Kuandika Kaburini

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuandika Kaburini

Question

Nini hukumu ya kuandika jina la maiti kaburini ili lisichanganyike na kaburi lingine, na je ndugu zake wanaweza kumzuru?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Asili katika hukumu ya kuandika ni kwa mujibu wa yale yanayoandikwa; basi pengine inaweza kuwa ni vyema au vibaya. Na haitajwi katika maana ya swali hilo ila hadithi moja inayozuia kuandika kaburini, nayo ni ile iliyotolewa na Tirmidhiy kutoka kwa Muhamad Bin Rabia, kutoka kwa Ibn Juraij, kutoka kwa Abi Al Zubair, kutoka kwa Jaaber amesema: "Mtume S.A.W. alizuia kuyapiga lipu makaburi, kuandika juu yake, kujenga juu yake, au kuyakanyaga". Tirmidhiy amesema: hiyo ni hadithi nzuri na sahihi, na imepokelewa kwa njia mbalimbali kutoka kwa Jaaber. Na baadhi ya wanachuoni miongoni mwao Al Hassan Al Bassriy wamerahisisha hukumu ya kuyapiga plasta makaburi kwa kutumia udongo. Na Al Shafiy amesema: "si vibaya kuyapiga plasta makaburi".

Na Al Haakim ameitoa Hadithi kutoka kwa Hafssu Ibn Ghaiyaath Al Nukhaiy, na Ibn Juraij, kutoka kwa Abi Al Zubair, kutoka kwa Jaaber, amesema: "Mtume S.A.W. alizuia kujenga juu ya kaburi, kupiga lipu, au kulikalia juu yake, na akazuia kuandika juu yake".

Al Haakim amesema: hiyo ni hadithi sahihi kwa sharti ya Muslim, na imetolewa kwa isnadi yake bila ya neno "kuandika", basi hilo ni neno sahihi geni, na kadhalika imepokelewa na Abu Muawiah kutoka kwa Ibn Juraij kisha ikapokelewa kwa njia ya Abi Muawiah, kutoka kwa Ibn Juraij, kutoka kwa Abi Al Zubair, kutoka kwa Jaaber; amesema: "Mtume S.A.W. alizuia kuyapiga lipu makaburi, kuandika juu yake, kujenga juu yake na kukaa juu yake."

Kisha Al Haakim akasema: isnadi hizo ni sahihi, na si za kufanyiwa kazi, kwani maimamu wa waislamu kutoka Mashariki na Magharibi ya Dunia makaburi yao yameandikwa juu yake, na hili ni jambo ambalo wafuasi walilichukua na kulifanya hivyo kutoka kwa waliowatangulia. Na Al Dhahabiy aliyafuatia hayo kwa kauli yake ifuatayo: nimesema: hatumjui hata sahaba mmoja aliyefanya hivyo, lakini hilo ni jambo walilolifanya wafuasi wa masahaba, kisha wale waliokuja baada yao. Na wala hawakuambiwa kuwa inazuiwa kufanya hivyo.

Na hadithi hiyo imetolewa na Muslim na haina masuala ya kuandika kaburini kwa hitilafu ya wasimulizi juu ya tamko hili, kwani baadhi yao walilitaja na wengine hawakulitaja. Na wala haisemwi: kwamba nyongeza inakubalika daima, kwa hivyo madhehebu ya wahakiki wa hadithi yanapaswa kuzitazama simulizi hizi na kuzilinganisha baina yake, pengine inaweza kuwa isnadi ni sahihi na yaliyomo ndani yake si ya kawaida kama inavyojulikana.

Na Al Darqattniy ametaja katika kitabu cha [Al Elal, 349/3, Ch. Dar Ttiba, Al Riyaadh], hitilafu ya wasimulizi juu ya Ibn Juraij katika hadithi hiyo, lakini hakutoa hukumu yoyote, na hakulinganisha baina ya yote yaliyomo.

Na kwa hali yoyote, lau tungekubaliana na usahihi wa hadithi hiyo, basi hiyo inachukuliwa kama ni chukizo kama vile ilivyo katika madhehebu yote, na kwa hivyo basi, sababu nyingi za kuandika kabirini ni kwa ajili ya kuweka alama ili liweze kutembelewa, na makusudio haya ni halali, na dalili kuu ya uhalali wake ni uhimizaji wa kuyatembelea makaburi na hasa yale ya ndugu na jamaa. Na Mtume S.A.W alilitembelea kaburi la mama yake. Na kwa upande wa dalili maalumu na maelezo ya jambo hili, ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mutwalib, amesema: "alipokufa Uthman Bin Madhuon, walijitokeza watu kwenda kumzika, na akazikwa. Na Mtume S.A.W. akaamuru mtu mmoja alete jiwe, mtu huyo hakuweza kuliinua jiwe hilo, basi Mtume S.A.W. akatoa mikono yake miwili, Katheer anasema: Al Muttaleb akasema: anayeniambia hayo kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: mimi kama vile nauona weupe wa mikono miwili ya Mtume S.A.W. pale alipoitoa mikono yake hiyo kisha akaliinua jiwe hilo na kuliweka kwenye kichwa cha maiti, na akasema ninalitumia kama alama ya kaburi la ndugu yangu, na ninawazikia ndugu zangu watakaokufa(kwa njia hio)". Imetolewa na Abu Dawud.

Na hukumu hiyo inayaunga mkono aliyoyataja Al Haakim katika wingi wa kazi ya kuyaandika makaburi, na yeye anayaongelea mambo yaliyoonekana na ambayo hayahitaji ugunduzi wa kifiqhi, kwa ajili hiyo Al Dhahabiy hakupingana naye katika jambo hilo, bali alijaribu kulitupilia mbali kwa kutotajwa kwake na masahaba, na kwamba waliolifanya miongoni mwa wafuasi wa masahaba hawakuambiwa waliache, na hili la mwisho ni uwezekano tu. Kwani yawezekana mwanachuoni akawa amefikishiwa katazo lakini halikuthibitika kwake au yeye akalichukulia kuwa si haramu, ni kwamba akalitafsiri au akalipa sifa maalumu au hata akaona bora kulifutilia mbalini. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa jambo kama hilo.

Kisha hakika zama za masahaba zilikuwa zama zenye uandishi mchache mno; na kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapa sifa ya watu wasiojua kusoma wala kuandika. Kama ni hivyo basi, tunapata wapi maamuzi ya kwamba eti wao waliliacha kwa ajili ya katazo kwa namna lilivyo? Na je? Kila katazo linazingatiwa kuwa ni haramu?!

Al Suyuttiy amesema: "Al Eraaqiy alisema: pengine kusudio ni kuandika kwa jumla ni kuandika jina la marehemu juu ya kaburi lake au tarehe ya kifo chake, au kusudio la kuandika aya ya Quraani na majina mazuri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ili kuomba baraka kwa kuangalia uwezekano kuwa kaburi hilo linaweza kuchanganyika na mengine au likadidimia ardhini na kuwa chini ya miguu". [Hashiat Al Syuttiy Ala Al Nisaaiy, 87/4, Ch. Maktabat Al Mattbuaat Al Islamia - Halab].

Basi jambo muhimu hapa ni uwezekano kama unavyoona, swala la kuandika juu ya kaburi linatofautiana kutoka kaburi moja hadi jingine, kwa mfano makaburi sasa nchini Misri maandishi huandikwa juu ya marumaru na huwekwa juu ya mlango wa kaburi. Na kuzalishaji maana kutoka matini inajuzu kwa baadhi ya wanachuoni.

Al Isnaawiy alisema: yaliyo mashuhuri miongoni mwa kauli za wanachuoni wa Usuuli na kauli ya Shafiy pia ni kuwa inajuzu kuzalishwa maana maalumu kutoka katika matini”. [Al Tamheed 375, Ch. Muasasat Al Resalah]. Kisha kama sisi tukikubaliana na chukizo, basi hili linaweza kufutwa kutokana na haja ya kisheria.

Ibn Abdeen alisema: "(kauli yake si vibaya kuandika ... n.k.) kwani katazo na hata kama litakuwa sahihi basi wanavyuoni wote wamekubaliana hivyo juu yake. Al Haakim ameondosha katazo hilo kwa njia mbali mbali, kisha akasema: isnadi hizo ni sahihi lakini hazifuatwi kiutendaji, kwa hivyo basi, maimamu wa waislamu wa mashariki na magharibi ya dunia hii, makaburi yao yameandikwa juu yake, na utendaji huu wafuasi waliuchukua kutoka kwa waliowatangulia.

Na inaimarishwa kwa iliyotolewa na Abu Dawud kwa isnadi nzuri: "kwamba Mtume S.A.W. alichukua jiwe na akaliweka kwenye kaburi la Authman Bin Madhuun na akasema ninaliwekea alama kaburi la ndugu yangu na nitawazika kwayo hivi ndugu zangu watakaotubu", kwahivyo kuandika ni njia ya kuliwekea kaburi alama. Inabainika kuwa mahali pa makubaliano ya wanachuoni wote kiutendaji ni ruhusa katika jambo hili na hasa iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo kwa ujumla, kama alivyoiashiria katika kitabu cha [Al Muheett] kwa kauli yake: "Na kama itahitajika kuandika; ili athari ya kaburi isifutike na kaburi kupuuzwa basi si vibaya kuandikwa.

Lakini hairuhusiwi kuandika bila ya kuwa na haja. Hata ikawa kwamba inachukiza kuandika aya yoyote ya Quraani juu ya kaburi, au mashairi, au maneno ya kumsifu na yanayofanana na hayo kwa kifupi. Nilisema: lakini baadhi ya wahakiki, miongoni mwa wanachuoni wa Shafiy walimili katika makubaliano hayo wakisema kuwa ni ya wengi na kama itasalimika basi sehemu ya hoja yake ni pale panapohusu marekebisho ya nyakati mbali mbali kwa namna ambayo inatoa njia ya kuamrishana mema na kukatazana mabaya. Na jambo hili lilisita kwa muda mrefu sana, kwani wewe huoni kuwa ujenzi juu ya makaburi yao kama alama ni zaidi kuliko kuandika juu yake kama inavyoonekana, na walitambua kukatazwa kufanya hivyo lakini wakaendelea kuandika" Kwa hivyo ni bora kuwa na msimamo kwa yale yanayoleta faida ya kutumia katazo bila ya kuwa na haja, kama ilivyotangulia". [Hashiyat Ibn Abdeen 2/237-238, Ch. Dar Alkutub Al Elmiyah].

Al Hattaab alisema: "inajuzu kuweka jiwe juu ya kaburi, au kibao kisichokuwa na nakshi ili kulitofautisha na makaburi mengine. Na kauli ya Al Musanaf inasema kuwa hayo yanajuzu, na hayo yanaonekana wazi kuwa ni kauli ya watu kadhaa. Al Mazriy amesema: Ibn Al Qaasem alichukizwa kuwekwa marumaru juu ya kaburi kwa kuandikwa, na si vibaya katika jiwe, mti na kibao, ili mtu aweze kulitambua kaburi la jamaa yake, kwa sharti la kutoandika juu yake.

Na mwandishi wa Al Madkhal amesema kuwa inapendeza ... na katika kitabu cha [Mukhtasar Al wadheha]: Na si vibaya kuweka jiwe moja katika pembe moja ya kaburi kama alama, ili kulitambua kaburi hilo na kujua lilipo, na ili mtu ajue kaburi la jamaa yake. Na kwa upande wa jiwe kubwa, na miamba kama wanavyofanya baadhi ya wasiojua katazo hilo, basi hakuna heri katika jambo hilo... Na Ibn Al Qaasem ameona kuwa inachukiza kuweka marumaru juu ya kaburi na kuliandika, na hakuona vibaya kufanya hivyo katika jiwe, kipande cha mti na kibao, kwa sharti la kutoandika juu yake, ili mtu ajue kaburi la jamaa yake. Na Ibn Rushd amesema: Malik ameona kuwa inachukiza kujenga juu ya kaburi, na kuwekwa marumaru inayoandikwa juu yake, kwani hayo ni miongoni mwa uzushi ambao waliuanzisha matajiri ili kujifaharisha na kutaka kujulikana. Na hili ni miongoni mwa mambo yasiyo na hitilafu kwa kuwa kwake linachukiza.

Na Ibn Al Arabiy amesema katika kitabu cha [Al Aaridha]: "na ama kuandika juu ya makaburi, basi hilo ni jambo lililoenea sana duniani ingawa kuna katazo lake, lakini kwa kuwa haikuwa kwa njia sahihi, watu walisameheana ndani yake, na hakuna faida yoyote ya kufanya hayo isipokuwa kuliwekea kaburi alama ili lisifutike." [Mawaheb Al Jalil katika Sharh Mukhtasar Khalil, 2/247]

Ibn Hajar Al Haitamiy amesema katika kitabu cha [Al Fataawa Al Kubra, 2/12, Ch. Al Maktabah Al Islamiyah] "(na aliulizwa) R.A. kuhusu inavyochukiza kuandika juu ya makaburi, je inajumuisha na majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Quraani, na jina la maiti na mengineyo? au inahusu jambo moja miongoni mwa hayo ambalo wamelifafanua? (Basi akajiba) kwa kauli yake kuwa wenzake wamesema kuwa inachukiza kuandika juu ya kaburi kwa kuwepo katazo la kufanya hivyo. Hadithi hii imepokelewa na Tirmidhiy, na akasema Hadithi hii ni nzuri na sahihi. Na Abu Abdullahi Al Haakem Al Naisaburiy mtaalamu wa Elimu ya Hadithi aliipinga na akasema kuwa si ya kufanyiwa kazi. Basi maimamu wa waislamu kutoka mashariki na magharibi ya dunia hii makaburi yao yameandikwa juu yake, na hii ni kazi ambayo waliichukulia wafuasi kutoka kwa waliowatangulia Radhi za Allah ziwafikie wote, na kilichopingwa katika jambo hili mwelekeo wake ni kwamba ikiwa wanachuoni wote wa zama hizo walifanya hivyo au walijua lakini hawakulipinga jambo hili, na ukanushaji wowote ni mkubwa kuliko maneno ya wenzetu kuhusu kuchukiza kwa kuitumia Hadithi hii.

Na Al Subkiy na Al Adhraiy walitafuta namna ya kuyafungamanishi hayo -kwa kiasi cha nyongeza ya kile kinachotokea kwa kuweka alama juu kaburi la mtu- na tamko la Al Subkiy, na itakuja baadae hukumu ya kwamba "kuweka kitu maalum kwa lengo la kuwekea kaburi alama ni kitu kinachopendeza" na kama kuandika ni njia miongoni mwake basi inapaswa kutochukiza kama pataandikwa kwa kiasi ya haja ya kuweka alama tu. Na tamko la Al Adhraiy; "Na ama kuandika juu ya kaburi inachukiza iwe pameandikwa jina la marehemu juu ya ubao juu ya upande wa kichwani au kitu kingine, hivi ndivyo walivyoachia bila ya kuhusisha, na kipimo kilicho wazi ni kuharamisha kuiandika Quraani katika pande zake zote za kaburi kwa sababu ya uwezekano wa kudharaulika na kupuuzwa kwa kukanyagwa makaburi au kuwepo uchafu wa sehemu ya maiti pale palipochimbwa chimbwa makaburi. Ama kuandika mashairi au mashairi huru inajuzu pamoja na uwezekano wa kuchukiza na kuharamisha kwa ajili ya kukataza.

Na ama kuandika jina la maiti juu ya kaburi lake, wamesema wanachuoni: "kwamba kuwekwa kitu ili kaburi lijulikane ni jambo linalopendeza. Kwa hivyo basi, kama hiyo itakuwa ndio njia ya kulitambua kaburi, basi kupendeza kwake ni wazi kwa kiasi cha haja ya kuweka alama bila ya kuwepo uchukizo wa aina yeyote ile, na hasa kuyawekea alama makaburi ya watu wema wa Mwenyezi Mungu. Kwani makaburi hayo hayajulikani baada ya muda mrefu isipokuwa kwa kuandikwa huko. Kisha pakatajwa yaliyopitia kutoka kwa Al Haakim, na Uqbah kwa kusema: kama mtu anataka kuandika jina la maiti ili kaburi lijulikane, basi hilo liko wazi. Ama zuio na katazo la kuandika makaburini, litakuwa ni kuandikwa makaburi kwa lengo la kujisifu, kuweka mapambo, sifa za uwongo, au kuandika Quraani na mengineyo mengi."

Na aliyoyatafiti Al Subkiy ni kutochukiza kuandika jina la maiti juu ya kaburi lake ili kaburi hilo lijulikane. na Al Adhraiy anaona kuwa inapendeza kufanya hivyo kama ukiwepo ugumu wa kuyatambua makaburi, kwa kuandika jina kwenye kaburi la mtu mwema au mwanachuoni na kwa kuchelea kutoweka kwa makaburi yao baada ya kupita muda mrefu, au watu kutoyatambua makaburi hayo. Na kinyume na sababu hizo, kuna uwezekano wa kuzuiwa kuandika juu ya makaburi. Kwani inajuzu kutoholewa kutokana na Aya au Hadithi maana inayoainisha hivyo, na hapa kuna haja ya kuainisha, nako kwa kupima ni vizuri kuwekea kitu juu ya kaburi kama alama inayolijulisha kaburi hilo, na inaingia hukumu yake katika kuliendeleza kuwepo kwa jina la mwanachuoni au mtu mwema; ili kupata rehma za Mola na Baraka zake kwa kumwombea marehemu huyo watu wanaolizuru kaburi lake. Na yaliyosemwa na Al Adhraiy kuhusu kuharamisha uandikaji wa Quraani yako karibu, hata kama ukanyagaji wa Qurani au kuwepo uchafu makaburini hayatokei; kwani kama hayo hayajatokea hivi sasa basi yanaweza kutokea katika zama zijayo, kutokana na kawaida ya uchimbaji wa maeneo ya makaburini, na kuwepo uwezekano wa kutoweka kwa makaburi hayo. Na kila jina tukufu linafuatana na Quraani kihukumu, na siyo kuandika mashairi au mashairi huru, kwani hivyo vingine ni Makruhu na wala siyo haramu hata kama uharamu utasemwa mara kwa mara ndani ya jambo hili, na kauli yake: na inabeba katazo... n.k. nimejua kuwa wakati mwingine huwa inabeba maana ya kuchukiza kwa upande mmoja, na hubeba maana ya uharamu kwa upande wa pili. Na uharamu huo ni kwa kuandikwa Quraani au jina tukufu, na vinginevyo. Na hata kama uandishi huo makaburini ilikusudiwa mapambo na kujigamba.

Al Bahutiy amesema: "(na) inachukiza (kuandika kaburini) kwa sababu ya yaliyotangulia katika hadithi ya Jaabber." [Kashaaf Al Qinai 2/40, Ch. Dar Al Fikr].

Na kutokana na yaliyotangulia: kwamba zuio lililotajwa katika kuandika kaburini kama litathibitika basi linachukuliwa kuwa inachukiza kuandika makaburini, ili isiingie fahari na kujigamba. Lakini kama uandishi huo utakuwa ni kwa kusudio la kuliwekea kaburi alama, kwa ajili ya kulizuru n.k, basi wakati huo chukizo hilo hufutika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas