Sharia ilihimiza usafi wa barabara
Question
Je, Sharia ilihimiza vipi usafi wa barabara?
Answer
Sharia ilihimiza usafi wa barabara, na ikaamrisha kutokojoa ndani yake, na kutupwa uchafu ndani yake. Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayra, (R.A), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) mesema: “ jiepusheni na sehemu mbili zinazopelekea mtu kulaaniwa” [Maswahaba] Wakauliza: Ni sehemu zipi hizo zinazopelekea mtu kulaaniwa? Akasema:
“Ni mtu kufanya haja katika njia wanazopita watu au katika vivuli wanavyoketi”
Pia alihimiza kuondoa madhara katika njia, na akaiona kuwa ni tawi la imani. Mtume (S.A.W) Amesema: “Imani ni zaidi ya mafungu sabini, imani kubwa ni kutamka shahada na ndogo ni kuondoa maudhi njiani na haya ni fungu katika imani.” Imepokelewa na Muslim.