Kubadilisha Herufi kwenye Neno Tala...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadilisha Herufi kwenye Neno Talaka kwa Herufi Nyingine

Question

Kubadilisha Herufi kwenye Neno Talaka kwa Herufi Nyingine

Answer

Utafiti wa msingi wa Sharia

Umeandaliwa na

Kitengo cha Tafiti za Sharia ofisi ya Mufti wa Misri

Watafiti wa kitengo cha tafiti za Kisharia

 Ayman Aarif         Mustafa Abdallah

       Khalid Umran        Mustafa Abdulkareem

Aliyeshiriki na kupitia

Ahmad Mamdouh Saad

Mkuu wa kitengo cha tafiti za Kisharia

Utangulizi

Kwa jina la Mwenyezi Mungu na Shukrani zote za Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimuendee Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.

Baada ya Utangulizi:

Miongoni mwa sifa muhimu za Sharia Tukufu za Kiislamu ni Sharia zenye kukamilika, hakuna tukio lolote isipokuwa litakuwa lina hukumu katika dini ya Mwenyezi Mungu, na hakuna kitendo chochote katika vitendo vya mtu aliyepewa amri na Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Amehukumu hukumu inayofungamana na wajibu au haramu au kutakiwa au kuchukiza au halali.

Mwenyezi Mungu Amesema: {Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini} Al-Maidah: 3.

Imamu Shafii anasema katika kitabu cha Risala: “Hakuna kinachoteremka kwa watu wa dini ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna dalili ya uongofu”([1]).

Na Imamu Al-Haramain Al-Juwainy amesema: “Rai na mtazamo uliokubalika kwetu ni kuwa hakuna tukio linalokosa hukumu ya Mwenyezi Mungu inalotokana na kanuni ya Sharia”([2]).

Na Imamu Abu Mudhwfaru Sam’any amesema: “Lazima Mwenyezi Mungu awe na hukumu katika kila tukio”([3]).

Katika huruma ya Mwenyezi Mungu sio dalili zote za Kisharia kuwa na mfumo mmoja wa hukumu, kwani katika hilo ameacha mlango wazi kwa watu wenye akili inayokubalika na kuwa na uwezo wa mtazamo na jitihada ili kuangalia maandiko ya Sharia na kufahamu kusudio la Mwenyezi Mungu na kulifikisha kwa waja wake pasi na hofu ya dhambi au adhabu, Mtume S.A.W. akasema: “Kiongozi anapohukumu jambo kwa jitihada kisha akapatia basi ana malipo ya aina mbili, na pindi anapohukumu kwa jitihada kisha akakosea basi anamalipo ya aina moja”([4]).

Kutofautiana Wanachuoni ni sehemu ya sura ya usamehevu wa Sharia hii na upana wake na kufaa kwake kwa wakati wote na sehemu yoyote, ambapo wote wanachukuwa kutoka chimbuko moja.

Kwani Wanachuoni wametofautiana katika matawi mengi ya Sharia, miongoni mwa matawi yenye tofauti kwa Wanachuoni Waislamu ni yale yanayohusiana na mlango wenye hatari kubwa na athari ya kina, ambapo mlango huo unahusiana uharamu na kuhalalisha tupu iliyowekewa ulinzi imara, nao ni mlango wa talaka.

Katika utafiti huu tutaeleza masula katika masuala ya mlango huu, nao ni mlango wa kubadilisha herufi ya neno talaka kwa herufi nyengine, na je talaka inabaki kuwa ya wazi au ya fumbo?

Tutataja tuliyoyapitisha na kuyajengea dalili na sababu, na kuyasaidia kwa kanuni za Kisharia na nukuu za Kifiqhi. Utafiti huu umekuja katika tafiti sita:

Utafiti wa Kwanza: Ufafanuzi wa makusudio ya kubadilisha herufi ya neno talaka kwa herufi nyingine.

Utafiti wa Pili: Talaka ya wazi na ya fumbo.

Utafiti wa Tatu: Hukumu ya kubadili herufi za neno talaka kwa herufi nyingine.

Utafiti wa Nne: Dalili za madhehebu yaliyoangaliwa.

Utafiti wa Tano: Sababu ya kuteua upande huu katika Fatwa.

Utafiti wa Sita: Jumla ya pingamizi na majibu yake.

Utafiti wa Kwanza

Ufafanuzi wa kusudio la kubadilisha herufi katika neno talaka.

Maana ya kubadilisha katika lugha: Ni kugeuza, au kwa maana ya kuwepo kitu sehemu ya kitu chingine kilichoondoka, husemwa kwa mfano: Hiki kina maanisha kitu na mbadala wake, na wanasema tena: Nimebadilisha kitu pindi unapokigeuza hata kama haujaleta mbadala. Mola Mtukufu Anasema: {Sema: Haiwi kwangu kubadilisha kwa utashi wa nafsi yangu} Yunus: 15. Nimekibadilisha pale unapoleta kitu chengine nafasi yake([5]).

Na maana ya neno talaka: Ni tamko la talaka ya wazi, nalo: Ni neno lisilohitaji nia kupatikana talaka.

Kutokana na hilo, kusudio la kubadilisha herufi ya neno talaka kwa herufi nyingine, kwa maana: Kubadilisha herufi au zaidi ya herufi moja za neno talaka ya wazi kwa herufi nyingine, na hilo ni kama kusema: “Taaliqu” badala ya neno “Twaaliqu” kwa manaa ya mwenye kuachika, na mfano wa hayo miongoni mwa maneno maarufu katika lugha ya Misri na kwingineko, kubadilisha herufi ya “Qaaf” kwa herufi ya “Hamza” na kutamkwa: “Twalii” badala ya “Twaaliq” kwa maana ya mwenye kuachika.

Utafiti wa pili

Tamko la wazi na fumbo katika talaka

Talaka haiwi isipokuwa kwa tamko, lau mtu atanuia talaka ndani ya moyo wake pasi na kutamka basi talaka hiyo haiwi kwa kauli ya Wanachuoni wengi, na Mtume S.A.W. amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameondoa kwa Umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi yake ikiwa hajayatamka au kuyafanyia kazi”([6]). Kwa sababu talaka ni matumizi yanayoondoa umiliki hivyo haiwi kwa nia kama vile kuuza au kutoa zawadi([7]).

Ikiwa imethibiti kinachozingatiwa katika talaka ni tamko, basi tamko hugawanyika sehemu mbili, tamko la wazi na tamko la fumbo, ufafanuzi wa mgawanyiko huo ni kama ufuatao:

Mlango katika kufahamu tamko la wazi:

Ama tamko la wazi katika lugha linakuja kwa maana mbili:

Maana ya Kwanza: Kuhusika, kwa maana neno limetengana na maneno mengine, inakusudiwa limeondolewa sifa inayochafua, kwa mfano unaposema: Kauli ya wazi: Ni ile ambayo haihitajiki dhamira au maana([8]).

Maana ya Pili: Ubainifu na uwazi, kwa mfano husemwa: Jambo ameliweka wazi: Kwa maana amebainisha na kulifichua. Ibn Faris anasema: “Uwazi ni kudhihiri kwa kitu na kuonekana kwake”([9]).

Ama katika maana ya kimsamiti, ni neno lilofahamika kusudio lake na kuingia ndani yake kibainishi na kinachohukumiwa([10]).

Na ikasemwa: “Maana iliyowekwa inayoendana na tamko au kuendana na ukweli au istiara”([11]).

Ama kusudio lake hapa: Ni ile inayokubaliana na maana ya kwanza kilugha: Nayo ni kuhusika, kwa maana inayotumika katika talaka na si kwa jambo jingine au huwekwa kwenye neno la talaka bila ya neno lingine.

Uwazi: Ni neno lisilochukuliwa uwazi wake zaidi ya talaka.

Wala halihitajiki tamko la wazi la talaka kuwepo nia ili talaka ipatikane, kwa sababu haiwi kwa tamko lingine, wala haipelekei nia kupatikana talaka, bali hutokea talaka kwa tamko hilo hata kama atanuia jambo jingine.

Imamu Az-Zarkashy anasema: “Tamko la wazi la talaka halihitaji nia, yamejengeka haya kwa kauli yao na wamezungumza maelezo mengi na kilicho karibu zaidi kinachosemwa: Tamko la wazi halihitaji nia” kwa maana ya nia ya kupatikana talaka, kwa sababu tamko ndio hasa maudhui yake hivyo imeondolewa nia.

Ama makusudio ya kuwekwa sharti, ili kuondoa masuala ya kutanguliwa na ulimi, na hapa hutengenishwa tamko la wazi na tamko la fumbo, kwani tamko la wazi linawekewa sharti moja: Nayo ni kukusudia tamko, na tamko la fumbo huwekewa sharti la mambo mawili: Kukusudia tamko na nia ya kutoa talaka([12]).

 Na kusudio: Ni kukusudia tamko la talaka pamoja na maana yake, kwa maana: Kulitumia katika maana yake na sehemu yake wakati wa kuwepo mtoa talaka([13]), hakuna talaka ya Kisharia kwa kukaririshwa, wala hakuna talaka kwa asiye Muarabu akatamkishwa neno talaka bila ya kufahamu maana yake, na talaka ya mtu aliyekosea kama vile kutanguliwa na ulimi, akiwa anataka kusema neno si talaka basi ulimi wake ukateleza na kutamka talaka pasi na kukusudia kwa kutaka kusema kwa mfano: Twahir kwa maana wewe ni msafi, au kutaka kusema Twaliba kwa maana wewe ni mwanafunzi, akajikuta ametamka “Twaliq” kwa maana wewe umeachika, hakuna talaka kwa hali hii kwa kukosekana makusudio([14]).

Na matamshi ya wazi yapo aina tatu: Talaka, Kuachana, na Upo huru. kwani imekuja ndani ya Qur`ani neno kuacha na upo huru kwa maana ya talaka, na yanayotokana na maneno haya matatu huzingatiwa ni talaka ya wazi: Kama kusema, nimekuacha, au wewe ni mwenye kuachika, au umeachika, au nimekutenganisha au na wewe mwenye kutenganishwa, au nimekuacha huru, au wewe mwenye kuachwa huru([15]).

Zarkashy amesema: Ama yasiyopokewa ndani ya Kitabu na Sunna, lakini yamezoeleka kidesturi kama mume kusema kumuambia mke wake: Wewe ni haramu kwangu, neno hili halijapokewa kwenye Sharia ni katika talaka, na imekuwa kawaida kidesturi kuikusudia talaka, lakini kilichosahihi zaidi ni fumbo([16]).

Na Imamu Assuyutwi amesema kwenye kitabu cha Al-Ashbah: “Imezoeleka kuwa chimbuko la tamko la wazi je ni kupatikana katika Sharia au mazoea ya kutumika? Kuna tofauti, na Assabaky akasema: Ambacho ninasema ni kuwa lenyewe lina hatua:

Hatua ya kwanza: Yaliyoelezewa na Qur`ani pamoja na Sunna na kuzoeleka kwa Wanachuoni na Waislamu hiyo ni kauli moja kwa moja ya wazi, kama tamko la talaka.

Hatua ya Pili: Maovu si yenye kuenea, kama tamko la kutengana, na kuacha huru kuna tofauti.

Hatua ya Tatu: Kuwepo bila ya kuenea, kama vile kutoa fidia, na ndani yake pia kuna tofauti.

Hatua ya Nne: Kupatikana kwake bila ya kupatikana neno la tatu, lakini imeenea kwenye lugha za wabeba Sharia, kama vile mwanamke kujivua kwenye ndoa, kilicho maarufu ni tamko la wazi.

Hatua ya Tano: Ambalo halijapokewa wala kuzoeleka kwa Wanachuoni lakini kwa Waislamu mfano: Halali ya Mwenyezi Mungu kwenye haramu, na sahihi ni kinaya([17]). Miongoni mwa matamko ya wazi pia: Kujivua kwenye ndoa ikiwa itatajwa mali, ikiwa mume atatamka tamko la wazi na akasema: Sijakusudia talaka – haikubaliki – na huondolewa lenye kuchukiza kwenye talaka, uwazi wake ni tamko la fumbo, ikiwa tutanuia talaka inapatikana na kama hakuna nia hakuna talaka.

Mlango katika kufahamu tamko la fumbo.

Ama maana ya fumbo katika lugha: Ni kuzungumzia kitu na kufahamika kifumbo bila kwa uwazi, kama vile kinyesi na haja kubwa, amesema katika kitabu cha Mukhtar As-Sahah: Fumbo, ni kuzungumza kitu na kukusudia kitu kingine([18]).

Na kwa upande wa watu wa ubainifu wana maanisha ni tamko linalokusudiwa maana yake pamoja na kufaa maana inayokusudiwa wakati huo, kama kusema: Mbeba upanga mrefu, kwa maana mrefu wa kimo([19]).

Kwa upande wa msamiati, ni jina limeficha kusudio la mzungumzaji kwa upande wa tamko, kama kusema katika kuuza: Nimekufanyia kwa kiasi fulani([20]).

Ama kusudio lake hapa, ni kila tamko linalochukuliwa talaka, na inakosekana talaka kwa tamko hilo kwa kuhitajika nia, ikiwa mtu amenuia talaka hupatikana na kama hajanuia basi hamna talaka, katika mifano ya talaka ya mafumbo ni kama kusema: Wewe upo mbali, wewe umevuliwa na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yanayochukuliwa kama talaka([21]).

Utafiti wa Tatu

Hukumu ya kubadili herufi kuleta herufi nyingine katika neno talaka.

Tulichochaguwa kwa ajili ya Fatwa ni kuwa: Kubadili herufi ya neno talaka kwa herufi nyingine, inaitoa kwenye tamko la wazi na kufanya tamko liwe la fumbo, wala talaka haipatikani isipokuwa akiwa amenuia talaka, ni sawa sawa ikiwa ndio lahaja yake na lugha yake au hapana, na hili ndio tumeliteua na kupitishwa na wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafi.

Khatibu Sharibiny amesema: Ikiwa ataleta herufi ya Taa badala ya herufi ya Twaa kama kusema: Anti Taaliq, kwa maana ya wewe ni mwenye kuachika, inakuwa ni fumbo na sio talaka ya wazi kama alivyoeleza Sheikh Shihab Ramly, ni sawa sawa hiyo ndio lugha yake au hapana([22]).

Na Qalyuny amesema katika kitabu chake cha sherhi Al-Mahally lilminhaaj: “Kubadilisha herufi ya Twaa ni fumbo kwa kauli iliyopitishwa, hata kwa yule ambaye ni lugha yake([23]).

Na Imamu Assuyuty amesema katika risala yake pale alipoulizwa kwa yule atakayesema kumuambia mke wake: Anti Taaliq, akiwa mwenye kunuia kwa tamko hilo talaka je talaka inakuwa? Akajibu kwa kusema: Kilichokuwa kwangu ni kuwa ikiwa amenuia neno talaka basi talaka inakuwa ni sawa sawa amekuwa si mwenye kujua au anajua, wala haisemwi ikiwa atasema: Anti faaliq au maaliq kwa maana ya wewe mwenye kuachika basi hakuna talaka, kwa sababu herufi ya Taa ipo karibu sana na matoleo ya herufi ya Twaa, kila herufi moja hubadilishwa na nyingine katika maneno mengi hubadilishwa herufi ya Twaa kuwa Taa katika kauli zao([24]).

Na akasema pia: Ikiwa atasema: Anti daaiq, kwa kutumia harufi ya Daal inawezekana kuja yaliyokuja katika neno Taaliq kwa herufi ya Taa, kwa sababu herufi ya Daal na herufi ya Twaa pia zipo karibu katika kubadilishwa, isipokuwa tamko hili si maarufu katika lugha kama ilivyokuwa maarufu neno Taaliq, wala haiwezekani kuja kauli na kupatikana talaka ikiwa nia imekosekana([25]).

Na wakaelezea watu wa madhehebu ya Imamu Malik kuwa, hii ni katika mafumbo yasiyo wazi([26]) kama haitakuwa ndio lugha yake, Nafarawy anasema: Ama lau atadondosha baadhi ya herufi zake kwa kumuambia mkewe: Anti Twaal bila ya kuleta herufi ya Qaf ili kuleta maana ya: Wewe ni mwenye kuachika, basi hiyo inakuwa ni miongoni mwa mafumbo, na mfano wake ni kama anaposema: Anti Taaliq kwa kubadilisha herufi ya Twaa kuwa Taa ambapo haikuwa pia lugha yake([27]).

Inaonesha kuwa Imamu Shafi na Imamu Malik wamekubaliana kuwa matamshi haya ni katika maneno ya mafumbo – ambayo yanalazimu nia ili ipatikane talaka – ikiwa si katika lugha yake, na wafuasi wa Imamu Shafi wakaongeza na wakasema: Yenyewe ni katika maneno ya mafumbo pia hata kama itakuwa ni katika lugha yake.

Ikiwa katika neno talaka akaitamka herufi ya Qaaf ya kati na kati.

 Herufi ya Qaaf ya kati na kati ni ile ambayo sio herufi ya Qaaf wala si Kaaf, bali yenyewe ipo kati na kati kwenye kutamka baina ya herufi ya Qaaf na Kaaf ([28]), nayo ni herufi ya Jiim ya Kimisri, mfano wake: Kutamka neno: Maakuul: Maajul, kwa maana ya jambo linaloingia akilini.

Na kutamka herufi ya Qaaf ya kati na kati ni lugha ya watu wa Bani Tamim, Imamu wa taaluma ya lugha Al-Hussein Ibn Faris amesema: Ama Banu Tamim wao hukutanisha herufi ya Qaaf na kuwa mzito sana, wanasema: “Al-Qawmu” neno hili huwa kati ya Kaaf na Qaaf, na ndio lugha yao.

Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafi wameeleza juu ya usahihi wa Suratul-Fatiha pindi ikisomwa: “Al-Mustaqim” kwa maana iliyonyoka, kwa herufi ya Qaaf ya kati na kati kutokana kuwa ni Kiarabu sahihi, Imamu Jamal Ad-Din katika kitabu cha Kawkabu Durry herufi Haa katika haa ni lugha chache, vile vile kubadilisha herufi Kaaf na kuwa Qaaf…ya pili kwa maana ya kubadilisha herufi ya Kaaf kwenye Qaaf, miongoni mwa matawi yake: Ikiwa atasoma neno: “Mustaqiim” kwa Qaaf ya kati na kati inayofanana na Kaaf nayo Qaaf ya Kiarabu, kwa maana: Ambayo wanaitamka, yenyewe pia inakuwa kama alivyotaja Sheikh Nasri Al-Miqdisy katika kitabu chake kinachoitwa Al-Maqsuud wa Rawyany, na Al-Muhibu At-Twabary fii Sherhi Tanbiih kubatilika kwake, lakini usomaji katika Suratul-Fat’ha hauzuii usahihi ikiwa haibadilishi maana kama alivyoelezea Raafii, pamoja kuwa ni haramu kama alivyosema An-Nawawy katika sherhi ya kitabu cha Al-Muhadhibu, na akaelezea kuwa Sala pia haikubaliki, na hapo usahihi katika mfano wa hali kama hii ni kwa sababu ya kupokelewa kwenye lugha([29]).

Sheikh Zakaria Al-Ansari amesema katika sherehe ya kitabu cha Al-Minhaj: “Ni lazima kuchunga herufi zake – kwa maana ya herufi za Suratul-Fat’ha – akiwa mwenye kuweza au kuwezekana kujifunza akaleta badala yake herufi nyengine kisomo chake hakitafaa kwa neno hilo, kwa kubadilisha kwake mifumo, ikiwa atatamka Qaaf inayocheza kati ya Qaaf na Kaaf itakuwa ni sahihi kama alivyoeleza Rawyany na wengine([30]).

Na Mwanachuoni Ar-Ramly amesema: Ikiwa atatamka Qaaf iliyo kati yake na herufi ya Kaaf kama wanavyotamka baadhi ya Waarabu itafaa pamoja na kuwa inachukiza kama alivyosema Sheikh Nasri Al-Maqdisy na Rawyany pamoja na Ibn Rafaa katika kitabu cha Al-Kifaya pamoja na kuwepo mtazamo katika kitabu cha Al-Majmuui([31]).

Imamu Shihab Al-Qalyuny amesema katika Hawashi yake juu ya Sherhi Al-Muhally Al-Minhaaj: Kwa ujumla ni kuwa wakati anapokwenda kinyume na yanayowajibika katika Suratul-Fatiha kwa kusahau si haramu wala Swala yake haibatiliki wala kisomo chake, lakini lazima kurejesha herufi iliyobadilishwa au kubadilisha maana wakati wa kukumbuka….wala si katika chenye kubadilisha herufi ya Raa kwenye neno Ar-Rahman kuiweka silabi ya Dhamma, wala silabi ya Fat’ha katika neno: “Naabudu” kwa maana ya tunakuabudu, wala silabi ya Kasra kwenye herufi ya Nuun na kutamkwa “Nistaiin”, wala herufi ya Sad kuwekwa silabi ya Dhumma kuwa Swuratwa badala ya Swiratwa, wala kutamkwa baina ya Qaaf na Kaaf([32]), kwa sababu huko si kubadilisha, bali ni kuweka herufi isiyo sahihi, tofauti na maelezo ya Ibn Hajar([33]).

Na Sheikh Al-Baijury amesema kwenye kitabu chake cha Fiqhi – kwenye kauli ya mshereheshaji pale aliposema “Au alibadilisha herufi – kwa maana ya Suratul-Fat’ha - kwa herufi nyengine” kwa maana kama kusema: Ad-Dhiin au Ad-Diin kwa herufi ya Dhaal au Daal, au akasema: Al-Hamdulillah, kwa herufi ya Haa, au akasema: Ad-Dhwaliin, kwa herufi ya Dhwaa badala ya herufi ya Dhaad, au akasema: Al-Mustaiim. Kwa herufi ya Hamza badala ya herufi ya Qaafu, tofauti na lau atatamka herufi ya Qaaf iliyopo kati yake na Kaaf kama wanavyotamka Waarabu, yenyewe inafaa kama alivyosema Rawyani na wengine, lakini kuna mtazamo mwingine katika kitabu cha Al-Majmuui([34]).

Kutokana na maelezo yaliyotangulia ikiwa mume amemuambia mke wake: Anti Twaliq kwa herufi ya Kaafu iliyopo baina yake na Qaaf, kwa maana ya kusema wewe ni mwenye kuachwa ambapo matamshi yake yanakuwa: Anti Twalij kama ilivyo kwa lugha ya watu wa nyanda za juu kusina nchini Misri, hii inakuwa ni talaka sahihi na wala haiwi upande wa fumbo na wala haihitaji nia, kwa sababu kutamka Qaaf ya kati ya Kaaf ni utamshi wa Kiarabu na wala si wa kigeni kama ilivyoelezwa, na haya yanatengana kutamka Qaaf yenyewe wakati wa kutamka Hamza, na sehemu hii imeelezwa na Maimamu wa madhehebu ya Imamu Shafi ndani ya vitabu vyao.

Imamu Suyuty amesema katika risala yake kwenye kitabu cha Fat’hu Al-Maghaaliq akasema: Lau atasema: Anti Twaliq – kwa herufi ya Qaaf iliyo karibu na herufi ya Kaaf kama inavyotamkwa na Waarabu – basi hakuna shaka kutokea talaka([35]).

Na aliyosema Imamu Suyuty ni yaliyosemwa pia na Sheikh Ally Nurudiin Shabramallisi katika kitabu chake cha Nihayatul-Muhtaaj([36]), Sheikh Abdulhamid Ash-Sharwany katika kitabu chake cha Tuhfatul-Muhtaaj([37]). 

Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua zaidi.

Utafiti wa Nne

Dalili za madhehebu yaliyopitisha

Dalili ya Kwanza:

Ni kuwa neno pindi linapogeuzwa kwa kutokea mabadiliko kama vile kubadilisha herufi kwa herufi nyingine, na bila ya kuleta maana mpya, basi yenyewe inakuwa ni kama tamko lisilo tumika.

Neno lililopokewa katika lugha lina tamko lake, ikiwa litatamkwa kinyume: Ima libadilishe maana, au kutobadili maana.

Ikiwa litabadili maana litaleta maana mpya kilugha na Kisharia, kama aliyetamka herufi ya Dhaad Dhwaa akasema: “Walaa Dhwaaliin” badala ya kusema “Wala Dhaaliin”, na Dhwaallu maana yake ni kivuli hivyo hubadilika maana, ikiwa atasoma hivyo kwa makusudi na anajua kubatilika kwake basi Swala yake itakuwa imebatilika([38]), vile vile neno “Mustaim” kwa herufi ya Hamza badala ya “Al-Mustaqiim” kwa herufi ya Qaaf.

Ama kutamka kinyume ambako hakubadili maana, kama mtu kuleta herufi ya Waw badala ya herufi ya Yaa katika neno “Al-Aalamiin” katika Suratul-Fat’ha, mabadiliko haya hayabatilishi Sala([39]).

Katika tamko la talaka pindi inapobadilishwa herufi ya Twaa na kuwa Taa, kwa mfano akasema: Anti Taaliq, kwa maana: Wewe ni mwenye kuachika, basi talaka haikamiliki isipokuwa akiwa amenuia kuacha, kama ilivyoelezwa kwenye vitabu vya madhehebu ya Imamu Shafi([40]).

Inafahamika kuwa herufi ya Twaa na herufi ya Taa zinashirikiana katika matoleo na baadhi ya sifa, Sheikh Muhammad Nasri Makky amesema katika kitabu cha Nihayatu Al-Qauli Al-Mufiid katika mlango wa tatu kwenye kubainisha tofauti kati ya herufi zinazoshirikiana kati ya matokeo na sifa: Herufi ya Twaa na Taa zinashirikiana katika matolea, na herufi ya Twaa imekuwa na sifa ya pekee kutamkwa na kupewa uzito, lau kusingekuwepo tofauti hii ingekuwa ni Daal, na lau kusingekuwa na vinyume vya herufi ya Taa ingekuwa ni Twaa, na tofauti na herufi ya Daal na Taa ni uwazi tu, lau isingekuwa uwazi basi ingekuwa ni Taa, na lau isingezama kwenye herufi Taa ingekuwa Daal, kwani herufi ya Twaa ipo karibu zaidi na herufi ya Daal na herufi ya Taa pasi na kinyume, kwa sababu Daal ipo karibu na Taa na kinyume chake([41]).

Na inafahamika pia kuwa: Herufi ya Qaaf inatoka kwenye ncha ya ulimi([42]) na herufi ya Hamza ni katika herufi zinazotoka kwenye kolomelo, hivyo herufi ya Qaaf inatoka kwenye sehemu ya tano ya matoleo kati ya sehemu ya mbali ya ulimi kwa maana sehemu inayoangaliana na kolomeo juu ya koo, ama herufi ya hamza matoleo yake ya pili nayo ni sehemu ya mbali ya kolomelo([43]).

Imekuja katika kitabu cha Asna Al-Matwalib maelezo ya kubadili tamko la “Twaaliq” kwa maana ya mwenye kuachika kwa tamko la “Taaliq”, na tamko hili linaitoa talaka kwenye talaka ya wazi na kuwa talaka ya fumbo, na inapatikana talaka kwenye neno hilo pale kunapokuwepo nia ya kuacha, kwani herufi ya Taa ipo karibu na matoleo ya herufi ya Twaa na herufi hizo mbili hubadilishana matamshi mengi([44]).

Na kwa maelezo hayo ikiwa neno “Taaliq” ni neno lipo nje ya wigo wa talaka ya wazi na kuwa ni fumbo basi ni bora zaidi neno “Twaalii” kwa herufi ya Hamza linatoka kwenye talaka ya wazi na kuwa ya fumbo, na sababu ya kuwa ni bora zaidi: Ni kuwa herufi ya Taa na Twaa zinashirikiana kwenye matoleo na baadhi ya sifa, na herufi ya Hamza na Qaaf zinatofautiana katika matoleo, hivyo neno Twaalii kwa hamza ni bora zaidi kuitoa talaka kwenye uwazi kuliko neno Taaliq.

Ama kubadilisha herufi ya tamko la talaka kwa herufi nyingine iliyo nje ya wigo wa tamko linalotumika na kuwa tamko lisilotumika, kwa sababu maneno ya Kiarabu yanayotumika: Ni yale yaliyowekwa na Waarabu ili kuonesha maana maalumu, nayo yana kanuni haifai kubadilisha, na wakati yanapobadilishwa uhukumiwa kuwa si maneno ya Kiarabu, hivyo huwa ni maneno yaliyotupwa na kupuuzwa, wamekubaliana kuwa maneno yaliyotupwa hayajawekwa kabisa na Waarabu([45]).

Hivyo neno “Twaalii” si neno la Kiarabu na wala halitumiwi kama linavyotumiwa tamko la talaka ya wazi “Twaaliq”, kwa kutofautiana kanuni ya maneno ya Kiarabu, na kuwa kwake halijawekwa na Waarabu ili kuleta maana ya talaka.

Neno linachukuliwa kuwa ni la wazi katika talaka kwa kupokewa kwake Kisharia au kilugha inayopelekea maana maudhui yake na wala si vyengine, ama tamko la wazi katika Sharia na lugha ni neno Twalaaq, kwani limethibiti sehemu zote mbili, ama yaliyothibiti katika Sharia ni neno kuachwa huru na kutengana.

Ikiwa katika Sharia au lugha halijapokewa neno kwa njia inayopelekea maana ya maudhui basi maana yake inatoka kwenye talaka ya wazi na kuwa fumbo.

Al-Qurafi amesema: Maneno maarufu ni kuwa tamko likiwa linaleta maana ya kiluga basi hilo ni la wazi,  na hii ndio neno Twalaaq, kwa sababu ya kuondoka kwa kizuizi kwani husemwa: Tamko la moja kwa moja, muelekeo wa moja kwa moja na halali moja kwa moja.

Mwenye kitabu cha Al-Jawahir amesema: Muundo huu vyovyote utakavyotumika kwa mfano: Anti Twaaliq, Anti Mutwalliqa, Kadi Twallaqtuki, au Twalaaq laazim, au Auqaati Alaiki Twalaaq na Ana Twaaliqu Minki, yote hayo kwa maana ya umeachika.

Na fumbo: Si maudhui yake kilugha lakini hutumika kama kuazima kwa kuwepo uhusiano wa karibu([46]).

Kwa maneno ya Al-Qurafi yanaonesha maana ya wazi na fumbo na kiwango chake kilugha, na wakati wote tamko lisipokuwa maudhui ya maana kama vile neno Twaalii haliwi tamko la wazi.

Dalili ya Pili:

Tunasema kuwa lugha ni kitu cha kusimamiwa, na imewekwa na Mwenyezi Mungu kama ilivyoelezewa katika elimu ya Misingi ya Sharia([47]), na madamu matamshi haya kwa maana: Matamshi ya talaka yaliyopotoshwa kama vile kubadilisha herufi ya Twaa kuwa Taa na mfano wa hayo, hayakuwekwa kwa ajili ya talaka ya wazi, kwani yenyewe yanakuwa ni katika mafumbo ambayo yanahitaji uwepo pia wa nia.

Al-Isnawi amesema: Sheikh Abu Al-Hassan Al-Ash’ari amesema kuwa lugha ni jambo la kusimikwa, na maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu Ameiweka na kutuwezesha, kwa maana tumefundishwa, na kupitishwa na Ibn Al-Hajib katika maelezo ya kipimo cha lugha mbalimbali.

Na kauli nyengine ni kuwa: Mwanzo wa lugha ni msamiati na maneno mengine yaliyobaki yanachukuliwa.

Na Ubbad Ibn Sulaiman na Wanachuoni wengine wamesema: Matamshi hayahitaji kuwekwa, bali yana maanisha yenyewe kwa yaliyopo kati yake na maana zake zinazokubaliana, vile vile imenukuliwa katika kitabu cha Al-Mahsuul na kutokana na maneno ya Al-Aamady katika kunukuu kwake kuwa kukubaliana kuna sharti .. kisha akasema: Ikiwa utafahamu hivyo basi ni katika sehemu ya masuala:  .. ikiwa mume atamuambia mke wake: Anti Alayya Haram, kwa maana wewe kwangu ni haramu, au akasema: Halalu Allah Alayya Haram, kwa maana halali ya Mwenyezi Mungu kwangu haramu, au akasema, Haramu Yulzimuni, kwa maana haramu inanilazimu, na mfano wa hayo, je hayo ni matamko ya wazi au mafumbo? Kuna mitazamo miwili:

Imamu Raafii amepitisha mtazamo wa kwanza, na Imamu An-Nawawi amepitisha mtazamo wa pili, ikiwa tutasema: Lugha ni misamiati inatosha kujulikana kwa mazoea na matumizi mbali kabisa na nia, basi itakuwa ni tamko la wazi, nayo ameipitisha Raafi.

Ikiwa tutasema: Lugha ni kitu kilichowekwa hivyo haiwezi kuwa nje ya misingi yake, bali hutumika vingine kwa njia ya ukiukaji, ikiwa atanuia talaka inapatikana na kama hajanuia basi hakuna talaka, nayo ni sahihi kwa Imamu An-Nawawi([48]).

Dalili ya Tatu:

Mazingatio katika mlango huu ni ujenzi wa neno na wala si maana, na hili linaonekana wazi katika uteuzi wa Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafi wa matamshi ya talaka ya wazi, hivyo wakathibitisha tamko la “Twalaaq” bila ya tofauti, na tamko la “Kutengana na kuachwa huru” kuna tofauti, na wametofautiana kwenye kutokea talaka kwenye maneno hayo mawili, kwa sababu kwenye Aya yamekuja maneno hayo mawili. Al-Jalal Al-Muhaly anasema katika sherehe yake ya kitabu cha Al-Minhaj: Talaka inapatikana kwa tamko lake la wazi bila ya uwepo nia tofauti na tamko la fumbo linahitaji nia, na tamko la fumbo linalochukuliwa maana ya wazi na nyingine, “Uwazi wake ni: Twalaaq” kwa kufahamika kwake kwa upande wa lugha na Sharia, “Vile vile neno kutengana na neno kuwa huru yanafahamika” kwa sababu yamekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kwa maana yake Mwenyezi Mungu aliyosema: {Na muwaache kwa kuachana kwa wema} Al-Ahzaab:  49, na akasema: {Au muachane nao kwa wema} At-Twalaq: 2. Kauli ya pili: Maneno hayo mawili ni fumbo, kwa sababu yenyewe hayakufahamika ufahamikaji wa talaka, na yanatumika kwenye talaka na kwenye mambo mengine, mfano wa tamko la talaka ni kama kusema: Twalaqtuki na Anti Twaaliq na Mutwalaqa, na Yaa Twaaliq, yote yakiwa na maana ya wewe ni mwenye kuachika, kwa sababu chanzo kinatumika katika upanuzi hivyo yanakuwa ni mafumbo mawili.

Na kauli nyingine maneno haya mawili ni maneno ya wazi kama kusema: Yaa Twaaliq, kwa maana Ewe mwenye kuachwa, na kupima maneno mengine yaliyotajwa kama vile: Faaraqtuki, na Sarrahtuki, kwa maana nimetengana na wewe na nimekuacha huru, maneno haya mawili ni maneno ya wazi na sio fumbo, na mfano wa maneno kama: Anti Mufaaraqa na Musarraha na Yaa Mufaaraqa na Yaa Musarraha, kwa maana ya Wewe Mwenye kuachwa, maneno haya yote ni maneno ya wazi, na ikasemwa pia ni maneno ya fumbo, kwa sababu maneno yaliyokuja ndani ya Qur`ani Tukufu katika matamshi hayo mawili ni kitenzi pasi na jina tofauti na neno Twalaaq. Mola Mtukufu Anasema:  {Na wanawake walio achwa wangoje} Al-Baqarah: 228. Na neno Anti Firaaq na Farraaq au Anti Siraah na Sarraah kwa maana ile ile ya wewe ni mwenye kuachwa, hayo ni maneno ya mafumbo kwa kauli sahihi zaidi([49]).

Hii ni kana kwamba muelekeo wao ni kuwa, mazingatio katika mlango huu ni muundo na wala si maana, nayo ni kanuni ya Kifiqhi yenye tofauti katika matawi yake, imetajwa katika vitabu vya kanuni kwa jina: Hal Ibra biswiyaghi Al-Uquud au bimaaniiha? Kwa maana je mazingatio ni muundo wa makubaliano au maana zake?([50]).

Mazingatio katika makubaliano ni matamshi na muundo na wala si makusudio na maana, ndoa ni makubaliano na yanayofungamana nayo huondolewa kwa talaka, na mazingatio katika kuvunja ndoa ni matamshi na hilo ni kama kuingia kwake makubaliano kwa matamshi na hasa katika matamshi ya wazi, ama matamshi ya mafumbo yanahitaji uwepo wa nia.

Pindi kauli ya mume anapomuambia mke wake kwa mfano: Anti Twaali, kwa maana wewe ni mwenye kuachika, neno ambalo linavunja ndoa basi kinachozingatiwa na kupitishwa uvunjikaji huo ni tamko na wala si upande wa maana, na kulipotosha tamko kwa tamko lingine lisilofahamika katika Kiarabu asili ya matoleo yake, kutokana na hivyo haiwezi kuzingatiwa kuvunjika kwa ndoa isipokuwa ikiwa amenuia kutoa talaka, nia yake inakuwa ndio dalili ya utashi wake wa kuvunja ndoa, ambapo mazingatio ni maneno ya Kiarabu yaliyowekwa([51]), na neno Twaalii ni neno lisilo na maana ya wazi katika lugha ya Kiarabu ya kuvunja ndoa, bali linahitaji kukutanishwa na nia ya muachaji ya kauli ya kutoa talaka.

Imamu Suyuty ametaja katika sherehe matawi mengi ya kanuni hii: Miongoni mwake: Ikiwa atasema, nimekabidhi kwako hii nguo kwa mtu huyu, haiwi kukabidhi moja kwa moja, wala makubaliano ya mauzo hayapo kwa tofauti ya tamko. Pili: Kwa kuangalia maana, na mengine yasiiyokuwa hayo katika matawi yanayofanana.

Katika haya tunaona kuwa huyu mtu ametamka tamko sahihi la kukabidhi kwa upande wa lugha, lakini kosa ni kwa upande wa Sharia, kwa sababu amefanya tofauti na maana yake ambayo imewekwa katika Sharia, wala hawajazingatia yanayopelekea maana ya tamko iliyokubaliwa, kisha wakatofautiana katika mazingitio ya maana: Je inakuwa ni mauzo au hapana?

Hili limefanana na lau atatamka kwa tamko la kupotoshwa la talaka tofauti na lilivyo katika lugha ya Kiarabu kama vile kusema: “Anti Twaalii” kwa maana ya Wewe umeachika, basi ni bora zaidi kutochukuwa dalili ya moja kwa moja ya tamko hili kwenye talaka Kisharia isipokuwa kwa kuwepo dalili nyingine, nayo ni kumuuliza mtamkaji wa neno hili nini nia yake.

Mlango wa sehemu ya nia katika tamko la fumbo.

Yanayopaswa kuelezewa ni kuwa nia katika tamko la fumbo kwenye talaka inapaswa kuwa ndio ya kwanza, ikiwa mtu atatamka kwa lugha ya fumbo pasi na kuwa na nia kisha baada ya hapo ndio akanuia basi talaka haitakuwepo.

Imamu An-Nawawi amesema: “Neno la fumbo halifanyi kazi lenyewe, bali ni lazima kuwe na nia ya talaka, na kukutanishwa nia na tamko hata kama tamko litatangulizwa, kisha likatamkwa bila ya nia, au sehemu ya tamko kisha akaleta nia, inakuwa bado talaka haipo, ikiwa atakutanisha mwanzoni mwa tamko na sio mwisho wake, talaka inakuwa kwa kauli sahihi”([52]).

Ibn Qudama Al-Hanbaly amesema: “Ama talaka isiyo ya wazi haiwi isipokuwa kwa nia, au dalili ya hali, na Malik akasema, maneno ya mafumbo yaliyo wazi ni kama kusema: Anti Baain au Haram au Batta, kwa maana Wewe ni haramu kwangu au Wewe umeachwa, maneno hayo talaka inapatikana pasi na kuhitaji nia,

Al-Qadhi amesema katika Sherhu: Na haya ni maneno ya wazi ya Imamu Ahmad na Al-Kharaqi kwa sababu ni yenye kutumika katika talaka kwa mazoea, hivyo yamekuwa sawa na maneno ya wazi.

Na sisi tunasema: Maneno haya ya fumbo hayakufahamika kukusudiwa talaka, wala kuhusishwa na talaka, wala hapakuwa na talaka kwa kutamkwa tu kama vile mafumbo mengine, ikiwa itathibiti mazingatio ya nia basi itazingatiwa ni dalili ya tamko, ikiwa itapatikana nia mwanzoni mwake na kuwekwa wazi basi talaka itapatikana.

Baadhi ya watu wa Imamu Shafi wamesema talaka haitakuwepo, ikiwa atasema kwa mfano: Anti Baain, akiwa ananuia talaka na nia yake kuwa wazi pale aliposema: Anti Baain hakuna talaka, kwa sababu kiwango ambacho kimeendana na nia hakipelekei kitu chochote.

Na tunasema pia: Kinachozingatiwa na nia kinatosha kuwepo kwake mwanzoni mwake, kama vile ibada ya Swala na Ibada zingine, ama ikiwa atatamka kwa neno la fumbo pasi na kunuia, kisha akanuia baada ya hapo, talaka haitakuwepo, ni kama vile amenuia kujisafisha kwa kuoga baada ya kumaliza kuoga([53]).

Utafiti wa Tano

Sababu ya Kuteua Mwelekeo huu katika Fatwa

Kazi ya Fatwa haitokani na kuwa Ijtihada katika utekelezaji wa hukumu za Kisharia kwenye uhalisia, kwani kwa mtazamo huu inapingana na kazi za utohoaji wa hukumu za Kisharia, ambapo hukumu haibadiliki lakini fatwa hubadilika kwa kubadilika pande zake kuu nne: Wakati, sehemu, watu na hali, kama inavyofahamika katika dhana yake.

Fatwa ya kati na kati ndiyo inayofikia makusudio ya Sharia na wala haiharibu andiko wala urithi, hivyo mwenye kuchunga hayo Fatwa yake inakuwa ipo sawa, kwa kuanzia na jambo hili na mengine tunaweza kuweka wazi sababu ya hivi sasa kuteua mwelekeo huu wa Fatwa kama ifuatavyo:

Mwelekeo huu upo nje ya mtungo wa Fiqhi ya zamani na wala haupingani nao, nao ni matawi ya madhehebu ya Imamu Shafi – kama dalili ilivyoelezewa – hivyo msemaji wa haya miongoni mwa Wanachuoni wa Umma atakuwa amesema si kauli ya kubuni wala kupingana na maandiko.

Mwelekeo huu ndio wenye kufikia zaidi makusudio ya Sharia, hiyo ni kwa sababu Fatwa yake ina fikia makusudio ya Sharia ya kulinda kizazi na kusimamia familia, na haya ni maslahi ya wazi yanapaswa kuangaliwa katika wakati ambao kulinda familia kumekuwa ni jambo muhimu mno, “Mufti anatoa Fatwa kwa yale yenye maslahi kwake”([54]).

Mufti wa zamani Sheikh Abdul Majiid Saliim - Mungu Amrehemu - amesema: “Mwenye kufuatilia yale Wanachuoni wa sasa waliyotofautiana na Wanachuoni wa zamani atafahamu kuwa waliyotofautiana nayo yamejengeka sana katika kuondoa uharibifu ambao unaendana na kauli za waliotangulia, wanaona kuwa wao wamezuia yale waliyopitisha watangulizi miongoni mwa ukodishaji wa mali ya wakfu kwa muda mrefu, ikiwa ni kuzuia ubaya wa madai ya mwenye kukodi kumiliki alichokodi, na wamezuia elimu ya kadhi kuwa ndiyo njia ya hilo pia .. na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale waliyotofautiana Wanachuoni wa sasa na wale wa zamani, na lau isingiekuwa hofu ya kurefusha basi tungetaja mengi katika masuala haya, na tungetaja kauli dhaifu walizozipa nguvu na kuzifanyia kazi kupinga uletaji masilahi au kuondoa uharibifu.

Kwa ajili hiyo baadhi ya Wanachuoni wa Abu Hanifa walisema: Mufti hapaswi kuwa na uelewa finyu katika maana ya wazi iliyopokewa kwenye nukuu pasi na kuchunga wakati na watu wake, na kinyume na hivyo atapoteza haki nyingi, na madhara yake yanakuwa ni makubwa zaidi ya manufaa.

Wakasema: Mufti hutoa Fatwa kwa maslahi yanayotokea kwake .. na yasiyokuwa hayo miongoni mwa maelezo ambayo yanaonesha kuwa kilichowajibu ni kuchunga na kuangalia matukio maalumu ili kufikia lengo hili, na wala haliwi hili kwao ni kwa sababu kauli za Wanachuoni zinapaswa kufahamika kwenye usahihi wake ambao unachunga uletaji wa masilahi au kundoa uovu, kwani ujenzi wa Sharia Takatifu upo kwenye hekima na masilahi ya waja duniani na Akhera([55]).

Hakuna shaka kuwa masilahi ndiyo hali ya kubaki mke na kubaki familia ndani ya wakati fikra nyingi na hali za ulimwengu zinatishia kuendelea kubaki familia na mwanadamu kuelekea kwenye maisha ya upweke.

Hilo kulitolea fatwa kunahitaji tahadhari.

Ambapo tahadhari katika masuala ya ndoa inahitaji kubaki kwenye ndoa, kwani wameelezea hili idadi kubwa ya watu wa elimu miongoni mwao Al-Jamal Al-Qasimy ambapo ametunga kitabu cheke cha “Al-Istiinaas litaswhiih Ankihati N-naas” na katika aliyoyasema humo: “Kanuni na asili ya hukumu za talaka ni aliyoyaelezea Imamu Ibn Hazm na kunukuliwa na Imamu Ibn Qayyim kuwa, ndoa yakini haiendelei isipokuwa kwa yakini, mfano wake ni kama Kitabu cha Sunna na makubaliano yakini ya Wanachuoni, mtu akipata moja ya haya matatu hukumu ya ndoa huondoka, na wala hakuna njia ya kuondoa kinyume na hivyo, hilo kwa sababu ndoa inapaswa kufanyiwa tahadhari, kwa maana jambo la lazima ni wanandoa kubaki na yakini ya ndoa ambayo Mwenyezi Mungu ameita makubaliano ya ndoa, mpaka iondoke kwa yakini.

Ni namna gani mtu anafanya haramu ya ndoa kwa yule aliyekuwa halali kwake kwa yakini na kuhalalisha kwa mwingine si yakini? Imamu Ahmad amezungumzia tahadhari hii katika talaka ya mtu aliyelewa, katika yale yasiyopelekea talaka – kwa maana talaka haiwi – ameleta jambo moja, na linalopelekea talaka ameleta mambo mawili: ameharamishiwa yeye na kuhalalishwa kwa mwengine([56]).

Kisha wepesi kwa watu na huruma kwao ni msingi ambao haupaswi kuondolewa kwa mtazamo wa Mufti, kilichokuwa chepesi zaidi kwa watu basi kukitolea Fatwa ni bora zaidi, na kutoa Fatwa kwenye wepesi huu kwa hali ya watu wa familia hasa mwanamke ambaye anaweza kupoteza familia kwa talaka, na watoto pia wanaweza kutokewa na matatizo ya kisaikolojia na kijamii kutokana na talaka.

Ibn Shaatw amenukuu katika kitabu chake tafauti za Al-Qurafi kwa kauli yake: Wametofautiana katika maana ya halali ikasemwa: Halali ni kile kisichofahamika kuwa haramu, na ikasemwa tena: Halali ni kile kilichofahamika asili yake, maana ya kwanza ni nyepesi zaidi kwa watu na hasa katika zama hizi, baadhi ya Maimamu wamesema: Katika zama hizi mwenye kuchukua kiasi cha mahitaji ya yake na familia yake pasi na kufanya ubadhilifu wala kuongeza zaidi ya mahitaji yake atakuwa hajala haramu wala shaka juu ya haramu([57]). 

Angalia ni namna gani katika mlango huu kauli ya kile kilichochepesi zaidi kinapewa nguvu, vilevile na sisi tunatanguliza zaidi hilo, wala haisemwi kuwa sisi katika hilo inapaswa uangalizi zaidi kwa sababu ni lazima kuchukua tahadhari kwenye ndoa, kwani kinachopelekea tahadhari katika mlango huu ni kuendelea ndoa na kutopatikana talaka, kama ilivyoelezwa kwenye maelezo ya Al-Jamal Al-Qaasimi.

Kauli hii kuendana na zama zetu:

Kama vile mwelekeo huu ndo mwepesi zaidi kubadilisha hali za watu wa wakati huu za kudharau kwa kutamka matamshi ya talaka pasi na kuangalia yanayoendana na Sharia, mazoea na wakati vinazingatiwa moja kwa moja katika Fatwa.

Ibn Aabideen anasema: Wamesema katika masharti ya Ijtihadi kuwa: Ni lazima katika Ijtihadi kufahamu desturi za watu, kwani hukumu nyingi hutofautiana kwa kutofautiana wakati kwa kubadilika desturi za watu wake au kutokea jambo la dharura au uovu wa watu wa wakati ambapo hukumu ikiwa itabakia kama ilivyokuwa mara ya kwanza basi kutapelekea matatizo na madhara kwa watu na kwenda kinyume na kanuni za Sharia zilizojengwa kwa msingi wa wepesi na kuondoa madhara na uovu ili ulimwengu ubakie kwenye mfumo timilifu na hukumu bora, kwenye hili Masheikh wa madhehebu wamekwenda kinyume na yaliyoelezwa na mwanajtihada katika maeneo mengi aliyofanyia Ijtihada katika zama zake kwa ujuzi wao kuwa lau ingekuwa katika zama zao wangesema yale waliyoyasema wakichukua kanuni ya madhehebu yao([58]).

Ni namna gani na sisi hatukokinyume na kauli za Ijitahada katika madhehebu ya Imamu Shafi? Bali katika madhehebu haya tumepata yanayokidhi zaidi mahitaji na maandiko yanayoendana sana.

Al-Qurafi amesema: Kupitisha hukumu kutokana na mazoea kisha mazoea hayo yakabadilika kunakwenda kinyume na makubaliano ya Wanachuoni na ujinga katika dini, bali kila yaliyopo kwenye Sharia ambayo hukumu zake zinafuata mazoea yatabadilika wakati wa kubadilika kwa mazoea na desturi na kufuata desturi mpya, hili si katika Ijitihada mpaka iwe sharti mtu kufaa kufanya Ijitihada, bali kanuni hii Wanachuoni wamefanya Ijtihada na kukubaliana kwenye hilo, hivyo sisi tunawafuata kwenye hilo pasi na kuleta Ijitihada mpya([59]).

UTAFITI WA SITA

Jumla ya pingamizi na majibu yake

Katika utafiti huu tunataja jumla ya pingamizi tulizozisikia baadhi yake kwa wale walioangalia na kupitia mwelekeo wetu katika masuala haya, na sisi tukatoa mchango wetu kwa pingamizi zingine zinazoweza kututokea, tumejibu pingamizi zote kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa nguvu zake, pingamizi hizo ni kama zifuatazo:

Pingamizi la Kwanza:

Kuenea tamko katika talaka na kufanya ni tamko la wazi, na kuenea nchini Misri tamko la “Twaalii” kwa herufi ya Hamza katika talaka, hufanya kuwa ni tamko la wazi na wala si tamko la fumbo kama wanavyoelezea.

Jibu:

Tumesema: Kulifanya neno maarufu kunalazimisha kuwa neno la wazi katika talaka tofauti pande tatu zilizoelezewa katika Fiqhi ya Imamu Shafii, Imamu An-Nawawi amesema: “Pindi tamko la talaka likapata umaarufu tofauti na matamshi matatu ni tamko la wazi…..”.

Katika kitabu cha Tuhafa, tamko la wazi lina sura:

Sura ya Kwanza: Iliyosahihi zaidi, ni kufikiwa kufahamika na kutumika sana, na kwa maelezo haya Al-Baghwi amemaliza, na kwa hivyo Fatwa ya Al-Qafal na Al-Qadhi Hussein na wengine zinafanya kazi.

Sura ya Pili: Hapana, na kupewa nguvu zaidi na Al-Mutawalli.

Sura ya Tatu: Imeelezewa na Imamu kutoka kwa Al-Qafal: Kuwa mwenye kunuia kitu chengine miongoni mwa chakula na vyingine, hakuna talaka, ikiwa atadai, ataaminiwa, na kama hajanuia chochote ikiwa ni mwenye ujuzi wa Sharia anafahamu kuwa fumbo halifanyiwi kazi isipokuwa kwa kuambatanishwa na nia, kinyume na hivyo hakuna talaka, ikiwa hajui Sharia tutamuuliza kile anachofahamu pindi anaposikia kwa mwengine, ikiwa atasema: Ninafahamu kuwa ni talaka, atabebeshwa na kile anachofahamu, na kile alichokielezea Al-Mutawally kutoka kwa Al-Qafal ni kuwa: Ikiwa atanuia si mke basi itakuwa hivyo, na kama hajanuia hivyo hakuna talaka kwa kawaida.

Nikasema – Maelezo ya An-Nawawi – ndiyo sahihi zaidi ambayo yamepitishwa na watu wa Iraq na waliotangulia, kuwa ni fumbo moja kwa moja.

Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi([60]).

Na haya ndiyo yanayofahamika katika maelezo ya Al-Khirqy tofauti na Imamu Ahmad – katika uwazi wa maneno yake – na Imamu Malik, Ibn Qudama amesema katika maelezo yake kuhusu mafumbo ambayo yamekuwa maarufu kwa watu katika talaka: “Yanafahamika maelezo ya Al-Khirqy kuwa hakuna talaka isipokuwa kwa nia, kwa kauli yake: Ikiwa atakuja na tamko la wazi la talaka basi talaka hiyo itakuwa ni sahihi ikiwa amenunia au hata kama hajanuia, maana yake ni kuwa tamko lisilo la wazi halipelekei talaka isipokuwa kwa nia, kwa sababu hili ni tamko la fumbo hivyo haijathibiti hukumu yake pasi na kuwepo nia kama vile maneno mengine ya mafumbo([61]).

Ameulizwa Imamu Ar-Ramly katika watu wa madhehebu ya Imamu Shafii kuhusu matamshi katika talaka kwa watu wa Dhayyar nchini India na kwa lugha yao na wala si tafasiri ya talaka bali ni matamshi yaliyo maarufu kwenye lugha yao wakati wa kutoa talaka, na umaarufu wa matamshi haya kwao ni zaidi katika talaka je yanazingatiwa ni katika matamshi ya talaka au hapana? Ikiwa mtasema: Ndiyo, je ni maneno ya fumbo au ya wazi? Na katika kutoa talaka kwa watu wa mji huu kwa tamko la talaka pamoja na kutofahamu kwao maana yake na upeo wa maarifa yao ni maneno ya kutengana kati ya mume na mke, je hutoka kwa talaka kwa maneno haya au hapana?

Akajibu: Maneno yaliyotajwa sio maneno ya wazi katika kuacha, kisha ikiwa yatachukuliwa ni talaka basi hayo ni maneno ya fumbo, na kama si talaka basi ni fumbo na tamko la talaka katika yaliyotajwa linakuwa ni ya wazi([62]).

Imekuja katika kitabu chake cha Asnaa Al-Matwaalib – maelezo ya kubadilisha tamko “Twaaliq” kwa tamko la “Taaliq” yenyewe ni maudhui isiyo ya talaka – “Ikiwa ni maarufu katika maana ya talaka inakuwa ni fumbo kama vile neno, Halali ya Mwenyezi Mungu kwangu haramu, na mfano wake, akajibu kuwa: Matamshi yaliyotajwa ni fumbo katika talaka hivyo haipatikani talaka kwa matamshi hayo isipokuwa kwa nia([63]).

Katika maelezo yaliyotangulia imekuwa wazi kuwa kiasi cha tamko kufahamika katika talaka haliwezi kutoka kuwa kwake ni katika mafumbo maadamu si katika uwazi wake.

Kigezo: Tamko linakuwa maarufu – katika nchi au jamii – linatumika katika talaka, na tamko hili limekuwa maarufu katika lugha ya jamii, lenyewe ni fumbo kwa upande wao kwa mtazamo wa Imamu An-Nawawi, na tamko la wazi kwa mtazamo wa Imamu Raafii, ama kwa upande wa wengine miongoni mwa Wanachuoni na jamii ya watu wa mji, neno hilo kama si maarufu katika lugha yao basi litakuwa ni fumbo, wala haiji kauli ya kusema ni tamko la wazi.

Ikiwa muangaliaji ataangalia kuwa Wanachuoni hawakuelezea juu ya tamko hili katika vitabu vyao, tumesema: Wanachuoni hawakuelezea kwa kina maneno yote ya mafumbo, bali wametaja kwa jumla kisha wakaelezea yale wasiyoyataja([64]).

Imamu Khatib Sharbiiny amenukuu kutoka kwa Imamu Abu Qaasim Raafii kauli yake katika maneno ya talaka za mafumbo kuwa “Yenyewe ni mengi”([65]). 

Ikiwa Wanachuoni wahakuelezea maneno yote ya mafumbo – kama alivyoeleza Imamu Assuyuti na kunukuliwa na Imamu Khatib kutoka kwa Raafii – ikiwa maneno ya mafumbo ndiyo matamshi ambayo si maudhui kabisa ya talaka ya wazi, basi neno “Twaalii” ni katika maneno yanayotokana moja kwa moja na maneno ya mafumbo yaliyotajwa.

Pingamizi la Pili:

Hivi sasa hakuna yoyote katika wanaotamka neno “Twaalii” linalotumika kwenye lugha ya watu wa Misri isipokuwa mtamkaji anajua kuwa lenyewe lina maanisha talaka, na hii ni dalili kuwa pindi linapotamkwa lenyewe lina maanisha kutokea talaka, ikiwa tutachukuliwa kuwa kuna mtu hakusudii hivyo basi mtu kama huyo ni wachache sana hakuna hukumu yoyote.

Jibu:

Hatupitishi moja kwa moja kuwa kila mwenye kutamka neno “Twaalii” ni mwenye kukusudia kutoka talaka, na madai haya kwa sura hii ni madai holela, tumechunguza matukio mengi kwa miaka mingi tumegundua kuwa asilimia kubwa, bali sema wengi zaidi wanaotamia tamko hili wakiwaambaia wake zao wanakusudia kuwatishia au kuwakemea au kumnyamazisha, wala hawakusudii talaka inayobeba maana ya kuvunja mahusiano ya ndoa, na wala nia haikutani kwa kutamka tamko hili kwenye hali hizo ambazo tumezifanyia uchunguzi kwa kukili wahusika wenyewe.

Ikiwa msemaji atasema: Hawa waliotajwa wamefanya hivyo ili kuachana na vitendo vyao ili kubakia kwenye mahusiano ya ndoa.

Tumesema: Hii ni dhana mbaya kwa Waislamu na tuhuma batili pasi na ushahidi wala dalili, na Mwenyezi Mungu Amesema: {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi} Al-Hujraat: 12, katika hili Waumini wamekatazwa kudhani sana, nayo ni kutuhumu na kufanya hiyana kwa ndugu watu wa karibu na watu wengine pasipo sehemu yake, kwa sababu baadhi ya hizo dhana zinakuwa ni dhambi moja kwa moja, hivyo huepukwa dhana nyingi katika hizo kwa tahadhari([66]).

Katika Hadithi Takatifu kutoka kwa Abu Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Jihadharini na dhana kwani kudhani ni katika uongo wa maneno”([67]). Ikiwa tutakubali ujumla wa maana ya tamko la maana ya talaka basi hili halitalazimisha kuwa kila mwenye kulitamka nia yake na makusudio yake ni kutoa talaka, kwa dalili ya hali tuliyoielezea.

Na inafikirika pia hili kufanywa na Msomi anajua hukumu ya kuwa tamko: “Twaalii” ni fumbo, na analisema kumuambia mke wake akiwa mwenye kukusudia kumtisha na kumnyoosha kama atakuwa hayuko sawa pasi na kukusudia kumuacha.

Kwa hali hiyo, madai ya kuwa watu wengi wanakusudia talaka wakati wa kutamka neno “Twaalii” na asiyekusudia talaka ni wachache ambao huwezi kutoa hukumu ni madai yanayojibika yasiyozingatiwa.

Na kama tutakubali basi masuala yatakuwa yanajibika kwa kanuni: “Kugongana asili na wingi” na kigezo hapo ni kuwa wengi wanapewa nafasi zaidi ya asili ikiwa wengi hao wana sababu yenye nguvu, ama ikiwa yanayopinga asili dalili yake ni dhaifu, basi hapo hupewa nafasi zaidi asili([68]).

Hapa asili katika masuala yetu ni kutokusudia, na uwingi unaodaiwa ni kukusudia, na uwingi huu unaodaiwa haupo nje ya kuwa ibara ya uwezekano usiofungamana na uhalisia au utafiti, au wenye uwezekano wa kuwa na sababu dhaifu, wala haupewi nguvu ya kubadilisha kuendana na asili.

Pingamizi la Tatu:

Kauli hii haifahamiki kwa Wanachuoni wa zamani na hata wa sasa.

Jibu:

Hiyari hii ambayo tumeipitisha kuhusu masuala sehemu ya tafiti hata kama hakuna tamko katika vitabu vilivyotangulia isipokuwa sisi tumekuta maelezo katika vitabu vya sasa vya madhehebu ya Imamu Shafi yanayounga mkono na kuyakubali, na sababu kati ya maelezo yetu na maelezo haya ni moja.

Mwisho Fatwa inafungamana na uhalisia, nao si hukumu ya Kisharia, bali ni mkusanyiko kati ya hukumu ya Kisharia na sura halisi inayohusiana na hukumu hii kwenye akili ya mwenye kufanya Ijitihada au Mufti na kuzalisha Fatwa, hivyo hukumu si Fatwa bali ni moja ya vipengele vyake, nayo ni nidhamu isiyobadilika, fatwa hubadilika kwa kubadilika yanayoendana na hukumu nayo ni hali halisi pindi inapobadilika pande katika pande zake nne: Wakati, sehemu, watu na hali, utakuta mambo hayakuwepo katika zama za mwanzo, kisha yakawa katika zama zilizofuata, kama vile hali hiyo ipo kwenye kadhia nyingi za Fiqhi ya Kiislamu, hii inakuwa kwa kubadilika hali katika miji mbalimbali, na hali hizi zinafahamika, na kuwa maelezo haya hayakutajwa kwenye vitabu vya Fiqhi sio hoja ya kukataliwa kwake, ambapo zinafungamana na mazoea yaliyopo hivi sasa katika maneno ya watu, Ibn Shaatw Al-Maaliki amesema katika kitabu chake juu ya tofauti za Al-Qurafa: “Ulazima wa kubadilika fatwa wakati wa kubadilika mazoea sahihi”([69]).

Mwanachuoni Muhammad Amin maarufu kwa jina la Ibn Aabidiin amesema: “Kuganda kwa fatwa au Qadhi kwenye uwazi wa nukuu na kuacha mazoea na kutojua hali za watu kunapelekea kupoteza haki nyingi na kudhulumu tabia za wengi”([70]).

Na akasema: “Fahamu kuwa hukumu nyingi ambazo zimeelezewa na mwana Ijitihada mwenye madhehebu kutokana na yaliyokuwa katika mazoea yake na wakati wake yamebadilika kwa kubadilika wakati kwa sababu ya uovu wa watu wa wakati husika au kuenea kwa dharura”([71]).

Na maelezo mengi yenye tofauti kati ya Abu Hanifa na watu wake wakielezea Maimamu wa Abu Hanifa tofauti kuwa: “Tofauti ni zama na wakati na wala si tofauti ya hukumu na ufafanuzi”([72]).

Pindi alipoulizwa Imamu Al-Qurafi kuhusu hukumu zilizoandikwa katika madhehebu za Wanaijtihada zinazohusiana na kawaida na mazoea ambayo yalikuwepo wakati wa kupitishwa na Wanachuoni hukumu hizi, je hizi kawaida ikiwa zitabadilika na kuwa zinaonesha kinyume na ilivyokuwa hapo mwanzo, je hizi fatwa zitabadilika na kutolewa fatwa zinazoendana na mila na desturi mpya au zitatoka fatwa zilizoandikwa kwenye vitabu pasi na kuzingatiwa mapya?

Akajibu kwa kusema: “Kupitisha hukumu ambazo zimezoeleka kisha kubadilika kwa hayo mazoea kunakwenda kinyume na makubaliano ya Wanachuoni na ni ujinga katika dini, bali kila yaliyopo kwenye Sharia hukumu zake zinafuata mazoea yatabadilika wakati wa kubadilika kwa desturi na kufuata desturi mpya….bali wala haiwekewi sharti la mabadiliko ya desturi, bali ikiwa sisi tutatoka katika hiyo nchi na kwenda nchi nyengine desturi yao ipo tofauti na desturi na nchi ambayo tulikuwa humo tutawapa fatwa kwa mujibu wa desturi zao, na wala hatutazingatia desturi za nchi tuliyopo, vilevile ikiwa atakuja kwetu mtu kutoka nchi ambayo desturi yake ipo kinyume na desturi tuliyonayo hatutatoa Fatwa isipokuwa kwa desturi yake pasi na kuangalia desturi ya nchi yetu”([73]).

Na Ibn Qayyim akasema katika kitabu cha Iilaami Al-Muwaqqiin: “Wala hawezi Mufti wa Kiongozi kutoa Fatwa na hukumu kwa haki isipokuwa kwa aina mbili za ufahamu, aina ya kwanza: Kufahamu hali halisi na kutohoa elimu ya kweli ya yanayotokea kwa dalili na alama ili awe na elimu nayo, aina ya pili: Kufahamu wajibu katika uhalisia, nao ni kufahamu hukumu za Mwenyezi Mungu ambazo amehukumu ndani ya Kitabu chake au kupitia kauli za Mtume wake katika uhalisia huo, kisha anafanyia kazi aina moja wapo kwa nyengine, mwenye kufanya juhudi na kutumia muda wake mwingi katika hayo hatokosa malipo ya aina mbili au aina moja, kwani Msomi ni mwenye kufikia maarifa halisi kuyaelewa na kufikia hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake”([74]).

  Pingamizi la Nne:

Kauli hii haijatolewa Fatwa na yeyote miongoni mwa wale tuliowakuta na kushuhudiwa kwao elimu na ucha-Mungu, miongoni mwao wapo Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafi, je walipitwa na haya, au waliyafahamu lakini hawakuyazugumza?

Jibu:

Mwanachuoni ambaye hakutoa fatwa kwa kauli hii hawezi kuwa nje ya moja ya mambo matatu:

Ima madhehebu yake anayoyafuata kuwa yameelezea tofauti na hilo, hapo atakuwa anafuata madhehebu yake na wala hayapingi wala kuyapinga kwetu, ambapo kanuni inasema hakuna anayepinga madhehebu juu ya madhehebu([75]).

Ima kuwa miongoni mwa asiyefuata madhehebu yoyote, na ukampeleka mtazamo wake na Ijtihadi yake tofauti na hilo, au amepitwa na ufahamu wa masuala, na sisi hatujadai masuala kukubalika na Wanachuoni wote.

Ima kuwa ni katika Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafii, na makubaliano katika madhehebu haya ni kuwa hilo halijawa mbali bali ni uwezekano tu, huenda umejengewa kwa ushahidi wa kuonekana sehemu au upungufu wa kusoma au ufahamu batili, na Mufti ambaye anafanya uhakiki katika kutokea talaka humuuliza maswali mengi mwenye kutaka fatwa kisha humjibu, na mwenye kutaka fatwa kwa Wasomi hafahamu maana ya kila swali analoulizwa, kwa maelezo hayo moja kwa moja hilo halijatokea kwa uwezekano tu, wala mtu hawezi kutoa hukumu ya moja kwa moja tu, na ikiwa imethibiti kuwa mmoja wa Mamufti wanaonasibishwa na Imamu Shafi ameipitia maana hii kisha akaikataa basi huenda atakuwa hajapima yale anayouliza miongoni mwa matukio mapya yaliyotamkwa.

Na maelezo ambayo tumeyataja katika vitabu vya Imamu Shafi katika kuthibitisha mwelekeo huu katika Fiqhi ya Imamu Shafii, hata kama hayajaenea sana kati yetu kwa sababu yoyote, kwani ni mara ngapi huachwa la kwanza kwa ajili ya la mwisho.

Pingamizi la Tano:

Kauli hii inachukiza kuingia katika Sharia na Dini.

Jibu:

Jambo halipo hivyo, maana ya kuchukiza katika Fatwa ni: Mufti kufanya haraka kutoa Fatwa pasi na mtazamo, au pasi na kuwa na vyanzo, au kufanya haraka kutoa Fatwa kwa utashi wa nafsi yake, tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kudondokea kwenye moja ya tahadhari hizo, lakini Fatwa baada ya kukusanya dalili na mtazamo katika makusudio ni katika mlango wa Ijtihada yenye malipo kwa mfanizi wake.

Ibn Salah amesema: “Haifai kwa Mufti kufanya haraka kutoa fatwa, na mwenye kufahamika hivyo haifai kwake kutoa Fatwa, na hilo linaweza kuwa ni kwa kutothibitisha na kufanya haraka kutoa Fatwa kabla ya kukamilika haki yake ya kuangalia na kufikiri, huenda anabebwa na hilo kwa dhana yake kuwa kufanya haraka ni werevu na utaratibu ni kushindwa na mapungufu, huo ni ujinga, ikiwa atafanya taratibu bila ya kukosea ni ukamilifu zaidi kwake kuliko kufanya haraka akakosea na kupotosha, akiwa na maarifa ya kile anachoulizwa basi kufanya haraka kujibu wakati wa kuulizwa hakuna ubaya kwake, na mfano wake anabeba yaliyopokewa kutoka kwa Maimamu waliotangulia, na inaweza kuwa uharaka wake ukabebwa na malengo maovu ya kufuata kilichokatazwa au kuchukiza na kushikamana na vyenye kuleta shaka ili kumpatia ruhusa mwenye kutaka manufaa yake au kumfanyia uzito mwenye kutaka kumdhuru, na mwenye kufanya hivyo anakuwa ameidharaulisha dini yake”([76]).

Pingamizi la Sita:

Lengo la hiyari hii likiwa ni kuwafanyia watu wepesi, je mmechukua wepesi kwa wengine katika mlango wa talaka?

Jibu:

Hili si pingamizi la kweli kwenye masuala hayo hayo bali ni alama ya mfumo kama anavyoona mpingaji na wala si kama ilivyo kwenye uhalisia wa jambo hilo, na hata katika ufunuo ni kuwa msukumo wa kutoa fatwa ni utashi wa kuwepesisha wala hailazimu hilo kuwa linatokea katika kila masuala miongoni mwa masuala ya talaka, kwa sababu utashi wa kufanya wepesi unaweza kupingana na kilicho na nguvu zaidi katika masilahi kwa upande mmoja na katika uovu kwa upande mwengine, kipimo cha fatwa si kufanya wepesi tu kwa kufuata mitazamo na madhehebu yaliyoruhusu kila masuala([77]).

Na kuteua Fatwa kuna sababu nyingi miongoni mwake:

Iwe sababu ya kuteua kwake ni anaipa nguvu rai ya Mufti na jitihada yake akiwa ni katika wa Ijtahada, na kufanyia kazi kauli yenye nguvu ni jambo la lazima([78]), au iwe fatwa yenye nguvu katika madhehebu yake ikiwa Mufti ahajafikia kiwango cha kufaa kufanya Ijtihada([79]).

Dalili kutosheleza hivyo Mufti ataelekea kwenye Fatwa ili nyepesi zaidi, na katika Hadithi Mtume S.A.W. amesema: “Hakuwa kupewa hiyari katika mambo mawili, moja lake likawa jepesi zaidi kuliko lengine isipokuwa aliteuwa jepesi lao maadamu halina dhambi”([80]). Ibn Abdulbarr amesema: “Anapaswa kuacha yaliyomagumu katika mambo ya dunia na Akhera, na kuelekea siku zote kwenye wepesi, na katika maana ya kuitumia ruhusa ya Mwenyezi Mungu na ruhusa ya Mtume wake S.A.W. pamoja na ruhusa ya Wanachuoni pindipo kauli itakapokuwa haina kosa la wazi”([81]). Maana hii imeelezwa na Wanachuoni wengi waliotangulia, Imamu Yahya Ibn Salaam amesema: “Inapaswa Mwanachuoni kuwabebesha watu ruhusa maadamu hana hofu ya dhambi”([82]). Na Muumar amesema: “Hakika elimu ni kusikiliza ruhusa kwa watu wanaokubalika, ama misimamo ya kielimu hupendwa na kila mtu”([83]). Sufyan At-Thawry amesema: “Elimu kwetu ni ruhusa kutoka kwa Wasomi wenye kuaminika, ama misimamo ya kielimu inapendwa na kila mmoja”([84]).

Awe ni mwenye kuendana zaidi na hali mtaka Fatwa kwa upande wa maslahi na maovu([85]).

Iwe sababu ya kutoa Fatwa kauli ya matatizo ya wengi, bali Wanachuoni wamepitisha kuwa mwanadamu anaweza kufuata madhehebu mapesi kwake katika hali ya matatizo na dharura au wasi wasi wa kuangukia kwenye haramu, kana kwamba kuna maeneo mawili, eneo la kwanza: Ni eneo liloharamu kabasa, na eneo la pili: Ni eneo haramu kwa kudhaniwa ambalo linaweza kuvuta mitazamo ya Wanachuoni ya kuwepo dhana katika dalili ya uharamu ni sawa sawa kwa upande upokezi au dalili, na eneo lengine ni kadhia ya maneno yetu, kadhia ya uharamu kwa upande wa mwenye kumfuata msemaji wake hauzingatiwi kuwa upande wa dhana, na dhana hii inakabiliana na dhana nyengine katika kauli ya kufaa, hivyo kauli imekuja ya kupitisha ufuasi wa rai na matazamo wa mwanajitihada anayesema inafaa, kwa sababu kufuata hakuzingatiwi kuwa mtu amehama kutoka kwenye dhana kwenda kwenye dhana, na kauli mbili – sawa sawa inayoharamisha au kuhalalisha – zipo chini ya mwanvuli wa Sharia hakuna moja wapo inakuwa nje ya Sharia, wala haiwezekani kwa yoyote kupitisha moja kwa moja kuwa kauli moja wapo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenye jambo hilo hilo.

Imekuja katika matini ya Abu Shujaa na sherehe yake ya Ibn Qaasim Al-Ghazi: “Haifahi pasipo kuwa na umuhimu mwanamume au mwanamke kutumia kitu chombo katika vyombo vya madini ya dhahabu au madini ya fedha si katika kulia chakula au kunywea au kwa matumizi mengine”.

Sheikh Al-Islaam Ibrahim Al-Baijuuri amesema: “Kwa upande wa Imamu Abu Hanifa kuna hukumu ya kufaa kwenye dharura ngumu, pamoja na kuwa kauli iliyopitishwa kwao ni haramu, hivyo inapaswa kwa mwenye kutumia chombo kama hiko kama inavyotokea kwa wengi kutumia ili kumalizana na haramu”([86]).

Hapa inapaswa kutahadharisha mambo yafuatayo:

Jambo la Kwanza: Kauli yetu ya kufaa kufuata kilicho halali haina maana kuwa sisi tunapitisha na kuruhusu kwa mtu yeyote kuwa nje ya Sharia, bali makusudio ya maelezo haya ni kusahihisha vitendo vya wat una mashirikiano yao kadiri iwezekanavyo, kwa kuwa mtu kufanya kitendo chenye sura ya kufaa Kisharia ni bora kwake kuliko kufungwa mbele yake milango yote bila ya kukuta mbele yake njia isipokuwa ni kuvamia yaliyoharamu, na alikuwa anasifika kwa kufuata waliopitisha.

Jambo la Pili: Kauli ya Mwanachuoni Al-Baijuri: “Inapaswa kwa mwenye kutumia chombo….” Neno inapaswa maana yake ni kutakiwa na wajibu kwa lugha ya istiari([87]), ni kana kwamba kuhama madhehebu iliyonyepesi katika hali iliyotajwa kwa kudhamiria na wala si ruhusa, kwa sababu kutakiwa maana yake ni kukubalika – si lazima – kwenye Sharia, na kutakiwa kuna maanisha kutekeleza na kubeba jambo, [Pia kuongezea kuwa halimtoi kwenye haramu isipokuwa mara nyingi kwa jambo la wajibu au Sunna].

Jambo la Tatu:  Baadhi ya watu wanachukua maandiko ya Mwanachuoni Al-Baijuri na Wanachuoni anaofanana nao kwa nafasi ya kufuatwa pasi na nafasi ya kutoa fatwa si sahihi, kwa sababu kufuata ikiwa mfuataji ni mtu asiyejua basi anazingatiwa kuwa hafahamu kauli za Wanachuoni wala madhehebu yao, wala hafahamu namna ya kuzifikia kauli zao kwa undani kuongezea pia kuzifahamu kwa usahihi, pia kutenganisha yaliyosahihi kuyafuata na yali yasiyosahihi kufuatwa, hivyo lazima kwake kuwa na mtu wa kumuongoza na kumpatia fatwa, kinyume na hivyo itakuwa ni fujo.

Ibn Aabideen amesema katika sherehe ya kitabu cha mfumo wa fatwa ya Mufti baada ya kutaja sehemu ya kauli dhaifu katika madhehebu ya Imamu Abu Hanifa: “Ikiwa Mufti atatoa fatwa kwa kauli hizi katika mambo muhimu ikiwa lengo ni kutafuta wepesi basi inakuwa ni jambo zuri na kwa fatwa hiyo akajua kuwa mtu aliyetanzika atafanyia kazi yeye mwenyewe hiyo fatwa kama tulivyosema, na Mufti anaweza kumtolea fatwa aliyetanzika, katika maelezo yaliyopita kuwa asifanyie kazi kauli dhaifu wala kuzitolea fatwa kunafanya kazi kwa mambo yasiyo ya dharura”([88]).

Pingamizi la Saba:

 Nyinyi mnakosoa Fatwa zisizo za kawadia kisha mnazitumia hizo hizo!

Jibu:

Kauli zisizo za kawaida hazizingatiwi, lakini hukumu za kauli zaisizozingatiwa zina sababu:

Miongoni mwazo: Kauil kuwa tofauti na makubaliano ya Wanachuoni, Imam Zamarkashi amesema kwenye kitabu cha Al-Bahri: “Tofauti ya pili haizingatiwi….na hivi ndivyo watu wa Abu Hanifa wanasema kuhusu tofauti kauli isiyo ya kawaida, ni kuwa haina tofauti wala kutafautiana, katika hilo wanakusudia kuwa tofauti yenye kufahamika iliyokaribu ndiyo yenye kuchukuliwa kuliko tofauti si za kawaida za mbali([89]).

Miongoni pia: Masuala kuwa hayajafahamika kuwa na tofauti, lakini haijadaiwa kukubalika na Wanachuoni, kisha kauli ikaja na kueleza hukumu tofauti na ya mwanzo ambayo haikufahamika kuwepo tofauti, Sheikh Taqiyyudiin Al-Sabaki amesema kwenye maelezo yake ya hukumu ya aliyekinyume na sharti lililopo: “Naye yupo kinyume na yale tuliyojifunza kwenye madhehebu manne, na yale tusiyoyajua kuwa na tofauti basi huyo ni kama aliyekinyume na makubaliano ya Wanachuoni, ikiwa itathibiti kuwepo tofauti basi inakuwa si ya kawaida, na tofauti isiyo ya kawaida haizingatiwi, kama vile uwezekano wa mbali haulitoi andiko kuwa kwake andiko”([90]).

Pia: Kuwa hakuna dalili, na kufanyia kazi yasiyo na dalili kunahitajika udhibiti, ambapo ndani yake kuna kuupa nguvu upande kitendo zaidi ya upande wa kuacha au upande wa kuacha zaidi ya upande wa kitendo bila kigezo kinachozingatiwa, na kuipa nguvu hukumu bila ya kigezo ni jambo lisilokubalika([91]).

Al-Qurafi amesema: “Fatwa bila ya dalili ni batili kwa makubaliano ya Wanachuoni, na haramu kwa msemaji wake na wanaoiamini”([92]).

Miongoni pia: Kauli kuwa inatokana na uelewa dhaifu. Mwanachuoni Al-Qurafi amesema katika kitabu cha Al-Furuuq: “Tofauti isiyo ya kawaida inatokana uelewa dhaifu .. haiondoi tofauti, bali hujipunguzia yenyewe ikiwa itatolewa hukumu kwa Fatwa inayotokana na uelewa”([93]).

Tuliyopitisha katika masuala yetu haya hayaaminiki kabisa kwa sababu ni fatwa isiyo ya kawaida, ikiwa haiendani na mtazamo wa Jamhuri hiyo si kwa kushambulia, kwani asili katika kuteua ni kuwa moja wapo ya madhehebu yanayofuatwa, lau atakuwa kinyume na Jamhuri na mfano wake, haisemwi kuwa si kawaida, na fatwa ambayo sisi tunaielezea tumechukua kauli zinazokubalika katika madhehebu ya Imamu Shafi kama ilivyoelezewa.

Pingamizi la Nane:

 Je! si katika kanuni iliyopitishwa kuwa asili ya ndoa ni tahadhari, basi ni kwa nini hapa haikuchuliwa tahadhari na kutokea talaka?

Jibu:

Tumeashiria jibu kuhusu pingamizi hili na tumesema, kinachopelekea tahadhari katika masuala ya ndoa ni kubakia maisha ya ndoa na wala si kuyamaliza, kwa sababu asili ni kubakia kama ilivyokuwa, na ndoa yakini haiondoki isipokuwa kwa yakini ya mfano wake, na kama sio hivyo basi wanandoa wanabakia kwenye ndoa yakini ambayo Mwenyezi Mungu Ameitaja kama makubaliano ya ndoa, nayo ndiyo aliyoyaelezea Imamu Ahmad ya kutokuwepo talaka ya aliyelewa, akasema katika mapokezi ya Abu Talib: “Ambaye haamrishi talaka atakuwa amekuja na jambo moja, na ambaye anaamrisha talaka atakuwa amekuja na mambo mawili, ameharamisha na kuhalalisha lingine, hili ni bora zaidi ya hili”([94]), hapa vilevile mwenye kutoa talaka atakuwa ameleta mambo haya mawili, na asiyetoa talaka atakuwa hajaleta isipokuwa jambo moja.

Kanuni ya tahadhari katika ndoa yenyewe ni kanuni sahihi isipokuwa yenyewe wakati wa kutekelezwa inaweza kupingana na kanuni nyingine inayopewa nguvu na uzito, kama vile inapokuwa tamko la kilugha linatofautiana na mazoea basi hutangulizwa maana ya iliyozoeleka kuliko maana ya kilugha.

Imamu Ibn Dakik Al-Eid amesema: “Tamko linaponukuliwa kwa maana iliyozoelea kuchukuliwa kwake kunakuwa ni bora zaidi ya kuchukuliwa kwa maana ya kilugha”([95]).

Imekuja katika hashiyatu ya Mwanachuoni Abu Kassim Ibn Shaat kwenye kitabu cha furuuq cha Qurafi: “Ikiwa mtu atasema “Talaka inanilazimu” pasi na kuwa na nia makusudio yake huchukuliwa ni ahadi, na “kanuni ya tahadhari ya ndoa” inapaswa kumlazimisha talaka tatu, kama aliyeacha lakini hafahamu ameacha talaka moja au tatu, hulazimika na talaka matatu kwa tahadhari, na hilo ni kwa vile hukumu ya kilugha na tahadhari ni kumlazimu talaka kwa idadi isiyo hesabika isipokuwa mhalalishaji hakubali zaidi ya tatu, kama akisema: “Anti Taaliq Miata” kwa maana: Wewe umeachika talaka mia moja, analazimika talaka tatu tu, kwa kukosekana kukubalika na mhalalishaji ongezeko juu ya hilo, lakini Wanachuoni wamekwenda kinyume na kanuni hii katika talaka, kama vile wamekwenda kinyume na kanuni ya kukanusha kuthibitisha, na katika kuthbitisha ni kukanusha katika imani kama tofauti zilizoelezewa, kwa sababu muundo wa talaka na imani ni mazoea, na mazoea ni kutumia hilo tamko kwa mwenye kuacha kwa talaka, Ibn Shaat amesema: Si mfahamu yeyote amelazimisha talaka tatu kwa tamko hilo, kwani lenyewe ni mazoea katika talaka([96]).

Pingamizi la Tisa:

Mmesema kuwa masuala haya yameelezewa na baadhi ya Wanachuoni wa hivi karibuni wa madhehebu ya Imamu Shafi, haya sio sahihi, hawakuelezea masuala haya bali wameelezea masuala mengine.

Jibu:

Hawa Wanachuoni wameeleza wazi baadhi ya masuala na wakataja sababu zake, kufahamu sababu na kuleta masuala mapya ni jambo linalokubalika katika Fiqhi, na hukumu huzunguka na sababu zake kuwepo na kutokuwepo kwake([97]), na Mufti anatekeleza nafasi hii katika masuala haya na mengine, hivyo hakuna sababu ya kupinga masuala haya pasi na masuala mengine, ikiwa nafasi ya Mufti itaishia kwenye maandiko tu basi ni nani atakayepambana na masuala mapya ya Umma?

Imamu Al-Qurafi amesema katika kitabu cha Al-Furuuqu: “Usigande kwenye maandiko ndani ya vitabu kwa umri wako wote, bali pindi anapokujia mtu asiye wa mji wako akitaka Fatwa yako basi usimpeleke kwenye mazoea yaliyopo nchini kwako, bali muulize mazoea yaliyopo nchini kwake na mpeleke huko na mtolee fatwa pasi na kutumia mazoea ya nchini kwako na yaliyoandikwa kwenye kitabu chako, huu ndiyo ukweli wa wazi, na kuganda na nukuu siku zote ni upotevu katika dini na ujinga wa makusudio ya Wanachuoni Waislamu na Waja wema waliotangulia”([98]).

Mwisho wa Tafiti

 Matokeo ya mwisho tuliyoyafikia katika utafiti huu ni kuwa: Yale yaliyozoeleka na watu nchini Misri na maeneo mengine katika matamshi ya talaka ya kutamka herufi ya Qaaf Hamza hutoka kwenye tamko la wazi na kuwa fumbo ambalo linahitaji uwepo wa nia ili ipatikane talaka.

Huongezwa kwenye hilo yale yaliyoelezewa kuwa hiyo nia inapaswa kuwa mwanzoni mwa kutamka neno la fumbo, ikiwa atatamka neno la fumbo pasi na nia kisha akanuia baada ya hapo hakuna talaka.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi, na shukrani mwanzo na mwisho ni za kwake

 

([1]) 1/20

([2]) Kitabu cha Burhan 2/485.

([3]) Kitabu cha Qawaatwii Al-Adilla.

([4]) Imekubaliwa na wapokezi wa Hadithi: Kwa Imamu Bukhari Hadithi nambari 6803 kwenye kitabu Al-Iitisam bil Kitabu wa Sunna. Na kwa Imamu Muslim Hadithi nambari 3240 kitabu cha Al-Aqdhia kutoka kwa Amr Ibn Al-As R.A.

([5]) Kamusi ya Maqaayiis Al-Lugha ya Ibn Faris, uhakiki umefanywa Na: Abdulsalaam Harun, mada ni “badala” 1/210.

([6]) Imekubaliwa na watu wa Hadithi: Imepokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha “Talaka” mlango unaozungumzia “Talaka wakati wa kuzama kulewa na hali ya uwendawazimu” Hadithi nambari 4968. Na Imamu Muslim katika kitabu cha Imani mlango wa “Mwenyezi Mungu huondoa mazungumzi ya nafsi na fikra za moyoni” Hadithi nambari 127 ni katika Hadithi za Abu Huraira R.A.

([7]) Kitabu cha Al-Mughny 7/294.

([8]) Angalia kitabu cha: Al-Misbah Al-Munir, uk. 337. Na Muujabu Al-Wasit, uk. 511.

([9]) Muujamu Maqaayiis Lugha 3/347. Na angalia Muujamu Al-Wasit, uk. 511.

([10]) Kitabu cha Al-Bahrul-Muhiitw 3/134.

([11]) Kitabu cha Hashiyatu Al-Atwar Alaa Sherhi Al-Jalai 1’315.

([12]) Kitabu cha Al-Manthuur fii Al-Qawaid 2/310.

([13]) Kitabu cha Hashiyatu Al-Jubairamy Alaa Al-Iqnaai cha Al-Khatib 3/488.

([14]) Angalia kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj 4/468.

([15]) Wanachuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa wanaona kuwa matamshi mawili kuwa huru na kutenganisha ni katika jumla ya maneno ya fumbo pia, hivyo hakuna talaka kwa maneno hayo isipokuwa kukiwa na nia, yamekuja hayo katika kitabu cha Badaaii As-Sanaaii miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Abu Hanifa 3/106: Watu wetu wamesema. Kauli yake: Nimekuacha huru na nimekutenganisha ni katika maneno ya fumbo haipatikani talaka kwa maneno hayo isipokuwa kwa njia ya nia kama maneno mengine ya fumbo.

([16]) Kitabu cha Al-Manshuur fii Al-Qawaid 2/306.

([17]) Kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhair, uk. 293.

([18]) Uk. 586.

([19]) Kitabu cha Iidhaah fii uluumi al-balagha, uk. 301.

([20]) Kitabu cha Bahrul-Muhiitw 3/134.

([21]) Fumbo kwa Wasomi wa Sharia ni tofauti na watu wa Bayana, kwa sababu hali ya kuwa fumbo kwa upande wa Wanasheria ni tofauti kwa watu wa Bayana, mfano wake: Lau mwanamke atamwambia mume wake: Nimekuzini, jibu la kauli yake: Nimezini? Basi hapo huchukuliwa kuwa mwanamke anamtuhumu mume uzinifu, na huchukuliwa pia mwanamke anataka kusema ikiwa wewe ni mzinifu basi nimekuzini, akini wewe mume wangu, mimi sijazini kama vile wewe hujazini, angalia kitabu cha Mwanachuoni Ibn Qassim Al-Ibady kitabu cha Al-Ghurar Al-Bahiya fii Sherhi Al-Bahja Al-Wardiya cha Sheikh Zakaria Al-Ansar 4/324.

([22]) Kitabu cha Mughny Al-Muhtaj ilaa maarifatil-alfaadh 4/458.

([23]) Hashiyatu Al-Qalyubi alaa Sherhi Al-Muhilly liminhaaji Twaalibiin 3/325.

([24]) Kitabu cha Fat’hul-Maani cha Imamu As-Suyuty 1/204.

([25]) Marejeo yaliyopita 1/207.

([26]) Watu wa Imamu Malik wanagawa maneno ya mafumbo ya talaka sehemu mbili: Mafumbo ya wazi, na mafumbo si ya wazi, fumbo la wazi hutumika katika talaka na kuondoa ugomvi, na kusudio hapa tamko linalotumika si sehemu yake.

Na kichodhibiti katika fumbo la wazi kutokana na maneno yao ni kuwa: Tamko likiwa na maana ya kuondoa tatizo kwa mara moja inayolazimisha talaka tatu bila ya kunuia, na hata kama haita maanisha hivyo bali ika maanisha talaka ya wazi.

Fumbo la wazi kama tala ya wazi halitumiki kwenye talaka isipokuwa kwa sababu inayobeba tamko na si nia, na wala haisimami matumizi yake kwa nia, bali ni kwa kiwango cha makusudio ya kuitamka,

Ama fumbo lisilowazi ni tamko maana zake za talaka zinasimama kwa wepo wa nia kwa mtamkaji.

Angalia kitabu cha: Sherhul-Kabiir alaa mukhtasar Khalil, pamoja na kitabu cha Imamu As-Suyuty cha Sherh As-Saghir alaa Aqrabi Al-Masaalik ilaa masdhehebi Malik, pamoja na Hashiyatu Saawy 2/561.

([27]) Kitabu cha Fawaqih Dawaaya alaa Risalati Ibn Abi Zaidi Al-Qairawany 2/34.

([28]) Kitabu cha Ittihaafu fiimaa yataallaq bil Qaaf kitabu cha kadhi wa Maraakish Wiqas Abi Muhammad Abdillah Ibn Khadhraa.

([29])  Kitabu cha Kawkabu Durry, uk. 480: 481.

([30]) 1/346 kitabu cha Hashiyatul-Jamal.

([31]) Kitabu cha Nihayatul-Muhtaj 1/48.

([32]) Mwanachuoni Al-Jamal amesema katika kitabu chake 1/346: Kusudio la neno Waarabu ni wale wasiotumia lugha fasihi, ama wale mafasihi wa lugha miongoni mwao hawatamki hivyo.

([33]) 1/149.

([34]) 1/133.

([35]) Kitabu cha Al-Haawi cha fat’wa 1/207.

([36]) 6/429.

([37]) 8/4.

([38]) Kitabu cha Al-Bajuuri sherhe ya Ibn Qassim Al-Ghuzai kwenye Matini ya Abi Shujaa 1/133.

([39]) Rejea: Kitabu cha Haafiyatu Ramly alaa Asnaa Al-Matwalib 1/151.

([40]) Rejea kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj cha Khatibu Sharbiny 2/280, na kitabu cha Al-Qalyuuby sherhi ya Minhaaji Twaalibiin cha An-Nawawy 3/325.

([41]) Kitabu cha Nihayatu Al-Qauli Al-Mufiidi fii ilmi Tajwiid cha Sheikh Muhammad Makky Nasri, uk. 61.

([42]) Herufi zinazotoka kwenye ncha ya ulimi ni mbii: Herufi ya Qaaf na Kaaf.

([43]) Marejeo yaliyopita, uk. 32, 34.

([44]_ Kitabu cha Asaa Al-Matwalib sherehe ya Raqdhu Twalib cha Sheikh Zakaria Al-Ansary 3/270.

([45]) Sherehe ya kitabu cha Kawkab Al-Muniir cha Ibn Najjar, uk. 35.

([46]) Kitabu cha Anwaar Al-Buruuq fii Anwaai Al-Furuuq 3/153.

([47]) Sherehe ya Al-Asfahany ya kitabu cha Mukhtasar Ibn Al-Hajib 1/150.

([48]) Kitabu cha Tamhiid fii Takhriiji alaa Al-Usuuli 137: 139.

([49])  Sherehe ya kitabu cha Al-Minhaj cha Qalyubi na Umaira 3/325.

([50]) Al-Manshuur cha Zarkashy 2/371, 374, na ktiabu cha Al-Ash’bah wa An-Nadhwahir cha Imamu As-Suyuty, uk.166, 169

([51]) Na hii haifahamiki kuwa talaka haiwi ya wazi isipokuwa kwa lugha ya Kiarabu itafasiri talaka ya wazi, kwa sababu neno talaka limewekwa kwenye lugha ya kigeni, ikiwa mume atamuambia mke wake kwa mfano: Anti Twaaliq si kwa lugha ya Kiarabu, basi talaka inakuwepo, katika sherehe ya kitabu cha Al-Minhaaj Al-Jalal Al-Mahall amesema: “Tafasiri ya neno talaka kwa lugha ya kigeni inakuwa ni talaka ya wazi kwa mujibu wa madhehebu, kutokana na kufahamika matumizi yake kwa watu kama inavyofahamika katika matumizi ya lugha ya Kiarabu kwa watu wake”.

([52]) Kitabu cha Rawdhatu Twaalibiin 6/32.

([53]) Kitabu cha Al-Mughny cha Ibn Qudama 7/306.

([54]) Kitabu cha Al-Ashbah wa An-Nadhwahir cha Ibn Nujiim Al-Hanafy, 2/338.

([55]) Kitabu cha Fatawa Darul-Iftaai Al-Msria, kwa maana ya Fatwa za Ofisi ya Mufti wa Misri, iliyosajiliwa kwa namba 32, namba ya Fatwa 8.

([56]) Kitabu cha Al-Istiinaas litaswhiih Ankihata Nnaas ukurasa wa 26.

([57]) Kitabu cha Ibn As-Shatwi cha tofauti 4/73.

([58]) Kitabu cha Nashru Al-Urufi fii binaai baadhi Al-Ahkaami alaa Al-Urufi cha Ibn Aabideen 2. 125.

([59]) Kitabu cha Al-Ihkaami fii Tamyiiz Al-Fataawa ani Al-Ahkaami ukurasa wa 218.

([60]) Kitabu cha Rawdhat Taalibiin 6/26.

([61]) Kitabu cha Al-Mughny 7/300.

([62]) Kitabu cha Fat;wa cha Ramli 3/340.

([63]) Kitabu cha Shihaabu Ramly cha Asnaa Al-Mataalib sherhe ya kitabu cha Rawdha Al-Mataalib cha Sheikh Zakaria Al-Ansary 3/270.

([64]) Kitabucha Fat’hu Al-Maghaaliq cha Imamu Assuyuti, 1/205.

([65]) Kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj ilaa maarifati Al-Faadhi, 4/460.

([66]) Tafasiri ya Ibn Kathir, 7/377.

([67]) Imekubaliwa na watu wa Hadithi: Imepokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha Adabu mlango unaokataza kufanya uhasidi, na imepokewa na Imamu Muslim katika kitabu cha wema na undugu pamoja na adabu -  mlango wa uharamu wa dhana na kuchunguza.

([68]) Angalia kitabu cha Al-Mathuuri cha Zarkashy 1/311 – 330, na kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhair cha Suyutwi ukurasa wa 64 – 68.

([69]) Hashiyatu ya Shaat, 3/209

([70]) Kitabu cha Sherhu Mandhuumatu Ukuud cha Ibn Aabidiin 1/ 47.

([71]) Sherhu Mandhuumatu Ukuud cha Ibn Aabidiin 1/44.

([72]) Angalia kwa mfano kitabu cha: Al-Mabsuut cha Sarkhasy 8/178, na kitabu cha Badaai Sanaai 6/31, pia kitabu cha Tabyiin Al-Haqaiq 1/43, kitabu cha Bahru Raiq 4/351.

([73]) Kitabu cha Al-Ihkaam fii tamyiiz Al-Fatawa, uk. 218: 219.

([74]) Kitabu cha Iilaami Al-Muwaqqiin, 1/70.

([75]) Angalia: Kitabu cha Ibn Shaat Al-Maaliki cha tofauti za Al-Qurafi 4/121.

([76]) Kitabu Adabu Al-Mufti wal-Mustafti, uk. 111.

([77]) Kufuata kilichochepesi zaidi katika kila madhehebu hata kama Wanachuoni wengi wameelezea ubaya wake. Zarkashy amesema katika kitabu cha Bahri  8/381, 382: “Lau atateua katika kila madhehebu kilichochepesi zaidi kwake basi katika ufasiki wake una sura mbili: Abu is’haqa Al-Maruuzy amesema: Kuna ufasiki, na Ibn Abu Huraira akasema: Hapana, Al-Hanati ameelezea katika fatwa yake, na Imamu Ahmad akaelezea: Ikiwa mtu amefanyia kazi kauli ya watu wa Kufa katika upandikizaji mbegu, na akafanyia kazi kauli ya watu wa Madina katika kusikia, na akafanyia kazi kauli ya watu wa Makka katika kustarehe anakuwa ni fasiki, na Al-Qadhi katika watu wa Imamu Hanbal akahusisha ufasiki kwa Ijtihada ikiwa jitihada yake haipelekea kuruhusu na ikafuatwa, na kwa mtu asiyefahamu mwenye kujitokeza kwenye jitihada hiyo pasi na kuifuata kwa kukosekana lengo lake ambalo ni kufuata. Ama siyefahamu pindi anapofuata hawi fasiki, kwa sababu amemfuata mtu mwenye kufanya jitihada zake, katika fatwa ya Imamu An-Nawawi ni kuwa haifai kufuata ruhusa, na akasema katika fatwa zake zengine alipoulizwa kuhusu mwenye kufuata madhehebu yake: Je inafaa kwake kufuata yasiyokuwa madhehebu yake katika ruhusa ya dharura na mfano wake? Akajibu: Inafaa kufanyia kazi fatwa ya anayofaa kutoa fatwa pindi anapoulizwa pasi na kupata ruhusa wala kutegemea swali la mwenye kujua kuwa madhehebu yake yameruhusu hilo”.  

Ibn Hajar Al-Haitami amesema katika fatwa yake 4/315: “Kilicho sahihi zaidi ni kuwa – kwa maana: Mtu asiyejua – ana hiyari kumfuata amtakaye hata kama ni mbora kwake pamoja na kuwepo aliyebora zaidi.

([78]) Kitabu cha Jamuu Al-Jawaamii pamoja na sherhu Al-Mahalli na Hashiyatu Al-Atar 2/404.

([79]) Angalia Sherhu Mundhuma Uquudi, ni katika kitabu cha Ibn Aabidiin 1/11-13.

([80]) Imepitishwa na Maimamu wote wa Hadithi: Imepokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha adhabu mlango wa kutekeleza adhabu. Na imepokewa na Imamu Muslim katika kitabu cha mambo bora mlango wa mambo aliyokuwa nayo mbali Mtume S.A.W. yenye dhambi na kumteua kwake Bibi Aisha R.A.

([81]) Ameinukuu Al-Iraaqi katika kitabu cha Tarh Tathriib 7/209, 210.

([82]) Kitabu cha Tamhiid cha Ibn Abdulbarr 8/147, na Yahya Ibn Salaam naye ni Imamu Mwanachuoni Abu Zakaria Al-Basry Muafrika.

([83]) Kitabu cha Tamhiid cha Abdulbarr 8/147,  na kitabu cha Jaamii Bayaan al-Ilmu 1/785. Na Muammar ni Muammar Ibn Raashid Al-Azdi amesema Dhahbi Imamu Al-Hafidh Sheikh Al-Islaam .. alikuwa ni katika Wasomi wenye uelewa mkubwa pamoja na ukweli na upembuzi wa mambo, alifariki mwaka 153A.H., na imesemwa ni mwaka 154 A.H., kitabu cha Sairi Aalaam Al-Balaa 7/7, 14, 15.

([84]) Kitabu cha Jaami Bayaan Al-Ilmi wa Fadhlihi cha Ibn Abdulbarr 1/784, na At-thawri ni Imamu anayefahamika, Adhahabi amesema: “Ni Sheikh Al-Islam Imamu Al-Hafidh, kiongozi wa Wasomi wa wakati wake” amefariki mwaka 261 A.H. kitabu cha Sairi Aalaam An-Nablaa, 7/230, 279.

([85]) Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A. kuwa aliulizwa kuhusu nguo ya muuaji akasema: Hana nguo, akaulizwa na  mwengine akasema: Anayo nguo, kisha akasema: Ama wa kwanza niliona machoni mwake utashi wa muuaji nikamzuia, ama wa pili ameuwa na alikuja kutaka msaada hivyo si kumkatisha tamaa. Kitabu cha Asnaa Al-Matalib, 4/281.

([86]) Hashiyatu Al-Baijuri ya sherehe ya Ibn Qassim kwa matini ya Abu Shujaa, 1/40.

([87]) Hashiyatu Al-Baijuri ya Sharehe ya As-Salam katika mantiki, uk. 30.

([88]) Kitabu cha Sherhu Munduuma Uquud Rasmi Al-Mufti – cha Ibn Aabidiin 1/50.

([89]) Kitabu cha Bahrul-Muhiit, 6/434.

([90]) Kitabu cha Fatawa As-Sabak, 2/19.

([91]) Kitabu cha Tarjiih liswadri Sharia pamoja na sherhi  Talwiih 1/352.

([92]) Kitabu cha Al-Ihkaam fii Tamyiizi Al-Fatawa ani Al-Ahkaam, uk. 225.

([93]) Kitabu cha Al-Furuuq, 4/51.

[94] Kitabu cha Iilaam Al-Muwaqqiin 4/39.

([95]) Kitabu cha Al-Ihkaam Al-Ahkaam, 2/67.

([96]) Hashiyatu Ibn Shaat, 2/106.

([97]) Kitabu cha Mughni Al-Muhtaaj, 3/305.

([98]) Kitabu cha Al-Furuuq, 1/176, 177.

Share this:

Related Fatwas