Baba Humlazimisha Binti Yake Kuvaa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Baba Humlazimisha Binti Yake Kuvaa Hijabu

Question

Je ni wajibu wa wazazi wa kiislamu kuwalazimisha mabinti zao wavae Hijabu? Na ikiwezekana kuwatishia kutowapa matumizi yao iwapo hawatavaa hijabu hiyo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hijabu ni vazi lenye hukumu ya Faradhi kwa mwanamke wa kiislamu aliyebaleghe, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao} [AN NUUR 31].
Na Abu Dawud, Al Baihaqiy na Atwabaraniy wamepokea kutoka kwa Aisha R.A., kwamba Asmaa Bint Abi Bakr R.A. aliingia Mtume S.A.W., Na alikuwa amevaa nguo nyepesi na Mtume S.A.W, akamkwepa, na akasema: "Ewe Asmaa, Hakika mwanamke anapobaleghe na kutokwa hedhi haifai kwake kuonekana sehemu za mwili wake isipokuwa hapa na hapa, akaashiria usoni na katika viganja viwili vya mikono.
Na akiwa ni binti asiye na hijabu basi ni wajibu wa mzazi kumuamrisha aivae hijabu hiyo, na aendelee kumnasihi, bila ya kumdhuru au kumuudhi au hata kutumia maguvu kwa kumlazimisha; kwani jambo hili ni katika ule mlango wa kuamrisha mambo mema na kukataza mambo mabaya. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.} [AAL IMRAAN 104].
Na Muslim amepokea Hadithi kutoka kwa Tamim Bin Aus Adariy kwamba Mtume S.A.W. Alisema: "Dini ni nasaha, mara tatu. Tukasema: Ni kwa nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na Kitabu chake, na Mtume wake, na kwa ajili ya viongozi wa Waumini na watu wote.". Na anaweza kumshinikiza kiasi awezacho, kwa sharti la kutomlazimisha kwa kumpiga au kumdhuru kunakoumiza au kwa kuzuia matumizi au manufaa au vitu vingine vinavyoleta madhara, na kutomlazimisha aache kazi. Asiifanye hiyo kuwa ni sharti kwa ajili ya kuishi maisha yake ya kawada, mpaka isije ikapelekea kuchukia Dini na kuchukia utekelezaji wa hukumu mbali mbali za Dini. Na utenzaji nguvu huu unaweza ukapelekea pia Unafiki na kumpaka mafuta.
Jambo ambalo halilei ndani yake kumchunga Mwenyezi Mungu, nalo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama wamuona, na hili ni moja ya nguzo Tatu ambazo Mtume S.A.W aliulizwa na. Jibrili, katika Hadithi ambayo wanazuoni wa Fiqhi wanaafikiana, kutoka kwa Omar Bin Al Khatwab R.A. Amesema: "Aliulizwa: Ihsani ni nini?: akasema: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama wamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona."
Na kutokana na hayo: Ni wajibu wa mzazi kumnasihi binti yake aivae hijabu hiyo, na hamlazimishi kwa kumpiga au kumdhuru kunakoumiza au kwa kuzuia matumizi au manufaa ya aina yeyote, kwani matumizi yake ni wajibu ikiwa ataendelea kuwa chini ya ulezi wake na wala hana mali yeyote inayomfanya asiihitaji matumizi hayo kutoka kwa mzazi wake, na hii ni sawa sawa awe binti huyo anavaa hijabu au havai. Na katika Upole wa Uislamu ni kuwa haujawajibisha kuondoshwa matumizi kwa sababu ya kuzembea utekelezaji wa mambo ya Faradhi, bali ni wajibu juu yake katika hali hii pia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas