Hadithi: “Umma wangu utagawanyika”

Egypt's Dar Al-Ifta

Hadithi: “Umma wangu utagawanyika”

Question

Je, Hadithi ya “Umma wangu utagawanyika” inaashiria kwamba makundi yote – mbali na yaliyonusurika– ambayo yameelezwa  kuwa yako Motoni, je, hiyo ina maana kwamba makundi hayo ni makafiri?

Answer

Hadithi hii imepokelewa kwa mapokezi mengi  ambayo kila mapokezi yanatia nguvu mapokezi mengine, na hivyo kundi la Maimamu lilitangaza usahihi wake, na baadhi yao wakayahusisha mapokezi hayo na kiwango cha Tawatur (yenye wapokeaji wengi).

Baadhi ya wale ambao wana muelekeo wa kukufurisha walichukua maana ya dhahiri ya Hadithi hiyo, na wakamtangaza kila aliyetofautiana na baadhi ya mambo ya imani kuwa ni kafiri, bali baadhi yao wakafikia hata kwa wale waliotofautiana katika matawi kuwa ni makafiri! Ukweli juu ya hili ni kwamba kanuni ya kimsingi ya makundi haya ni kuwa wao ni watu wa umma wa kuitikia, na kwamba kupinga kwao hakulazimu ukafiri wao, bali kunawaweka kwenye adhabu kama dhambi nyingine zote, kama inavyojulikana, na maana ya kauli yake: “Wote wakiwa motoni” maana yake ni: wanaingia humo, kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake na vitendo vyake, kwa sababu wanafichuliwa na kile kinachowaweka motoni, na kwa sababu hiyo baadhi ya wanachuoni wa Sharia wameona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hatomwadhibu yeyote.

Kauli yake: “Umma wangu utagawanyika makundi sabini na tatu, wote wakiwa motoni,” inaonesha kuwa madhehebu haya yote hayako nje ya dini. Kama Mtume (S.A.W.), aliwafanya wote kuwa sehemu ya umma wake. Inaashiria kuwa mfasiri haotoki katika dini hata kama amekosea katika tafsiri yake. Na kauli yake: “Isipokuwa dini moja” maana yake ni: Hao ndio walioongoka wanaoshikamana na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa walioongoka baada yangu, nao ni wenye elimu na fiqhi waliokusanyika kufuata athari zake zote na hawakuzua kwa upotoshaji na mabadiliko, na kinachomaanishwa mgawanyiko wa umma ni mgawanyiko wao katika misingi na imani, sio katika matawi na utendaji.

Share this:

Related Fatwas