Hukumu ya Mwanamke Kumkataa mume ambaye Familia yake Imemchagulia.

Je, inajuzu kwangu kuolewa na mtu ninayempenda licha ya kutokubaliwa na familia yangu kwa sababu ana maradhi ya kisukari na wana shaka kuwa hataweza kupata watoto? Ikithibitika kuwa anaweza kupata watoto, je naweza kuipinga familia yangu na kuwakataa wale walionichaguliwa badala yake?

Soma zaidi....

Kutokuwepo kwa Mume

Mwanamke aliolewa na mwanamume Muislamu anayefanya kazi Uingereza, na akahamia kuishi naye katika nyumba ya ndoa huko Uingereza. Baada ya mwaka mmoja hivi, kutoelewana kulizuka kati yao, na maisha ya ndoa pamoja naye yakawa magumu sana, yasiyovumilika, na yasiyowezekana. Baada ya kujifungua mtoto wake na familia yake, alimtumia kiasi cha pesa kwa miezi 6 baada ya kuzaliwa, kisha akakata uhusiano naye kabisa. Kufikia sasa, yeye na mtoto wake wanaishi pamoja na familia yake, na mahusiano yote yamekatika, iwe ya kifedha, kimaadili, au kimwili. Kisha akajua kwamba alioa mwanamke mwingine na kwa sasa anaishi naye. Kisha mwanamume mwingine akamchumbia mke huyu, akitaka kumwoa. Aliuliza ikiwa bado alikuwa ameolewa, au ametalikiana kwa sababu alikuwa amekata mahusiano naye kifedha, kimaadili, na kimwili tangu 1991 hadi sasa? Afanye nini ili aolewe na mwanaume wa pili anayetaka kumuoa?

Soma zaidi....

Mipaka ya Uhusiano kati ya Mume na Mke

Ni kuhusu mipaka ya kishaia ya mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamume na mke wake, na je mwanamke ana haki ya kumtii mumewe katika kila anachotaka kutoka kwake wakati wa kujamiiana?

Soma zaidi....

Kumuoa Dada wa Baba au Mjomba kwa Mama

Nina mjomba wa upande wa mama yangu tu, na mjomba huyu ana dada wa upande wa baba tu. Je, inajuzu kwangu kumuoa?

Soma zaidi....

Sherehe ya Ndoa Katika Nyumba ya Bibi-arusi na Mahari yake

Katika nchi yetu - Turkistani Mashariki - sherehe ya ndoa hufanyika katika nyumba ya bibi-arusi. Je, hatua hii inapingana na sheria au inaonekana kama uzushi? Pia, kuna desturi kwamba mlezi wa bibi-arusi anachukua mahari kutoka kwa mume, na anatumia hiyo kununua vifaa vya ndoa kama dhahabu na mavazi, na yaliyobaki hutumika kwa gharama za sherehe ya ndoa. Je, haya ni halali?

Soma zaidi....

Ndoa yenye shahidi mmoja

Ni kuhusu uhalali wa mkataba wa ndoa ya kimila, mada ya Kesi Na. 17 ya 2008, Familia, iliyowasilishwa na/N. C. Dhidi ya/R. M., ambaye alimwoa kwa njia ya ndoa ya kimila 8/11/2007, na ilishuhudiwa na shahidi mmoja na bila kufahamu mlezi wake.

Soma zaidi....

Kufunga ndoa msikitini tena baada ya kuifunga nyumbani.

Ninaandika mkataba wa ndoa katika nyumba ya mmoja wa bibi arusi mbele ya familia zao na idadi ndogo ya watu. Ndoa ikikamilika hutangazwa Msikitini. Kisha tunafanya mkataba wa hiari na kukubali tena mbele ya umati wa watu na walioalikwa. Baadhi ya watu wanatupinga kwa hoja kwamba Mtume (S.A.W) hakufanya hivyo. Ni ipi hukumu juu ya hilo?

Soma zaidi....

Utiifu kwa Mume

Ikiwa mwanamke ataolewa na mumewe akafunga naye ndoa na yeye anaishi nyumbani kwake, ni jukumu la nani kumsaidia? Baba au mume?

Soma zaidi....

Kufunga Ndoa kwa Njia ya Simu

Nini maoni yako kuhusu ile inayoitwa “Kufunga ndoa kwa njia ya simu” ambayo imeenea kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu siku hizi?

Soma zaidi....

Ndoa na Mahurulaini (mabikira wa peponi)

Tulichagua mada ya "ndoa" kama moja ya mada zilizofunikwa na jarida letu kwenye Jukwaa la Utamaduni la Austria huko Cairo (Ubalozi wa Austria). Hii ni pamoja na ndoa katika Uislamu. Kwa hivyo tunahitaji habari fulani. Kwa kuwa kuna habari nyingi kwenye Mtandao ambazo zinapingana kwa sehemu kubwa, hivyo sisi tunakuelekeeni nyinyi moja kwa moja.

Maswali:

Je, peponi kuna ndoa katika maana ya kidunia? Je, peponi kuna ndoa kama tujuavyo - yaani, kati ya mwanamume na mwanamke? Je, ni lazima kuwe na ndoa peponi na pia kuna talaka? Je, kutakuwa na uaminifu kwa mmoja wa wenzi wa ndoa peponi? Daima tunasikia kwamba wanaume watalipwa peponi kwa Mahurulaini, lakini je, hii inatumika pia kwa wanawake? Kwa ujumla, wanawake watalipwaje thawabu peponi?

Mada nyingine ni:

Nini maoni ya Uislamu kuhusu ushoga - yaani, mwanamume na mwanamume na mwanamke na mwanamke?

Natumaini mnaweza kutusaidia katika utafiti.

Shukrani

Soma zaidi....

Mume kumbana Mke wake katika Matendo yake yote.

Nimechanganyikiwa kuhusu haki zangu kama mama na wajibu wangu wa kumtii mume wangu. Kwa mfano, je, nina haki ya kuamua binti yangu ale nini, anapolala, au nimnyonyeshe au la? Ikiwa najua sina maziwa ya kutosha kumnyonyesha, je, mume wangu ana haki ya kukasirika na kunifokea kwa sababu hiyo? Je, ana haki ya kuamua kuhusu kumuogesha mtoto wangu na kuweka kikomo kwangu kufanya hivyo kila baada ya siku 2-3? Je, ana haki ya kukasirika nisipokata nyanya kama anavyotaka yeye au nikiweka mbatata nyingi kwenye chakula? Je, ana haki ya kuniambia la kusema katika kila hali ninayokumbana nayo: ninapoghairi mkataba wangu na kampuni ya simu, au ninapoenda kwenye maktaba na kukuta kwamba wamenitoza faini isiyo na sababu? Je, nina haki ya kutumia akili yangu au kuchukua hatua ya kwanza kutatua matatizo fulani ya kimsingi? Haki yangu kama mama ni ipi? Je, nina haki ya kufanya yaliyo sawa kwa binti yangu licha ya kuingiliwa na mume wangu?

Soma zaidi....

Kumkalifisha Mke Kufanya Kazi za Nyumbani

Ningependa kujua kama sharia ya Kiislamu inawalazimisha wanawake kufanya kazi za nyumbani. Ahsante.

Soma zaidi....

Hukumu ya Kusafiri Mke Kinyume na Mapenzi yake

Nimeoa na nina mtoto wa mwaka mmoja na nusu. Kwa sasa ninafanya kazi Saudi Arabia na nina kazi nzuri na mshahara mzuri pia. Mke wangu aliniuliza kabla sijasafiri kukaa Misri kwa takriban mwezi mmoja ili kumaliza mambo fulani kabla ya yeye kusafiri. Lakini hivi majuzi aliniambia hangekuja; kwani haipendi nchi hii kwa sababu kuna joto sana na hakuna michezo ya mtoto na hataki akae hivi bila kufanya chochote maana itaathiri akili yake, pamoja na kujua kwamba ninawapa njia zote za faraja. Lakini kama mnavyojua kazi ni ngumu sana kwani mimi hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni. Hakuna umuhimu wa kumpeleka nje kila siku baada ya kazi. Sijui nifanye nini? Nataka maisha yenye utulivu na familia yangu, na sitaki kuyatumia kwenda na kurudi Misri, na siwezi kumudu gharama za usafiri. Nini maoni ya Kiislamu juu ya hali hii?

Soma zaidi....

Mke Hupewa Jina la Familia ya Mume.

Ndoa katika Ufaransa inampa mke jina la mumewe, mtazamo wa Dini ni nini kuhusu suala hili? Je, ni kosa kama Muislamu akifanya hivyo ? 

Soma zaidi....

Mke Kujizuia Kulala Kitandani Pamoja na Mumewe.

Mke akiwa amegombana na mumewe kisha akakataa kulala naye kitanda kimoja, je jambo hili linakubalika? Kwa kuzingatia kwamba sababu ya kukataa kwake ni kuwa mumewe anamtaka kila mara, naye mke huwa analalamikia tabu azipatazo za kuihudumia nyumba na watoto mchana kutwa, na pia matamanio yake huwa yako mbali tofauti na mumewe. Nini kifanyike? Je mke akiongea na mumewe kwa jeuri atapata adhabu ya moto?

Soma zaidi....

Tovuti za kuwezesha ndoa

Niko mbioni kuanzisha ofisi ya huduma ya kuwezesha ndoa. Tafadhali naomba hukumu ya kisharia juu ya hili?

Soma zaidi....

Kumlaumu mke kwa dhambi yake

Mume wangu na mimi tumepitia nyakati ngumu, kwa bahati mbaya kutokana na dhambi zangu. Alinitaliki mara mbili kabla ya hivyo. Tumepatanishwa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu, na tumeazimia kuwa na ndoa yenye furaha. Hata hivyo, mara nyingi mimi huona shaka machoni pake, kwani imani yake kwangu imetikisika. Je, mnatushauri tufanye nini ili maisha ya ndoa yetu iwe na utulivu? Je, kuna kitu kama "utakaso" baada ya nyakati hizi ngumu za ugomvi baina yetu, sisi tunasoma sana Qurani Tukufu, na tunataka kumkaribia Mwenyezi Mungu na kumshukuru milele? Pia ningependa mtujibu iwapo inajuzu katika Uislamu ndoa kuendelea ikiwa pande zote mbili zina nia ya kutopata watoto. Mimi ni mke wa pili na mume wangu ameoa mwanamke mwingine na ana watoto wawili naye. Sina watoto na mume wangu hataki kuzaa na mimi kwa sababu ya kosa nililofanya huko nyuma. Mume wangu anataka kujua ikiwa ana haki ya kufanya hivyo na ikiwa kupata watoto ni jambo lisiloepukika katika ndoa ikiwa uwezo wa kupata watoto unathibitishwa kinadharia? Asante sana.

Soma zaidi....

Kuolewa na wazee

Wapo baba na mama wanaowalazimisha mabinti zao kuolewa na wanaume waliowazidi miaka zaidi ya ishirini, hasa ndugu wa Kiarabu. Kuna soko maalumu la kuolewa wasichana baada ya kuwapa baba zao pesa. Ndoa hizi zote zinashindwa, na wasichana wanarudi Misri tena, kwa kushindwa. Swali ni: Je, inachukuliwa kuwa ni kutomtii mzazi ikiwa wasichana wanawaasi baba zao au walezi katika kuikubali ndoa hii na kueleza kutokubali kuolewa? Je, inajuzu kwa ndoa kukamilika kati ya baba na bwana harusi bila ya uwepo wa msichana na ridhaa yake? Je, inajuzu kuwaadhibu wazazi hawa katika mazingira kama haya? Je, wana msimamo gani wa kaka wa kiume wanaowalazimisha dada zao kufanya hivi?

Soma zaidi....

Kusafiri kwa Mume na Kutokuwepo kwake kwa Mkewe

Ikiwa mtu hayupo katika nchi yake ili kusafiri hadi nchi ambako anwani yake, kazi yake, kampuni zake, na mahali anapoishi, Je, anahesabiwa kuwa hayupo na maisha yake au kifo chake hakijulikani, au ni msafiri na bado yu hai kwa mujibu wa sharia? Kwa kujua kuwa yeye hutembelea nchi yake mara kwa mara akiwa na wenzake na marafiki zake kutoka nchi anayosafiri, na pia husafiri baina ya sehemu mbalimbali za dunia kwa ujumla na hasa nchi za Kiarabu.

Soma zaidi....

Mke kusafiri na Mumewe Kwenda Nchi ya Uhamisho

Muulizaji anasema kuwa ameolewa na mwanaume na ana binti naye. Alisafiri pamoja naye hadi Japani kwa muda wa mwaka mmoja, kisha akarudi Misri na kusafiri naye tena hadi Kanada kwa muda wa miezi miwili. Alirudi Misri kwa sababu ya kuogopa nafsi yake mwenyewe na binti yake kutokana na majaribu ambayo Waislamu wanakabiliwa nayo huko. Mumewe alikataa kumpatia matumizi yeye na bintiye kwa kisingizio kwamba hamtii. Afanye nini? Je, amtii na kwenda naye katika nchi ya uhamisho ambako Waislamu wanateswa na mateso ya kidini, huku akihofia majaribu kwa nafsi yake na binti yake, au afanye nini?

Soma zaidi....

Mke anamsaidia baba yake kwa pesa zake mwenyewe.

Je, mume ana haki ya kumzuia mke wake kutoa msaada wa kifedha kwa baba yake mzee ambaye hawezi kufanya kazi kwa pesa zake mwenyewe? Je, ni ipi hukumu ya Kiislamu kwa mume kutumia nguvu na jeuri kwa mkewe hadi kusababisha alama kwenye mwili wa mke na kutoa maneno yanayopingana na dini ya Kiislamu?

Soma zaidi....

Kutotimiza kwa Mume Ahadi zake

Mume wangu hakuwa mwaminifu kwangu na alienda kinyume na kila kitu tulichokubaliana. Iwe katika makao yetu au katika jinsi alivyonitendea mimi na watoto wetu, alinitendea vibaya na kunishambulia mimi na watoto wangu zaidi ya mara moja, na akafanya maisha ya familia yetu kuwa habari ya kuchapishwa katika magazeti na kuwapa habari zisizo za kweli kunihusu. Je, ni ipi hukumu ya Sharia ya Kiislamu juu ya hili?

Soma zaidi....

Kunyanyasa watoto na mke.

Mume wangu alijaribu kunikinaisha kuwa pigo la mume kwa mkewe na kumuadabisha na kumtisha na kumtia hofu pia kwa watoto ni katika mambo yanayofaa kwa mujibu wa sharia ya kiislamu. Pamoja na kuwa ninasoma Qur`ani Tukufu siku zote ila nimehisi kuwa jambo hili si sahihi bali niliona kinyume chake kuwa Uislamu ni dini ya huruma na upole.

Je, madai ya mume wangu ni sahihi?

Soma zaidi....

Gharama za Matunzo ya Binti ambaye Hajaolewa

Je, baba anawajibu wa kumgharamikia bintiye ambaye hajaolewa ingawa binti huyo ana kipato chake kinachomtosha?

Soma zaidi....

Gharama za Kumwozesha Binti

Je, gharama za kumwozesha binti na matumizi yake ni wajibu wa nani, baba au mama?

Soma zaidi....

Kutengawa kwa Mamlaka ya Kifedha ya Mke na Mamlaka ya Kifedha ya Mumewe

Ni ipi athari ya ndoa katika haki za kifedha za wanandoa na ipi hukumu ya kutengawa kwa mamlaka ya kifedha ya mume na mamlaka ya kifedha ya mkewe kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu?

Soma zaidi....

Hukumu ya kumdai Mume Vitu vya Nyumbani (orodha ya samani) Atakapo jivua (Khul’u, ) na Matunzo ya Mke Muasi

Ni ipi hukumu ya gharama za Matumizi na matunzo kwa mke Muasi? Na ipi hukumu ya kumdai mume dhahabu na vitu vya nyumbani Atakapo jivua (Khul’u, )?

Soma zaidi....

Kupetuka Mipaka katika Mahari na Athari zake

Kuna tatizo la kijamii nchini India hasa katika eneo la Milibar, eneo hili linawasichana wengi wa Kiislamu ambao hawakuolewa, kwa sababu ya mahari kuwa juu. Muulizaji anaomba kuwekewa wazi hukumu ya sharia katika hilo?

Soma zaidi....

Mipaka ya Miamala kati ya Wanadoa kabla ya Harusi

Naomba kufahamu kwa ujuzi na maarifa yenu ambayo tunayafuata kwa kuwa sisi si wajuzi wa baadhi ya mambo, hivyo tunaomba ushauri kwa wenye elimu na maarifa, ili tufanye mambo kwa mujibu wa Fatwa zenu katika mambo hayo:

Mimi ni kijana mwenye umri wa kiaka ishirini nane, nimeoa miezi mitano iliyopita lakini sijamuingilia mke wangu, kutokana na hali anayopitia kijana kwa zama zetu, baadhi ya rafiki zangu wameniambia kwamba huyo anazingatiwa kuwa ni mke wangu, na ninaweza fanya nae tendo la ndoa muda wa kuwa tumeshafunga ndoa mbele ya ndugu na jamaa, japo sina haki ya hilo. Nataka kujua ni upi ukomo wa mahusiano yetu ya mke na mume?

Soma zaidi....

Hukumu ya Ndoa ya Misyaar (Ndoa ya Mwanamke kukubali kuacha baadhi ya haki zake)

Tunatarajia kutoka kwenu wanazuoni waheshimiwa kutuelezea maana ya Ndoa ya Misiyaar, na mtubainishe hukumu yao?

Soma zaidi....

Ndoa ya Mwanamke Aliyejitolea

Hivi karibuni kupitia baadhi ya vituo vya runinga kuna mtu amejitokeza na kutangaza kile kinachoitwa “Ndoa ya Mwanamke aliyejitolea” na anasema: Ndoa hii inakamilika ikiwa mwanamke atasema kumwambia mwanamume: “Nimejimilikisha kwako mimi mwenyewe”, kisha mwanamume akamjibu: “Na mimi nimekubali, na nitakuandikia uhuru kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa - mfano - itakuwa ni thamani ya uhuru wako”. Kisha akasema huyu mtu: Hakika mwanamke kwa maneno haya anakuwa ni mtumwa kwa huyu mwanamume, hivyo anaweza kuishi naye maisha ya ndoa, na kuwa na uwezo mwanamke wa kuimaliza ndoa hii au utumwa huu kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa nia ya kutengana, basi atakuwa huru kwa mara nyingine,

Huyu mtu anajaribu kuyaunga mkono maneno yake kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} [AN-NISAA, 03].

Pamoja na kauli ya Mola Mtukufu: {Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara} [An-Nisaa, 25].

Na kuwa Mtume S.A.W. alijiwa na mwanamke mmoja na kujitoa yeye mwenyewe mwanamke kutaka kuolewa na Mtume - na wala hakusema nimejioza kwako mimi mwenyewe - basi baadhi ya Masahaba walitaka kumwoa, akamwambia: “Nimekumilikisha kutokana na Qur`ani uliyonayo” anasema: Hakika hii ni dalili ya uhalali wa kuoa mwanamke aliyejitoa kama zawadi yeye mwenyewe kwa mwanamume, na anasema: Hakika makubaliano ya kimataifa ya kuondoa utumwa hayazingatiwi ni jambo la lazima kutekelezwa na Waislamu katika kuharamisha kilichohalalishwa na Mwenyezi Mungu, na anasema pia: Hakika hizi ni jitihada zake ambazo haipaswi kwa yeyote kuzizuia, hivyo tunatarajia uwazi na ukweli wa madai haya kwa upande wa kisharia.

Soma zaidi....

Hukumu ya ndoa ya kimila za utotoni

Ni ipi hukumu ya kisheria ya ndoa za kimila za utotoni?

Soma zaidi....

Ughali wa mahari na athari zake

Ni ipi hukumu ya Kisharia katika ughali wa mahari na athari zake?

Soma zaidi....

Ndoa ya Misyaar

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Soma zaidi....