugha mbili kwa pamoja.
Kauli yenye nguvu ni kuwa neno “Idris” si la Kiarabu lakini halikubali mabadiliko, nalo ni sawa na majina mengine ya Kigeni.
Kwa ufupi: Kwa Mtume huyu kuna majina mengi kila watu humuita na kufahamika kwa jina hilo, nalo ni kama kwenye lugha zingine katika kubadili baadhi ya maneno na majina.

9- Kutumwa Mtume Kwa Watu Wote.
Swali: Je Mitume walipelekwa kwa wana wa Israeli tu au Mwenyezi Mungu alipeleka Mtume kwa kila Umma?
Aya yenye kuleta shaka:
Imekuja ndani ya Qu`rani Tukufu:
{Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa} [YUNUS: 47].
Na Qur`ani ikasema:
{Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha} [AN-NAHL: 36].
Na Qur`ani ikasema tena:
{Na siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayotokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu} [AN-NAHL: 89].
Qur`ani inasema kuwa Mwenyezi Mungu alipeleka kwa kila watu au Umma Nabii, na Kitabu Kitakatifu kinasema: Manabii na Mitume wao ni wana wa Israeli na wamepelekwa kwao na ulimwenguni kote, ikiwa maneno ya Qur`ani yatakuwa yana ukweli basi ni kwa nini kwa watu wa Afrika Ulaya Marekani Australia na Asia hawakutoka Manabii watokanao na wao na hata kupelekwa kwao? Na ikiwa kwa Umma kuna Mitume wanaotokana na wao na kupelekwa pia kwao basi ingefaa kwa Waarabu kuwa na Mtume anayetokana na wao.
Jibu:
Mwenyezi Mungu amehukumu kutuma kwa kila Umma Mtume ili iwe hoja kwao siku ya Kiyama, na Umma ndani ya Qur`ani inakuja kwa maana mbalimbali – kama ilivyoelezwa na Wanachuoni wa tafasiri – na kusudio la Umma katika Aya hizi: Ni kundi kubwa la watu wanaokutanishwa na jambo la dini au muda au sehemu moja, ni sawa sawa mkusanyiko huo ukawa ni wa hiyari au kwa nguvu, wala haielezewi kuwa na idadi maalumu au ndani ya miaka maalumu kama vile watu wa Nabii Aad ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpeleka kwao Mtume wake Huud, na watu wa Thamuud ambao Mwenyezi Mungu aliwapelekea Mtume wake Saleh, na watu wa Madian ambao Mwenyezi Mungu alimpeleka kwao Mtume wake Shuaibu, na kwa Wayahudi ambao Mwenyezi Mungu alimpeleka kwao Nabii Musa Amani ya Mungu iwe kwake.
Ama kauli yao kuwa Kitabu Kitakatifu kinasema: Manabii na Mitume ni wana wa Israeli tu kutoka kwao ndio wakapelekwa ulimwenguni kote, maneno haya si sahihi na yanapingwa na uhalisia pia yanapingwa na Kitabu Kitakatifu, kwa sababu lau ingekuwa Manabii wanatokana na wana wa Israeli tu wamepelekwa kwao na kwa ulimwengu wote basi wapo wapi Manabii na Mitume wa ulimwengu kabla ya kuwepo kabisa kwa wana wa Israeli, na ni vipi inasemwa kuwa wao ni wa ulimwengu wote na Nabii Isa Amani ya Mungu iwe kwake anasema kama ilivyokuaja kwenye Injili: “Sikutumwa isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” Mathayo 15: 24 na wala hakusema kuwa kutumwa kwake kulikuwa ni kwa ulimwengu wote?
Ama hoja kuwa kwa Waafrika watu wa Ulaya Marekani Australia na Asia hakutoka Nabii anayetokana na wao wala Nabii aliyepelekwa kwao, tunasema: Hizi ni nchi na wala sio umma, pamoja na hilo nchi hizi ni zenye kutakiwa kuamini Mtume aliyepelekwa na Mwenyezi Mungu kwao na Mwenyezi Mungu akamfanya kuwa ndio hitimisho la Mitume mpaka siku ya Kiyaa, naye si mwingine bali na Mtume wetu Muhammad S.A.W
Jambo la kushangaza ni muulizaji kutoa ushahidi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao} [AN-NAHL: 89].
Kuwa kusudio la Aya ni umma duniani, na usahihi ni kuwa Aya inazungumzia mambo ya Akhera nayo ni ushahidi wa kila Nabii kwa umma wake, na wala haina uhusiano wa kupelekwa Mitume kwa watu, vile vile kuhusu ushahidi wa Mtume S.A.W kwa umma wake na kwa umma zingine.

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas