Sharia inatuhimiza kudumisha usafi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Sharia inatuhimiza kudumisha usafi wa mwili wa mwanadamu

Question

Ni vipi Sharia inamhimiza mtu kudumisha usafi wa mwili wake?

Answer

Uislamu unahimiza usafi wa kinywa na meno kutokana na mabaki yenye madhara kwa afya ya binadamu. Mtume (S.A.W) Akasema: “Lau si kuogopa tabu kwa umati wangu, basi ningewaamrisha wapige mswaki kila wakati wa Swala”, Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na akatuongoza kwenye Sunnah za kimaumbile, kama kukata kucha na kusumua nywele za makapwa kunyoa nywele sehemu za siri. Kama katika hadithi ya Bibi Aisha, (R.A), amesema: Mtume (S.A.W) Amesema: “Mambo kumi ni katika sifa za kimaumbile: kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kuvuta na kutoa maji  puani na , kukata kucha, kusafisha makunjo viungoni, kuondoa nywele za makapwa kunyoa nywele sehemu za siri, na  kusukutua” Imesimuliwa na Muslim.

Share this:

Related Fatwas