Kuuliza kuhusu Mwenyezi Mungu kwa [...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuliza kuhusu Mwenyezi Mungu kwa [yuko wapi?]

Question

Mtu anaye ni uliza kwamba: Mwenyezi Mungu yuko wapi? Naweza kumjibu kwa kusema nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kama ikiwa ni aya swali hili ni kujua mahali pa Mwenyezi Mungu na upande wake, na jibu lake linahitaji kuthibitisha mahali na upande wa Mungu Mwenyezi, tunasema kwamba haifai kuuliza Mwenyezi Mungu yuko wapi kwa maana hii, kwa sababu upande na mahali vinahusiana na vitu vingine, kwa maana kwamba kama tukitaka kueleza kitu kimoja katika upande maalum hali hii inahitaji kwamba upande huu uwe unahusiana na kitu kingine. Tukisema, kwa mfano: Anga katika upande wa juu, basi upande wa juu utakuwa juu ya wanadamu, na upande wa chini kwa angani, na kadhalika, na kwa kuwa upande siyo maalumu kabisa, basi haifai kusema hivyo, Mwenyezi Mungu Hana mfano wake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitakatifu: {Hakuna kitu kilicho mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona} [Ash-Shura: 11]. Mtu analazimika kutofikiri akilini mwake, katika nafsi ya Mwenyezi Mungu kwa njia ambayo inaleta picha. Jambo hili ni hatari kubwa na linasababisha kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe wake. Ni lazima kutafakari juu ya nguvu zake na ishara za ukuu wake ili tujizidishe imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ni lazima Mwislamu aamini kwamba Mwenyezi Mungu ni wajibu wa kuwepo kwake, na maana ya hiyo ni kwamba: Hairuhusiwi kwake kutokuwepo. Yeye hakubali kutokuwepo tangu na tangu, na kamwe, na kwamba kuwepo kwake ni kwa utashi wake binafsi na wala siyo kwa sababu moja au nyingine. Kwa maana kwamba mwingine hana taathira juu ya kuwepo kwake Mwenyezi Mungu. Itakuwa haina maana kuwa wakati na mahali zinaathiri kuwepo kwake na sifa zake.
Waislamu wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ana sifa ya utangu. Yaani: Wao wanathibitisha sifa ya utangu, nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye wa tangu na tangu na ndiye wa milele yeye mwenyewe pekee, na ina maana ya kuwa hakuna mwanzo wakuwepo kwake, au hakuna uwepo wa awali kabla ya kuwepo kwake. Na maana hii tumeitoa kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: {Yeye ndiye wa Mwanzo} [AL-HADID:3].
Na Hadithi ya Mtume S.A.W. "Wewe ndiye wa Mwanzo na hakuna chochote kabla yake" [Imepokelewa kutoka kwa Muslim katika Sahihi yake]. Basi sifa ya utangu inakanusha kuwa kuwepo kwake kumetanguliwa na kutokuwepo au kuwa kuna chochote kabla ya kuwepo kwake. Yaani sifa hii inakanusha kwamba kuna viumbe kabla yake.
Pia sifa za Mwenyezi Mungu ni za tangu, nazo hazina mabadiliko kufuatana na matukio, na kuthibitisha mahali na upande kunasabibisha mabadiliko haya. Kwa maana kwamba Mwenyezi Mungu hakuwa na sifa ya ujuu wa upande isipokuwa baada ya kuumbwa kwa ulimwengu, kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu hakuwa katika upande wa juu kwa sababu hakuna viumbe vinavyoishi chini, na kwa hivyo, sifa ya ujuu ni sifa inayoathiriwa na vitu vingine, basi kwa hivyo sifa hii haifai kuwa sifa ya Mwenyezi Mungu.
Na tunafahamu hivyo kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hakuna kitu kilichona mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona} [ASHURA: 11], Na miongoni mwa Hadithi za Mtume S.A.W. ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ubai ibn Ka'b R.A. Kwamba washirikina walisema: Ewe Muhammad taja asili ya Mola wako mlezi, Mwenyezi Mungu alijitambulisha kuwa: {Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee (1) Mwenyezi Mungu Mkusudiwa (2)} [AL-IKHLAS: 1.2] alisema, “Mkusudiwa” ni ambaye {Hakuzaa wala hakuzaliwa (3) Wala hana anayefanana naye hata mmoja (4)} [AL-IKHLAS: 3,4], kwa sababu hakuna kitu ambacho huzaliwa ila hufa, na hakuna kitu ambacho kina kufa ila hurithiwa, na kwamba Mwenyezi Mungu hafi wala harithiwi, {Wala hana anayefanana naye hata mmoja} [AL-IKHLAS: 4], alisema: “hana anayefanana naye, hakuna kitu kilicho mfano wake”. [Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim katika Mustadrak katika tafsiri ya Sutatu lIkhlas 2 / 589. Akasema: Hadithi hii mapokeo yake ni Sahihi].
Mwenyewe Mwenyezi alijieleza, na Mtume wake S.A.W. alimweleza, kwa kuwa hana anayefanana naye, na Waumini wamefahamu hivyo.
Na kutokana na hayo yaliyotangulia hapo juu, hairuhusiwi kumzungumzia na kumwelezea Mwenyezi Mungu kwa sifa hizi, wala hairuhusiwi kumwulizia kwa sifa zile, basi haiwezekani kumwulizia Mwenyezi Mungu kule aliko kwa nia ya kujua upande wake na mahala pake, lakini inaruhusi wa kuulizia Mwenyezi Mungu alipo kwa nia ya kujua utawala wake, au malaika wake, au kitu chochote ambacho inawezekana kukiulizia kuhusu kitu hicho, na kukielezea kwa sifa hizi. Na kutokana na hayo, maana ya yale yaliyotajwa katika Sheria kuhusu kuuliza wapi wa Mwenyezi Munguau kuelezea kuhusu upande wake yana tafsiriwa kwanza maama yake,
Na Mwnyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas